Mathayo 19:1-11
1 Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo, akatoka Galilaya akafika mipaka ya Uyahudi, ng'ambo ya Yordani.
2 Makutano mengi wakamfuata, akawaponya huko.
3 Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?
4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.
9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
10 Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.
11 Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.
MAANA YAKE
Hutakiwi umuache mkewe isipokuwa kwa uasherati tu. Kama umemfuma kwa uasherati na ukavunja ndoa basi unatakiwa hudumie famili yako mtoto/watoto ukipendezwa na mkeo ila si kuingiliana kimwili. Kwasababu tayari umemuacha, hapo utakuwa umeoa mke mwingine ila kama umemsamehe hautakiwi kuoa mwanamke mwingine kwasababu unafanya uasherati (wazini).
Turudi kwenye mstari wako, hapa umeoa na ndoa yako haijavunjika na una mke mwingine. Ndoa inayotambulika ni ya yule ya mke wa kwanza tu (elewa). Ya mke wa pili utakuwa unafanya usherati kwahiyo unatakiwa uendelee kumhudumia mke wako wa kwanza kwa kila kitu na umtosheleze kwa mahitaji yake kwasababu ndiyo Mungu anayoitambua. Ila mke wa pili haitambuliwi na unafanya uasherati. Ukiamwacha ukahamia kwa mke wa pili bado unaendeleza ushaerati (wazini). Unatakiwa umhudumie mkeo wa kwanza kwa kila kitu.
Ndoa ya mke wa pili haijaruhusiwa ndiyo maana Mungu anatambua ndoa ya mke mmoja na mume mmoja ile ya kwanza na hutakiwi umuache. Mhudumie
Someni Biblia vizuri. Biblia haisomwi kama gazeti.