LUHALI
Member
- Sep 11, 2022
- 20
- 16
Mnakera mnaosema bibli
A haiosomwi kama gazeti mbona baadhi ya vifungu huwa hamsemi hivyoIsaya 4: 1
"Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu"
Ukisoma Biblia kama gazeti huwezi kupata maana kamili na utaishia kupata maana isiyo sahihi
Soma vizuri huo mstari mwisho unasema utoondelee aibu yetu? kwanini wanasema utoondelee aibu yetu?
Mungu hajaruhusu ndoa ya wake wengi, ameruhusu ndoa ya mke mmoja na mme mmoja tu. Amri kuu ya ndoa ilianza kwa Adamu na Eva kwenye bustani ya Edeni.
Mwanzo 2:22-25
"na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya"
Turudi kwenye mstari wako.
Huu mstari ni kama ilitabiriwa itakuwa hivyo ila haijaruhusiwa kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja.
Baada ya binadamu kuingia kwenye dhambi, akamuasi Mungu na kufuata matendo yao. Tamaa zikawa miongoni mwao ndiyo tunaona haki sawa kwa wanawake na mwanaume, wanawake wanataka mtu mwenye mali, hela, anajua kuoga, wanadanga, wanavaa nguo nusu uchi, wanaanza mapenzi wakiwa kwenye umri mdogo n.k
"Utakuta mwanamke anasema mimi naingiza milion 20 kwa mwezi na mwanaume anaingiza laki 5 kwa mwezi, unataka nikufulie nguo? Haiwezekani." Mwanamke kama huyu unaweza kumuoa? huwezi hata kumtuma akuletee maji ya kunywa. Ndiyo hao baadae watajikusanya wakitaka waolewe lakini watajihudumia wenyewe
Wanawake wanamali lakini matendo yao maovu na wamekosa watu wa kuwaoa kwasababu hawana sifa ndiyo unapata mstari utuondolee aibu yetu" Utakuta mwanamke anasema, nipe mimba nilee ili mradi tu awe na mtoto.
Jitahidini kusoma Biblia vizuri na haisomwi kama gazeti