Kutoka 21:10 huu ni uzinzi au ndoa ya mke zaidi ya moja ilikuwa halali?

Kutoka 21:10 huu ni uzinzi au ndoa ya mke zaidi ya moja ilikuwa halali?

Hakuna mafumbo bana vitu viko wazi,mkipewa msitari unaenda kinyume na Imani yenu mnaanza habari za roho mtakatifu,mafumbo
Unataka kuifuatisha biblia kama ilivyo?
Je unaweza kufuatisha sheria ya jino kwa jino na auaye kwa upanga sharti auawe kwa upanga?

Kuna sheria ziliwahusu Wayahudi pekee tena kwa wakati ule tuu.
 
Tena wanaume wakiuona watasema kumbe ni ruhusa kuwa na wanawake wawili😅
Mathayo 19: 8-1
8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.
9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
 
Kuna shida kubwa katika kutafsiri maandiko ya biblia, kuna maandiko mengi yapo kwenye biblia lakini hayasomwi makanisani. Mf kuhusu ndoa za mitara, kujichua nk.
 
Mathayo 19:1-11
1 Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo, akatoka Galilaya akafika mipaka ya Uyahudi, ng'ambo ya Yordani.
2 Makutano mengi wakamfuata, akawaponya huko.
3 Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?
4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.
9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
10 Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.
11 Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.
MAANA YAKE
Hutakiwi umuache mkewe isipokuwa kwa uasherati tu. Kama umemfuma kwa uasherati na ukavunja ndoa basi unatakiwa hudumie famili yako mtoto/watoto ukipendezwa na mkeo ila si kuingiliana kimwili. Kwasababu tayari umemuacha, hapo utakuwa umeoa mke mwingine ila kama umemsamehe hautakiwi kuoa mwanamke mwingine kwasababu unafanya uasherati (wazini).
Turudi kwenye mstari wako, hapa umeoa na ndoa yako haijavunjika na una mke mwingine. Ndoa inayotambulika ni ya yule ya mke wa kwanza tu (elewa). Ya mke wa pili utakuwa unafanya usherati kwahiyo unatakiwa uendelee kumhudumia mke wako wa kwanza kwa kila kitu na umtosheleze kwa mahitaji yake kwasababu ndiyo Mungu anayoitambua. Ila mke wa pili haitambuliwi na unafanya uasherati. Ukiamwacha ukahamia kwa mke wa pili bado unaendeleza ushaerati (wazini). Unatakiwa umhudumie mkeo wa kwanza kwa kila kitu.
Ndoa ya mke wa pili haijaruhusiwa ndiyo maana Mungu anatambua ndoa ya mke mmoja na mume mmoja ile ya kwanza na hutakiwi umuache. Mhudumie
Someni Biblia vizuri. Biblia haisomwi kama gazeti.
"Naye amwoaye yule alieachwa azini" : Katika maelezezo yako hapo chini ni kama yamejichanganya . Mimi nilivyoelewa mwanamke akichwa kwa sababu ya uasherati akiolewa tena basi yule aliyemuoa azini .
 
Mathayo 19: 8-1
8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.
9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
Hii naijua hii🤔
 
Ndiyo maana mnakuja na maana tofauti. Biblia inatakiwa isomwe na watu wenye utulivu wa akili kwasababu ukisoma nje ya hapo utakuja na maana ambayo watu watabaki wanakushangaa.
Ngoja nikurudishe shule kidogo.
Shuleni tulikuwa tunaulizwa kilo moja ya manyoa na kilo moja ya mawe ipi ni nzito? Gari ilipata ajali mpakani mwa Kenya na Tanzania majeruhi watazikwa wapi?
Unaposema Biblia unatakiwa uwe na utulivu wa nafsi.
Isaya 4: 1
"Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu"
Hapa ukisoma juu juu lazima uchangayikiwe lazima ujiulize tuondolee aibu yetu, aibu gani?. Huu mstari unahusu nini, ulianzia wapi? kwanini wanawake 7 wamekusanyika waende kwa mwanaume mmoja? sababu ni ipi wanawake wamekuwa wengi au? Hayo majibu yote yapo kwenye Biblia.
Sasa hapo Kuna fumbo!?..we ni punguwani,kitabu kimeandikwa na watu zama za mawe za kati wawe na mafumbo mtu wa Karne ya sayansi na tek ashindwe fumbua!!..acha ujuha
 
Unataka kuifuatisha biblia kama ilivyo?
Je unaweza kufuatisha sheria ya jino kwa jino na auaye kwa upanga sharti auawe kwa upanga?

Kuna sheria ziliwahusu Wayahudi pekee tena kwa wakati ule tuu.
Biblia ni kitabu Cha wayahudi,na Sheria ni hiyo ukiua uuawwe,ukimtoa mwenzio jino nawe utolewe,siyo uue Kisha uachwe unaburuza tu korodani zako duniani,patakua na wauaji wengi
 
Ndiyo shida ya kusoma Biblia kama gazeti. Biblia imeandikwa kimafumbo inabidi utulize akili ili upate maana kamili. Tafuta nyoka au nge umkanyage kwasababu umepewa mamlaka

Luka 10:19​

" Nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na kushinda nguvu zote za yule adui; wala hakuna kitu cho chote kitakachoweza kuwadhuru".​

Hahaha mimi sio kondoo mkuu tafuta kondoo uwashike masikio.
 
Ndiyo shida ya kusoma Biblia kama gazeti. Biblia imeandikwa kimafumbo inabidi utulize akili ili upate maana kamili. Tafuta nyoka au nge umkanyage kwasababu umepewa mamlaka

Luka 10:19​

" Nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na kushinda nguvu zote za yule adui; wala hakuna kitu cho chote kitakachoweza kuwadhuru".​

Sasa kwa nini iandikwe kwa mafumbo? Lengo la kufumba ni nini?
 
Back
Top Bottom