Google chrome
JF-Expert Member
- Nov 26, 2017
- 2,276
- 12,780
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
huyu bwana ajawahi kuwa msomi, huyu ni mpumbavu aliye pita pita shule ila hakufanikiwa pata kitu kichwani japo alipata makaratasi ya kumtambulisha alipita shuleHawa ndio hazina ya wasomi wa Tanzania.
Mkuu sio mawazo.yake hayo ni mawazo yao!Maamuzi mengine wana force kwa Mkono wa Chuma Mkuu ,una fikiri ktk Nchi zinazo jitambua unaweza kupata Kiongozi kama huyu ?
Ndio nasema si mawazo yake hayo bali ni mawazo yao! Hawa ndio wanaosababisha ghasia katika nchi zetu za kiafrika mapinduzi na uasi kila kukicha
Kwani ile Bar ni yake? si pale relini?Ameongea hayo akiwa ametoka kwenye ile bar yake Titanic pale Vingunguti?
Sent using Jamii Forums mobile app
This shit is castrated! SimbachaweneNimesikiliza angalau kipande cha mchango wa Ndugu George Simbachawene kuhusu muswada wa sheria ya vyama vya siasa,nilichokigundua sasa ipo hoja inapazwa kwa kasi kuwa.....
1.Kufa kwa viwanda nchini Tanzania ni sababu ya uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu mfumo wa Vyama vingi nchini.
2.Kufa kwa Mashamba makubwa yaliyotoa ajora za kutosha ni kwa sababu ya uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu mfumo wa Vyama Vingi nchini.
3.Uwekezaji ambao haukuwa na tija kwa taifa letu kulisababishwa na uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu Vyama vingi.
4.Tatizo la ajira nchini ambalo linakuwa siku baada ya siku limesababishwa na mfumo wa Vyama vingi nchini.
5.Kashfa kubwa za Rushwa kama EPA,Escrow,Richmond,Meremeta,Dowans n.k zilisababishwa na nchi kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi.
6.Kufa kwa Shirika la Reli,Shirika la Ndege/Anga kulisababishwa na uamuzi wa mwaka 1992 wa kuanzisha mfumo wa Vyama vingi.
Ndiyo maana George Simbachawene anasema nchi kama China ina chama kimoja tu na uchumi wake sasa ni imara.
Simbachawene anatamani Tanzania tubaki na chama kimoja ili tujenge taifa lenye nguvu duniani.Sijui kwa nini George hajatumia mifano ya mataifa ambayo yameendelea na yana mfumo wa vyama Vingi?
George Simbachawene ambaye kama sikosei aliondoshwa kwenye Wizara ya Madini na Mh Rais kutokana na kutuhumiwa na Kamati ya Mh Rais ile ya Makanikia,anasema huko nyuma nchi ilikuwa kwenye presha muda wote na akataja harakati kama..
1.Movement for Change
2.Oparesheni Sangara n.k
Kwa mtazamo wa Ndugu Simbachawene,harakati hizi zilichangia kuchelewesha maendeleo nchini.
Nakumbuka harakati hizi zlikuwa zinapiga kelele dhidi ya hiki anacholia nacho Mh Rais Magufuli kila kukicha,wizi,Rushwa,kujilimbikizia mali,Uwekezaji wa hasara.
Je Simbachawene anataka kusema Vyama vya upinzani vingekaa kimya wakati Buzwagi wanawasainisha mawaziri wetu mikataba mibovu hotelini?
Je Simbachawene anasema Vyama vya Upinzani vingekaa kimya wakati baadhi ya Mawaziri,wafanyabiasha na watumishi wa Umma wanagawana pesa za Escrow kwenye sandarusi?
Je Simbachawene alitaka Vyama vya Siasa vikae kimya wakati wakazinwa Nyamongo wanateseka na maji yenye sumu kutoka mgodi wa North Mara,wanapigwa Risasi na wawekezaji?
Je Simbachawene alitaka Vyama vya upinzani vikae kimya wakati wawekezaji kwenye migodi walipojigeuza miungu watu(wasiguswe),walipokuwa wanawahakisha wenyeji kinyama tena usiku wa manane bila fidia?
Je Simbachawene alitaka Vyama vya upinzani vikae kimya wakati wawekezaji hawa walipokuwa wanachimba madini bila kulipa kodi?huku suala la mapato wakilifanya kuwa ni Siri kati yao na Serikali
Je Simbachawene alitaka vyama ya upinzani vikae kimya wakati Twiga wanahamishwa kwenda nje kwa ndege?wanyama wanauwa na wawindaji haramu?
Je Simbachawene alitaka watu wakae kimya huku kuna watumishi wa Umma walikuwa wanakula mishahara hewa?
Je Simbachawene alitaka wapinzani wakae kimya wakati baadhi ya Viongozi wetu wakuu walipoamua kujiuzia mpaka migodi ya madini?
Yaani haya yote,adhabu yake ni kuwazuia wanasiasa wasiseme chochote mpaka wakati wa uchaguzi na wakikaidi Msajili anawafuta katika wigo wa Siasa?
Kwa nini tusitunge Sheria ambazo zitakuja kuwafanya Watanzania wazidi kuwa wamoja zaidi bila kujali tofauti zao za kisiasa,kidini,kikabila na hata kimtazamo?
Kwa nini baadhi yetu kila siku tunawaza kutunga Sheria ambazo zinalenga kubinya haki za wengine?
Kwa nini tufikirie kutunga Sheria ambazo zinatengeneza hofu badala ya Ujasiri?
Mambo haya yanatafakarisha sana sana.