Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

ITV Arusha ni mngurumo tuu kupitia cable, Itv tumewaambia tumechoka, hata bila ilani kura ni ukawa, tumeichoka ccm
 
Mh Lowassa nimekubali hii sera ya kulinda ajira za watanzania na kuwapa kibaumbele.

Kwa walio kwenda china hii sera china inahitumia sana. China wana sera hii uwez kuta mgeni anajafanya kazi za ovyo ovyo kama hapa kwetu Tanzania.hii sera chadema Bigup sana.sasa mmepata kura yangu!!!!
 
Usijidanganye dunia nzima hakuna rais au mkuu yeyote wa nchi ambaye hawezi kujieleza kwa watu anaotaka kuwaongoza iwe marekani au uingereza. Tanzania itakuwa nchi ya kwanza duniani kufanya hivyo. By the way mkuu umewahi japo kwa kidogo kufuatilia chaguzi kama za us na uk? Kama umewahi utanielewa ninachozungumza.

Tunaishi kwenye dunia ya tatu isiyokuwa na demokrasia ambapo viongozi wanatawala na kungángánia madaraka kwa kutumia mabavu. Huwezi kulinganisha uchaguzi wa US au UK na kinachotokea hapa. Hao madikteta wanaopindua nchi huwa wanajua kijieleza kwa watu wao? Kupanda jukwaani na kuita watu malofa na wapumbavu ndio kujieleza?
 
Staili safiiiiii ya aina yakeeee!!! Lowasa=mabadiliko...mabadiliko=Lowasaaaaaa
 
Yuko ITV anataja vipa umbele vyake,vimeshiba kweli kweli na sio porojo za mapimb.i wa CCM!
 
HATIMAYE HAKI ZA RAIA KUWEKWA REHANI NA Mzee Lowassa



Uraia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania una haki zake zilizoainishwa kikatiba ambapo kila raia wa kundi lolote la jamii ana haki zote zinazofungamana na uraia wake.



Kinga ya haki za kiraia na kijamii ni katiba ya nchi. Kiongozi anaweza kuwa na nafasi yake katika dhamana ya utawala lakini yeye kama yeye hawezi kuwa hakikisho la haki za raia.



Hivi sasa Nchi imeingia katika kampeni za kumchagua Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni kampeni zitakazochukua takribani miezi miwili.



Katika kipindi hicho, wagombea, kupitia Vyama vyao mbalimbali, wananadi Ilani zao ambazo zitajumuisha ahadi mbalimbali pamoja na sera. Wagombea watakuwa na ahadi nyingi lakini lazima izingatiwe kuwa hawatatenda mambo kinyume na katiba.
Ni vipi sasa wafungwa waachiwe bila utaratibu kisa mzee kawa rais?


Mgombea yoyote hawezi kuaminika kwa ahadi kuwa yeye atawafanyia watu mambo ambayo yatakuwa kinyume na sheria mama. Tangu hapo, raia hawapaswi kutenganisha ahadi za mgombea na katiba ya nchi.



Haki zote za kiraia zilizoainishwa kikatiba hazipaswi kunadiwa wala kuwekewa ahadi na mgombea kwa sharti la kumpigia kura. Haki hizo za kijamii hazihitaji ahadi za mgombea bali zinahitaji kutekelezwa na yoyote yule atayeshinda kikatiba.



Kwa maneno mengine, Rais yoyote kutoka chama chochote cha siasa ana wajibu wa moja kwa moja wa kikatiba kutimiza haki za kiraia na kijamii za kila raia na kila kundi la jamii pasipo kutazama dini yake.



Waislamu, kama jamii, hawahitaji kuzifungamanisha haki zao za kikatiba au kisheria na ahadi za wagombea kisa urais.Je ni waislamu wangapi watanufaika na uvunjifu huo wa kikatiba? Kufanya hivyo kunaziweka hatarini haki zao kwani hakuna uhakika wa moja kwa moja kwamba mgombea huyo atashinda au la!



Maadam Jamii ya Waislamu na wakristo ina hakika kuwa haki zao za kiraia, kijamii, kisheria na kadhalika zote zina dhamana ya moja kwa moja ndani ya Katiba ya nchi, basi Mgombea asijaribu wala kuthubutu kuomba kura kwa ahadi ya kutimiza jambo lolote ambalo, tangu hapo, litakuwa ni sehemu ya wajibu wake wa kiutawala.



Atoe ahadi, asitoe ahadi, bado wajibu wa serikali ni kutimiza haki za kikatiba za raia. Uislamu na Ukristo utabakia palepale.


Hatari hiyo ni ile ya kujaribu kuitazama karatasi ya kura kama nusra ya jamii yao. Ukubwa wa hatari hii haupo tu katika ukweli kuwa kiongozi anayeaminiwa anaweza kwenda kinyume na ahadi hiyo, au chama chake kumkwaza, bali anaweza kushindwa uchaguzi, na kuwaacha Waislamu mikononi mwa yule ambayo hawakuwa na ahadi naye.


Mathalani, Waislamu wakisema kuwa watampigia kura mgombea wa chama fulani ili eti awatoe Waislamu waliofungwa jela kwa mashitaka mbalimbali, swali linalowarudia, ni je, akishindwa uchaguzi ndiyo ina maana Waislamu waliondani waendelee kukaa huko?



Achilia mbali hilo, ni mgombea gani ambaye anaweza kuchukua ahadi ambayo itakuja kukinzana na matakwa ya sheria? Ifahamike kuwa Uchaguzi wa Rais haufuti sheria wala hauondoshi majukumu ya Majaji na Mahakimu katika kutoa tafsiri ya sheria na hukumu.

Utakuwa utapeli wa kisiasa kwa mgombea kutoa ahadi ya jambo ambalo litakinzana na matakwa ya muhimili mwingine wa Dola. Tafsiri za sheria za Mahakama Kuu na zile za Mikoa na Wilaya zitabaki palepale licha ya mabadiliko ya Uongozi wa Kitaifa.



Jitihada za kisheria ziendelee kufanyika katika kukabiliana na tafsiri za sheria za Wanasheria wa Serikali bila kusubiri Oktoba, wanasiasa wenye hoja kutugawa wanapaswa kupewa ONYO KALI.

WAPIGA KURA WASIKUBALI KUBULUZWA,WATUMIE HAKI ZAO ZA MSINGI KUCHAGUA KIONGOZI ATAKAYE KUWA NA TIJA KWA WATANZANIA WOTE.
 
Baada ya uzinduzi nimelazimika kufuata maelekezo ya mgombea kwamba ilani ipo kwenye website ya chadema ambayo ni Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo – Chadema kusema ukweli haipo. kuna tab ya nyaraka+ ukiingia kuna link ya ilani ya uchaguzi but ukiingia inakupeleka kwenye fomu ya kugombea ....

Pia nimewasili kwenye blog ya chadema Chadema Blog pia mbali ya picha hakuna ilani.....

hakuna ilani wala hotuba!!!

wakuu mwenyenayo please naitafuta...

Webadmin wao alichukua likizo kitambo!
 
Tunaishi kwenye dunia ya tatu isiyokuwa na demokrasia ambapo viongozi wanatawala na kungángánia madaraka kwa kutumia mabavu. Huwezi kulinganisha uchaguzi wa US au UK na kinachotokea hapa. Hao madikteta wanaopindua nchi huwa wanajua kijieleza kwa watu wao? Kupanda jukwaani na kuita watu malofa na wapumbavu ndio kujieleza?
Nasikitika umeshindwa kuielewa hoja yangu mwana ukawa.usiku mwema
 
CCM HAWANA SERA ZA KUMKOMBOA MTANZANIA MASIKINI, sera za kweli zipo UKAWA,na sio matusi na mipasho kama ile ya wazee wa CCM.
 
Unapoandika thread humu uache bias ili ujumne ufike kwa walengwa na waupokee na wauchambue ili UPATE MAJIBU HALISI NA SIO YA KINAFIKI. Vipaumbele vya Taifa sema wewe ndio huvifahamu usiseme watanzania hawafahamu. Alafu Lowassa angetanguliza katiba nngemuona mjanja ila kwa uzembe wake anasema elimu wakati vituvingine kwenye elimu vingkua bora zaid kama angerekebisha katiba kwanza.

alafu mnapoiponda CCM mara zote kua inaahidi vitu vilevile kwani leo mmeongea nini kipya? au kufungua wafungwa na kufufua wafu ndio kipya?

Lowassa ni mnafiki kwa sababu watanzania siku zote wanaimba wimbo wa balali kwanini asingejitokeza aseme kama anajua balali alipo? Leo ili kuawahaada wananchi anawaambia nitalishughulikia. Tunahitaji sera na sio ahadi za mipira yenye sura yako, kufungua wafungwa na kufufa wafu.

Tatizo nimeichoka ccm sio mtu
 
Tunaishi kwenye dunia ya tatu isiyokuwa na demokrasia ambapo viongozi wanatawala na kungángánia madaraka kwa kutumia mabavu. Huwezi kulinganisha uchaguzi wa US au UK na kinachotokea hapa. Hao madikteta wanaopindua nchi huwa wanajua kijieleza kwa watu wao? Kupanda jukwaani na kuita watu malofa na wapumbavu ndio kujieleza?

Achana na hawa vibaraka wa CCM,wao na sera zoote kwenye ilani yao kwa miaka zaidi ya 50 imewasaidiaje watanzania masikini?
 
Hatutaki mboyoyo mingi. Hatutaki watu wanapiga sound mpaka wanaanguka jukwaani
 
Back
Top Bottom