Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Pipozzzzz,,, kazi kweli kweli,,,, nafikili mgombea urais ukawa ni SUMAYE,,,
 
Baada ya uzinduzi nimelazimika kufuata maelekezo ya mgombea kwamba ilani ipo kwenye website ya chadema ambayo ni Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo – Chadema kusema ukweli haipo. kuna tab ya nyaraka+ ukiingia kuna link ya ilani ya uchaguzi but ukiingia inakupeleka kwenye fomu ya kugombea ....

Pia nimewasili kwenye blog ya CHADEMA Chadema Blog pia mbali ya picha hakuna ilani.....

Hakuna ilani wala hotuba!!!

wakuu mwenyenayo please naitafuta...
 
Bora ujaribu kuwaelimisha waliofunikwa na magamba mpaka kwenye upeo.
 
.
NI Usanii pale Mbowe kaufanya kujifanya Kingmakerkwa kulamba pesa za #FisadiLowassa wakati anajua kwamba hana uwezo wa kiafya! La pili alilotupiga chenga ameshindwa kutuambia #Lowassa anampiku kivipi #Dr.Slaa kupeperusha bendera ya Chadema? Kwanini anacheza na akili ya mgonjwa kumfurahisha kwa gharama ya demokrasia na hatima ya watanzania? Kweli tuchague rais mwenye afya yenye mgogoro wa kiafya uliopitiliza itakuwa kwa faida ya nani? Eeh Mola tawala! Tuepushe na huu usanii

Kweli umati ule wooote umekuja kumfurahisha mgonjwa.......hawa si ndio wanaoitwa wapumbavu na malofa.....wamekuja kumsapoti lofa mwenzao, mgonjwa mwenzao...lofa mwenzao....mpumbavu mwenzao.....wale wazima wa akili wasio malofa kazi kwako sasa.....malofa ndio hao wameshaanza kukusanyana...wakiendelea hivi sijui tarehe 25 oct itakuwaje?
 
Sumaye kumbe mtupu kiasi hiki yupo kundi moja na kina Tambwe Hizza, kulikuwa hamna haja ya kuongelea ugonjwa wa Lowassa, umewapa pakusemea kina Lusinde, nampa pole sana Lowassa, Sumaye kamtafutia matatizo...daah
 
Siyo tu Watanzania kushangaa mgonjwa kupeperusha bendera ya chama chao; ila ajabu zaidi imejitokeza baada ya mgombea huyo kuwaambia wananchi wakasome ilani yake kwenye tovuti ya chama hicho. Baada ya muda mfupi yalijitokeza maajabu mengine pale alipowataka watu wa dar wakamuombee kura kwa watu wa bara

Hii ni ajabu ya mbalamwezi kuanikia muhogo, watu walipolalamika kuwa mgombea hafai na ni mgonjwa mlijitokeza kumtetea kwa nguvu zote. je, mnayaona haya? sasa wapiga kura tumeshaamua hatutomchagua kamwe
#hapakazitu

toa bori kwenye jicho lako kabla hujatoa kibanzi kwa mwenzio, vp munarusha mawe ili hali mupo kwenye nyumba ya vioo mumesha saha mara hii 2010 kuna mgombea alikuwa anadondoka majukwaani nashukuru sumaye kesha waeleza ukweli wenu
 
mimi ni ukawa damdam pia namkubali saana lowasaa na kura yangu kashaipata kitambo kwasababu lowassa ni mtendaji na mfatiliaji mkubwa wa mambo ila shida moja tuu ni kwamba kwenye speech jamaa bado hajajipanga vizuri.. ombi langu ni moja tuu kwa viongozi wa ukawa ebu tujaribu kumpanga mzee vizuri kwenye speech...bse wananchi wanaitaji kusikia sera ya chama yoote na sio summary

mkuu tabia za watendaji. Sio waongeaji kama kasuku, hilo ulifahamu mkuu,

hata YESU alisema maneno yenu yasiwe mengi.

Watanzania kwa sasa hawahitaji ngonjera wanahitaji matendo.
 
Ilani ya waka huu ya UKAWA no kimtoa babu Sega kumfufua balali na kuwaachia mashehe hahahahaha chama kimeshauzwa sasa hivi sio tena CHADEMA chama cha mabadiliko ila no lowasa na mabadiliko!!chama kimeuzwa hicho mtasubiri sana mwaka huu
 
Hebu tujikumbushe yalio tokea leo Jangwani na yaliyo semwa na Loassa mgombea wa Ukawa aka Chadema.

1: Lowassa amesema atamtoa Babu Seya akiwa Rais. Je huko sio kuingilia utawala wa sheria? Je ana uhakika gani alisingiziwa? Hivi ndio vipaumbele vya serikali kwenye nchi yenye matatizo kiasi hichi? Tokea lini Lowassa amekua hakimu? Je, na wafungwa wengine atawaachia huru?
2: Lowasa kasema atatuletea/kumfufua Balali, sasa najiuliza si watuambie leo hii yuko mji gani ama nchi gani na kwanini asubiri awe raisi ndio watuletee Balali? Hichi nacho ni kiapumbele? Au hii ndio ilani ya UKAWA?
3: Lowasa kasema eti, elimu itakuwa bure! Kuanzia primary-University lakini ameshindwa vibaya sana kusema fedha zitatoka wapi? Hivi, wakati wa Nyerere nani alilipia elimu?
4. UKAWA wamekiri wao ni ma lofa kutokana na t-shirt walizotengeneza na kuuza uwanjani lakini hapo hapo wameambiwa wakasome hotuba ya mgombea Urais mtandaoni je kama ni kweli ni ma lofa wana access ya internet? Kulikuwa kuna aja gani ya mkutano kama mngeweka vitu vyote online? Vipi kuhusu wazee wa Mashambani, nao waingine dot com kusoma ilani?
5. Ukawa wametuhakikishia kuwa hawana sera wala ilani zaidi ya kufukuza upepo.
6. Ukawa wamebakia kumjibu Mtaafu Rais Mkapa ambaye aliwateka Kisaikologia na kuwa gumza la Ukwa leo Jangwani.


11951204_1068783333154019_992321555451370143_n.jpg




Anza kwa mtiririko kama alivyosema yeye! Mabango ya kumtoa babu Seya kasema 'nimeona na nitashughulikia'
 
Back
Top Bottom