Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Hebu tujikumbushe yalio tokea leo Jangwani na yaliyo semwa na Loassa mgombea wa Ukawa aka Chadema.

1: Lowassa amesema atamtoa Babu Seya akiwa Rais. Je huko sio kuingilia utawala wa sheria? Je ana uhakika gani alisingiziwa? Hivi ndio vipaumbele vya serikali kwenye nchi yenye matatizo kiasi hichi? Tokea lini Lowassa amekua hakimu? Je, na wafungwa wengine atawaachia huru?
2: Lowasa kasema atatuletea/kumfufua Balali, sasa najiuliza si watuambie leo hii yuko mji gani ama nchi gani na kwanini asubiri awe raisi ndio watuletee Balali? Hichi nacho ni kiapumbele? Au hii ndio ilani ya UKAWA?
3: Lowasa kasema eti, elimu itakuwa bure! Kuanzia primary-University lakini ameshindwa vibaya sana kusema fedha zitatoka wapi? Hivi, wakati wa Nyerere nani alilipia elimu?
4. UKAWA wamekiri wao ni ma lofa kutokana na t-shirt walizotengeneza na kuuza uwanjani lakini hapo hapo wameambiwa wakasome hotuba ya mgombea Urais mtandaoni je kama ni kweli ni ma lofa wana access ya internet? Kulikuwa kuna aja gani ya mkutano kama mngeweka vitu vyote online? Vipi kuhusu wazee wa Mashambani, nao waingine dot com kusoma ilani?
5. Ukawa wametuhakikishia kuwa hawana sera wala ilani zaidi ya kufukuza upepo.
6. Ukawa wamebakia kumjibu Mtaafu Rais Mkapa ambaye aliwateka Kisaikologia na kuwa gumza la Ukwa leo Jangwani.


11951204_1068783333154019_992321555451370143_n.jpg



Nenda kule hamtubadilishi ng'oo
 
Ainingii akilni mtu aliyetuhumiwa kwa ufisadi etiii leo anikomboe,
Mh. Sumaye amekuwa waziri mkuu miaka 10 etiii leo mkombozi, ameshindwa kutukomboa pindi yupo madarakani na akiwa mtendaji mkuu wa serikali, leo hii atatukomboa etiii.
Mkombozi wa kweli ni Mungu pekeee tu.

hayo ni maoni yako siyo ya watz nenda kakombolewe kwa mafisadi wa ccm siku ukijielewa uje ukawa
 
Licha ya kadhi, huyo hata aseme ataifanya Tanzania kuwa nchi ya Kiislam kura hatumpi. Unafikiri tumesahau kuwa yeye ndiye alisaini MoU?

Huyo hana kura isipokuwa za wapumbavu na malofa tu, akina Ku Klux Klan Tanzania.

Kwanza zezeta hilo.

Sijawahi ona mwanamke ning'ini'a kama huyu
 
Mkuu alisema kutokana na muda ataweka hotuba yake kwenye blog hiyo.sio ilan ya uchaguzi pili aliposema ataiweka haikua namaana kwamba ataiweka muda ule subir
 
Kuhusu masheikh na babu seya ndio Kasema atawashughulikia na atawatoa... Kwa upeo wa haraka hawakustahili kuwapo kule walipo sasa... Tumia akili unapotoa post usiwe wakurupuka kama Mkapa

Mahakama imeona wanahatia yeye ni nani mpaka awatoe kama wangekuwa hawana hatia wangekua huru sasa,"eti kwa upeo wa haraka hawakustahili kuwepo kule walipo sasa" hivi kweli muhalifu mbakaji,mlawiti na mchochezi wa uhalifu leo umuache awe huru hivi anaakili kweli?
 
mimi ni ukawa damdam pia namkubali saana lowasaa na kura yangu kashaipata kitambo kwasababu lowassa ni mtendaji na mfatiliaji mkubwa wa mambo ila shida moja tuu ni kwamba kwenye speech jamaa bado hajajipanga vizuri.. ombi langu ni moja tuu kwa viongozi wa ukawa ebu tujaribu kumpanga mzee vizuri kwenye speech...bse wananchi wanaitaji kusikia sera ya chama yoote na sio summary

Uzinduzi wa Kampeni. Kagusia baadhi tu ili kuendana na muda. Wakat wa kampeni atazungumzia yote!
Hata leo magufuli kaongelea suala la masoko ya Tumbaku lakini wakat ule hakugusia siku ya uzinduzi!
 
Lowasa ni mwanasiasa wa kutumia pesa hana hoja wala hana siasa za hoja yeye ni rushwa tu.
nyie wenye hoja na sera mmetufanyia nini?? Zaidi ya kushibisha tumbo zenu zisizoshibaaa!! Waongea kama nyinyi Mara nyingi Ni matapeli na mmetutapel vya kutosha sasa imetoshaaaaaaaaaaa
 
Jamani uzinduzi murua sana, sunaye aligongelea msumari wa mwisho kwenye jeneza la magamba, lowasa katoa vipaumbele ilani itaendelea kutolewa kwenye kampeni kila kona....hatutaki porojo, tunataka vitendo.
 
Licha ya kadhi, huyo hata aseme ataifanya Tanzania kuwa nchi ya Kiislam kura hatumpi. Unafikiri tumesahau kuwa yeye ndiye alisaini MoU?

Huyo hana kura isipokuwa za wapumbavu na malofa tu, akina Ku Klux Klan Tanzania.

Kwanza zezeta hilo.

Matusi ndio kawaida yako, hakuna demokrasia ya kumkataa mtu kwa matusi, wewe ni ndio zezeta tena unahatarisha amani.
 
Kuwa mahiri jukwaani si uthibitisho wa kuwa kiongozi bora. Lowassa anazo sifa nyingi na tunazifahamu lakini ntakupa sifa moja tu ambayo hamna kiongozi yeyote wa CCM anayo. UTHUBUTU.

Kikwete ni hodari sana jukwaani ila utendaji ni sifuri.
 
Back
Top Bottom