Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Leo ndiyo nimeamini kabisa maneno ya Mkapa, tena na mimi nnaongezea, licha kuwa ni wapumbavu wanaoshadidia lile gonjwa lichaguliwe, pia ni mazumbukuku na mapunguani wa hali ya juu.

Jana kajidai ataongea akiwa amekaa kwa kuwa yeye "mrefu" sana, mikono akashindea kunyanyua kusalimiana na wasanii, leo wamemweka aongee dakika za majeruhi ili avunge muda hautoshi.

Hivi hawa watu wa aina gani jamani?

Kwa niliyoyaona, 100% Mbowe kapiga pesa na anajuwa huyu hafai, wanachofanya pale ni maigizo ya kumridhisha tu kuwa waashalamba mshiko.

Najaribu kufikiria huyu mtu kweli angegombea kupitia CCM tungemtetea vipi?

Unatumia nguvu nyingi sana dada yangu, mumeo ana kazi.
 
Na Bado! Ukawa ina watu wachache sana ambao magamba mnawapigia kelele! Sumaye leo kadokoa kidogo tu, mnalialia, hamjajipanga? Haya sasa na Tambwe Hiza kaingia, mtavuliwa nguo mpaka mkome! Mafisadi wote mmejaa CCM!
 
mimi ni ukawa damdam pia namkubali saana lowasaa na kura yangu kashaipata kitambo kwasababu lowassa ni mtendaji na mfatiliaji mkubwa wa mambo ila shida moja tuu ni kwamba kwenye speech jamaa bado hajajipanga vizuri.. ombi langu ni moja tuu kwa viongozi wa ukawa ebu tujaribu kumpanga mzee vizuri kwenye speech...bse wananchi wanaitaji kusikia sera ya chama yoote na sio summary
 
Mazoea bana, hotuba Masaa 3...meli kila ziwa, Singapore kila Kanda nk...then ubwabwa..

Hii Karne mpya, mambo mapya na waachieni Ukawa, nyie Sumaye kawavua sasa fast jet itabidi akalazwe tena lol

Yaani msemo wa watu wa DSM niombeeni kura Bara ni ajabu ? Hamjui wengi vijijini wa naulizia na ku taka ushauri wa ndg zao wa mijini? Au mnadhani alimaanisha haendi Bara ??
 
"Watanzania wanahtaj mabadlko, wacpoyapata..." leo hii nchi yeny raslimal nying watoto bado wanakaa sakafun mashulen, tunaish Tz km tumeazimwa. UKAWA 2naingia ikulu
 
Siyo tu Watanzania kushangaa mgonjwa kupeperusha bendera ya chama chao; ila ajabu zaidi imejitokeza baada ya mgombea huyo kuwaambia wananchi wakasome ilani yake kwenye tovuti ya chama hicho. Baada ya muda mfupi yalijitokeza maajabu mengine pale alipowataka watu wa dar wakamuombee kura kwa watu wa bara

Hii ni ajabu ya mbalamwezi kuanikia muhogo, watu walipolalamika kuwa mgombea hafai na ni mgonjwa mlijitokeza kumtetea kwa nguvu zote. je, mnayaona haya? sasa wapiga kura tumeshaamua hatutomchagua kamwe
#hapakazitu

Umesema huasikia sera, halafu tena ghafla unasema umesikia sera ya elimu, elimu, elimu..
Sasa mbona unajichanganya,...? Kumbe umesikia, ila basi tu ajira inakubana..!!
 
Kwamtoro - ikiana! Unamwelezaje Mh Sumaye kukana wajibu na madaraka ya Waziri Mkuu! Unamwelezaje huyohuyo Mh kuisema vibaya serikali aliyoitumikia akiwa yeye ni kiongozi wa pili toka juu!

Angaa waree! Sumaye amefanya kitu ambacho asingeweza kukifanya pindi akiwa kwenye system. Ametuambia ukweli ili uma wa Watanzania umuelewe. Uzuru Sumaye ni mkweli
 
Kutekeleza ilani 100 ndani ya miaka 5 nayo inahitaji muujiza. Wakati huo huo kufufua habari za 'marehemu', kufungua kesi zilizofanyiwa maamuzi na 'vyombo vya sheria' inaweza kuwa ni sehemu ya kuonyesha dalili ya kisasi. Tuombee amani nchi yetu.
 
mimi ninawashangaa sana wanaccm. Mnatia haibu kabisa.

Mlitaka lowassa aongee nini?
wacheni wivu wakijinga, kama ninyi chaguo lenu ni magufuli, basi kuweni wa staarabu,

cctumesha hamua kumchagua lowassa, mtasema sana lakini mwisho wa siku nchi lazima ipate kiongozi bora na sio mtawala,

Wanataka aongee kama Magufuli.....ndio kipimo chao......
 
Short and clear.hatuhitaji maneno mengi tunataka utekelezaji .tunahitaji mabadiliko sio wingi wa maneno tumrsikia sana lakini hadi sasa yamebaki kwenye kumbukumbu maktaba.
 
bado nina imani sana na lowasa. elimu bure toka primary mpaka chuo kikuu..
Mkuu unaweza kunifahamisha hiyo ni ilani ya Chadema au mawazo binafsi ya Lowassa isije kuwa drama kama ile ya mvua za Thailand.
 
Mkuu kama umemfuatilia vizuri Lowasa kwa hizo dakika mbili alizoongea, utaona hakuweza kuainisha strategies zozote zenye mashiko za kuinua nchi. Sana sana, ameleta stori za udaku tuu......!!! Obviously, uwezo wake wa kujenga hoja za msingi ni mdogo sana.!!!!!!! Hicho ndo watanzania walichoona leo

Mkuu mimi kuna siku niliwaambia hapa jamani lowassa ni mwepesi sana kichwani (kilaza) watu wakanijia juu nashukuru leo watanzania wamejionea.
 
Back
Top Bottom