Kusema kweli viongozi wengi wa Tanzania hasa wa ccm huwa na maneno mengi, kwa kujinadi hawajambo lakini utekelezaji ndio sifuri, nimefurahishwa sana na hotuba ya mheshimiwa lowassa ilivyo fupi na yenye kutekelezeka, kuna watu huwa wanaelewa lakini wanajifanya hawaelewi, ni mambo mengi ambayo lowassa amekuwa akizungumzia tangu ahamie ukawa katika mikutano yake, haikuwa na haja kurudia yote sababu alishayaanisha. Kusema kweli, hata ukijaribu kutafiti, wale watu ambao huwa hawaongei sana huwa wanafanya kwa vitendo ili kumaanisha wanachotaka kusema. Haimaanishi kuongea sana ndio utekelezaji. Mimi kwa kweli nimechoka porojo za mitandao ya kijamii, nimeamua kujiunga ukawa niongeze nguvu ya kura yangu ata kama ni moja tu najua ni moja kati ya milioni moja. Jamani mzee wa watu muacheni kabisa, watu wanamkejeli kwa kuwa aliongea kuhusu babu seya, masheikh na balali. Hizo hazikuwa sera zake, mimi nilikuwa pale mbele, ni maneno ambayo alilazimika kuyasoma kwenye mabango baada ya kuona hao wenye mabango hapo mbele wanamshangilia kwa furaha ili tu ayaone na ndipo alipoamua kuyasoma. Kwa mtu ambaye si timamu na si mpenda mabadiliko ataona kuwa zile zilikuwa ni sera, na isitoshe asilimia 80 ya sera ambazo alitakiwa lowassa aongee zalishaongelewa na viongozi waliotangulia, na ikiwa ni kuhusu kashfa, sumaye alishamaliza. lakini hapana. Kama humtaki lowassa, mkatae mwenyewe, kumbuka kura hupigi mwenyewe. Huku mtagombana bure, mtabishana bure, utachoka bure, huku kuna watu akili zao zimelala, lakini ni wenzetu tu hatuwakai wala kuwasema kwa ubaya, Ni basi tu kwa kuwa ndio asili yetu.
Ni heri ujaribu upinzani kwanza, ikiwa utashindwa, ndio uthibitishe kuwa wote ni wale wale kuliko usijaribu hata kidogo alafu ubaki kulia umasikini. Ni kama kati yetu sisi wakristo huwa tunasema, ni heri uamini mungu yupo uende umkose, kuliko useme hayupo uende umkute. Tujaribuni upinzani tuwapime je wataweza??? Au ni wale wale tu wanaporojo
Ni hayo tu wadau.
Amani iwe juu yenu, mungu ibariki Tanzania yetu.