Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

TAARIFA MUHIMU; Lowassa kuhutubia live usiku huu; Mgombea Urais wa CHADEMA ambaye pia anawakilisha UKAWA, Edward Lowassa atahutubia taifa usiku huu moja kwa moja kupitia Kituo cha Televisheni cha ITV mara baada ya taarifa ya habari. Hii itakuwa Kwa ajili ya Watanzania ambao kutokana muda kuwa mfupi hawakupata fursa ya kusikia hotuba yote aliyopanga kuitoa leo Kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za kitaifa za CHADEMA na UKAWA.

Anasoma alichoandikiwa and nothing more. Hajainua kichwa kuongea nasisi wananchi. Hii ni dalili kuwa hayo hakuyatayarisha yeye na hayako moyoni mwake. ----@#$?!??
 
Kikwete ni hodari sana jukwaani ila utendaji ni sifuri.

Watu wote ambao ni mahiri kutongoza wanawake wakiingia kwenye siasa wanafanikiwa kupata madaraka kirahisi kwa kuwa jukwaa wanalimudu lakini wanapotakiwa ku deliver wengi wao huwa wanapwaya sana.
 
Sorry, nimejibu kulingana na muanzisha thread. Yeye kamkejeli mgombea aliyebanwa na muda.
 
Sera imetulia. Mwanzo niliogopa. Ukawa noma!

Usiku huu kasoma sera poa kabisa ITV. Alisema mchana aliogopa sheria za nchi. Huyu jamaa ni mjanja tofauti na Lumumbas wanavyomfikiria. Anajua kuteka watu. Mchana hakuongeza hata dakika 1 katika muda uliowekwa kusheria. Ni mjanja sana na ni mtaalam wa kusoma alama za nyakati!
 
Kama Mwakyembe ni mwanaume kweli atuambie yale aliyoyaacha kwenye ripoti ile ili serikali yote isianguke aache kubwabwaja kwenye majukwaa. Ikulu nayo ijibu hoja za Lowasa kama kweli Kikwete hausiki.

Thubutu! Watamnyonyoa nywele tena na safari hii hazitaota kabisa!
 
Lowassa hana uwezo wowote ule zaidi ya kubebwa na ukanda wa KASKAZINI.

UKAWA KWISHA HABARI YAO
 
HATIMAYE HAKI ZA RAIA KUWEKWA REHANI NA Mzee Lowassa


Uraia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania una haki zake zilizoainishwa kikatiba ambapo kila raia wa kundi lolote la jamii ana haki zote zinazofungamana na uraia wake.
Kinga ya haki za kiraia na kijamii ni katiba ya nchi. Kiongozi anaweza kuwa na nafasi yake katika dhamana ya utawala lakini yeye kama yeye hawezi kuwa hakikisho la haki za raia.
Hivi sasa Nchi imeingia katika kampeni za kumchagua Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni kampeni zitakazochukua takribani miezi miwili.
Katika kipindi hicho, wagombea, kupitia Vyama vyao mbalimbali, wananadi Ilani zao ambazo zitajumuisha ahadi mbalimbali pamoja na sera. Wagombea watakuwa na ahadi nyingi lakini lazima izingatiwe kuwa hawatatenda mambo kinyume na katiba.
Ni vipi sasa wafungwa waachiwe bila utaratibu kisa mzee kawa rais?

Mgombea yoyote hawezi kuaminika kwa ahadi kuwa yeye atawafanyia watu mambo ambayo yatakuwa kinyume na sheria mama. Tangu hapo, raia hawapaswi kutenganisha ahadi za mgombea na katiba ya nchi.
Haki zote za kiraia zilizoainishwa kikatiba hazipaswi kunadiwa wala kuwekewa ahadi na mgombea kwa sharti la kumpigia kura. Haki hizo za kijamii hazihitaji ahadi za mgombea bali zinahitaji kutekelezwa na yoyote yule atayeshinda kikatiba.
Kwa maneno mengine, Rais yoyote kutoka chama chochote cha siasa ana wajibu wa moja kwa moja wa kikatiba kutimiza haki za kiraia na kijamii za kila raia na kila kundi la jamii pasipo kutazama dini yake.
Waislamu, kama jamii, hawahitaji kuzifungamanisha haki zao za kikatiba au kisheria na ahadi za wagombea kisa urais.Je ni waislamu wangapi watanufaika na uvunjifu huo wa kikatiba? Kufanya hivyo kunaziweka hatarini haki zao kwani hakuna uhakika wa moja kwa moja kwamba mgombea huyo atashinda au la!
Maadam Jamii ya Waislamu na wakristo ina hakika kuwa haki zao za kiraia, kijamii, kisheria na kadhalika zote zina dhamana ya moja kwa moja ndani ya Katiba ya nchi, basi Mgombea asijaribu wala kuthubutu kuomba kura kwa ahadi ya kutimiza jambo lolote ambalo, tangu hapo, litakuwa ni sehemu ya wajibu wake wa kiutawala.
Atoe ahadi, asitoe ahadi, bado wajibu wa serikali ni kutimiza haki za kikatiba za raia. Uislamu na Ukristo utabakia palepale.

Hatari hiyo ni ile ya kujaribu kuitazama karatasi ya kura kama nusra ya jamii yao. Ukubwa wa hatari hii haupo tu katika ukweli kuwa kiongozi anayeaminiwa anaweza kwenda kinyume na ahadi hiyo, au chama chake kumkwaza, bali anaweza kushindwa uchaguzi, na kuwaacha Waislamu mikononi mwa yule ambayo hawakuwa na ahadi naye.

Mathalani, Waislamu wakisema kuwa watampigia kura mgombea wa chama fulani ili eti awatoe Waislamu waliofungwa jela kwa mashitaka mbalimbali, swali linalowarudia, ni je, akishindwa uchaguzi ndiyo ina maana Waislamu waliondani waendelee kukaa huko?
Achilia mbali hilo, ni mgombea gani ambaye anaweza kuchukua ahadi ambayo itakuja kukinzana na matakwa ya sheria? Ifahamike kuwa Uchaguzi wa Rais haufuti sheria wala hauondoshi majukumu ya Majaji na Mahakimu katika kutoa tafsiri ya sheria na hukumu.
Utakuwa utapeli wa kisiasa kwa mgombea kutoa ahadi ya jambo ambalo litakinzana na matakwa ya muhimili mwingine wa Dola. Tafsiri za sheria za Mahakama Kuu na zile za Mikoa na Wilaya zitabaki palepale licha ya mabadiliko ya Uongozi wa Kitaifa.
Jitihada za kisheria ziendelee kufanyika katika kukabiliana na tafsiri za sheria za Wanasheria wa Serikali bila kusubiri Oktoba, wanasiasa wenye hoja kutugawa wanapaswa kupewa ONYO KALI.
WAPIGA KURA WASIKUBALI KUBULUZWA,WATUMIE HAKI ZAO ZA MSINGI KUCHAGUA KIONGOZI ATAKAYE KUWA NA TIJA KWA WATANZANIA WOTE.
 
lowasa leo umeendeleza comed zako ,watu mamia kwa maelf wamekusanyika mkukusikiliza wakisobwa kwa meri kutoka zanzibar na kila kona ya jiji na mamantilie ,bodaboda na madreva daladala na wamama, uliowaarika kwa mikutano takribani wiki nzima leo wanakuja kukusikiliza kwa hamu kubwa unawambia nini?

Muheshimiwa lowasa,

eti wakasome hotuba yako kwenye websit? Kweli?
Nafikiri wanaokushabikia bado hawajatambua wanachofata kwako siku wakijua watakukimbia,

Kajifunze kuandika basi kwanza
 
Yaani dreva nilimwambia aendeshe gari kama limeibwa lakini sijauwahi huu mkutano wa kihistoria,wewe nifah umenitelekeza kunitumia picha japo uliniahidi!!! Kwaaaaaaaaaaa

Nisamehe best wangu, pls!
Ila nilikuambia kuwa sitoenda na simu jangwani. ..pia baada ya kufika home nikatoka sikupata muda wa kukutumia.
Hope umefika salama.
 
lowasa leo umeendeleza comed zako ,watu mamia kwa maelf wamekusanyika mkukusikiliza wakisobwa kwa meri kutoka zanzibar na kila kona ya jiji na mamantilie ,bodaboda na madreva daladala na wamama, uliowaarika kwa mikutano takribani wiki nzima leo wanakuja kukusikiliza kwa hamu kubwa unawambia nini?

Muheshimiwa lowasa,

eti wakasome hotuba yako kwenye websit? Kweli?
Nafikiri wanaokushabikia bado hawajatambua wanachofata kwako siku wakijua watakukimbia,

Kumbe ulikuwa unafuatilia LIVE!
 
kikwete naye Kesi Ya jinai inamsubili kwani yeye ndio kubwa LA mafisadi Richmond, epA, escrow, mabehewa ya treni n.k
 
sikio la kufa halisikii dawa. huyu mgonjwa kwa kweli anamatatizo makubwa sana, sidhani kama yupo seriaz na urais, maana dakika 7 kweli ndio anaongea kwa kutetemeka pale mbele huku kainamisha kichwa chini tu maskini yarab
 
Angezidisha mud mungesema aadhibiwe........tutaruka viunzi vyote mwaka huu, na pale ni ufunguzi tu wa kampeni, bado muda upo hiyo ilani itasomwa sana na kila mtu ataielewa.
 
Back
Top Bottom