Kuwa mahiri jukwaani si uthibitisho wa kuwa kiongozi bora. Lowassa anazo sifa nyingi na tunazifahamu lakini ntakupa sifa moja tu ambayo hamna kiongozi yeyote wa CCM anayo. UTHUBUTU.
Ndugu Lowasa anatambua tatizo kubwa linalowalabili watanzania.katika hotuba yake ya mbeya,arusha na leo katika uzinduzi wa kampeni ni babu sea jamani hii ni shida kubwa sana
wiki moja imepita nilisema chadema hawana ilani ya uchaguzi panya road wakatoa matusi lakini nikajua hawajui hata maana ya ilani ya uchaguzi
You know hata mimi nawashangaa baadhi ya watu humu coz wanaongea kama vile uchaguzi ni kesho so leo ndio ilikuwa mwisho wa kampeni na hivyo hakutakuwa na muda tena wa kuzungumzia hiyo ilani......Ndugu zangu leo ni mwanzo tu!Campaign ni mpaka October 24, hivyo kila kitu kilichopo kwenye ilani kitawekwa wazi
Tumaini Makene fanyeni hivyo haraka..wengi hatujapenda..tunataka hotuba ya maana leo hii
Lakini si walikuwa na siku nzima kuanzia saa 800 mpaka 1800 walishindwaje kujipanga? Huwo ni muda mrefu sana wa kuweza kuchagua ni kipi muhimu cha kufanyika kwanza, sasa kama hata hilo hawaliwezi yaani jinsi ya kupangailia muda wataezaje kuongoza nchi na kuleta mabadiliko wanayowadanganya watu!
Tulia majibu utayapata kampeni ndio zimeanza!Wakuu salaam. Nikiwa mtanzania wa kawaida kabisa ambaye napima mambo ya kisiasa kwa vigezo vya msingi kuliko ushabiki, hatimaye nimejiwekea mambo machache tu na ya kawaida kabisa ambayo UKAWA na Lowassa wanatakiwa kuyafafanua leo ili nijenge imani kwao. Mambo haya ni :
1. Kwa kuwa Lowasa kati ya mwaka 1997 na 2000 alikuwa akiiongoza wizara ya kuondoa umasikini, alifanya nini kinachompambanua kwamba anachukia umasikini? Hapa mfumo si hoja yenye tija sana kwa sababu mifumo mibovu ina kawaida ya kuwajenga viongozi bora kwani hujipambanua wazi wazi.
2. Kati ya mwaka 1993 na 1995 Lowassa alikuwa akiiongoza wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi, alifanya jambo gani la kumtofautisha na watendaji wengine? Wananchi wamkumbuke kwa lipi katika wizara hiyo ambayo ilikuwa maalum kuhakikisha wananchi wanapata makazi bora na kuondoka katika dimbwi la umasikinttti.
3. Mwaka 2000 - 2005 huyu mheshimiwa aliongoza wizara ya maji na mifugo. Ninachotaka kujua ni kwa nini katika kipindi chake cha uongozi migogoro ya wakulima na wafugaji ilizaliwa. Ni dhahiri kuwa ni wakati huu wafugaji walipata nguvu ya kuvamia maeneo ya wakulima na kusababisha tatizo ambalo limekuwa sugu hata leo.
UKAWA kwa upande wao naomba watueleze ni kwa nini tuendelee kuwaamini iwapo wamerudi kukanusha yale waliyotuaminisha hata tukawapenda.
1. Vita dhidi ya ufisadi. CHADEMA walijipambanua kama wapiganaji wa kweli dhidi ya ufisadi. Hii ndio sera ambayo bila ubishi iliwapatia umaarufu mkubwa.
CHADEMA wasimame na kukiri hadharani leo kwamba yale waliyotuaminisha kwa muda mrefu juu ya ufisadi ni uongo. Haitoshi tu kusema Lowassa hakuwahi kutueleza ukweli kuhusu Richmond. Hii ni ushahidi kuwa Chadema si chama makini hata kidogo. Kinaendesha siasa za kitapeli kwa malengo binafsi.
Tena msamaha huu uende mbali zaidi kukiri kuwa yale mliyokuwa mkijidai kuwa ni ushahidi mzito mlionao ulikuwa uongo ili kupata huruma ya wananchi.
2. CHADEMA ikiri na kuomba radhi kwa watanzania kwa kitendo chake cha kukiuka misingi kiliyojiapiza kuisimamia na kukanyaga demokrasia. Msamaha uombwe dhidi ya dharau na kejeli walizofanyiwa waliokipigania chama hata kukifikisha hapo kilipo. Mchakato wa kupata wagombea katika ngazi za urais na ubunge umegubikwa na sintofahamu kiasi cha kusababisha mgawanyiko wa kisiasa. Intelijensia ya CHADEMA imekuwa juu ya matakwa ya wananchi.
3. CHADEMA iombe radhi kwa utapeli wa kisiasa ilioufanya dhidi ya mauaji ya Olasiti. Ule mkanda unaoonyesha wauaji wakitekeleza mauaji hayo umeota mbawa. Hizi ni siasa za kitapeli. Kutafuta huruma za wananchi kwa hila.
4. CHADEMA wafafanue mipaka ya mashirikiano yao na CUF hasa linapokuja suala tata na nyeti kwa maslahi ya nchi la sera ya ULIBERALI. Watanzania tumeaminishwa na CHADEMA kwamba CUF wanasimamia ushoga na wanauunga mkono. Naomba CHADEMA waelezee msimamo wao, ama waombe radhi kwa kuwazushia uongo CUF.
Haya ni baadhi ya masuala ya msingi sana ambayo natarajia mkutano wa leo wa UKAWA utayatolea ufafanuzi.
Tujadili kwa hoja, matusi mwiko. Lizaboni, RIZ1, et al
Lowasa akihutubia njoo unikate shingoTAARIFA MUHIMU; Lowassa kuhutubia live usiku huu; Mgombea Urais wa CHADEMA ambaye pia anawakilisha UKAWA, Edward Lowassa atahutubia taifa usiku huu moja kwa moja kupitia Kituo cha Televisheni cha ITV mara baada ya taarifa ya habari. Hii itakuwa Kwa ajili ya Watanzania ambao kutokana muda kuwa mfupi hawakupata fursa ya kusikia hotuba yote aliyopanga kuitoa leo Kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za kitaifa za CHADEMA na UKAWA.
Tunataka sera sio mipasho,au mnataka kushika dola bila ya kuwa na sera,mimi nilidhani leo ilikuwa siku ya kusikia ilani na sera za usharika wenu,haya mambo ya Twiga mbona tunayajua,na yamefanyika miaka mingi,au Sumaye ndio anajua leo,hizo ni hasira za makapi.