Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kwa upande wangu, Mkutano ulifana sana hasa kwa uwingi wa watu, watu walikuwa wengi saana haijawahi kutokea kwenye medani ya Siasa za Tanzania, tatizo nililoliona kwenye ratiba ya UKAWA, muda aliopewa Mgombea Urais ulikuwa ni mdogo sana, otherwise nawapongeza sana.
Mimi nilikoshwa na hamasa ya wote waliohudhuria pia na amani ilitawala.
 
LOWASA! LOWASA! LOWASA!!!
i) Post nyingi za wanaccm Facebook
zinamzungumzia Lowasa!
ii) Post nyingi za wanaUKAWA Facebook
zinamzungumzia Lowasa!
iii) Post nyingi za wanaACT Facebook
zinamzungumzia Lowasa
iv) Magroup mengi ya siasa whatsaap
yanamzungumzia Lowasa muda mwingi!
v) Twitter tweets nyingi zinamzungumzia
Lowasa
vi) Viongozi wa kubwa wa vyama mbalimbali
vya siasa wameacha kunadi Sera zao
wamekalia Lowasa!
vii) Viongozi wa serikali wameacha ofisi zao
wapo Ngurudoto kuzungumza juu ya Lowasa
viii) Thread nyingi za Jamii forum
zinamzungumzia Lowasa!
ix) Magazeti Mengi habari zenye uzito ni
Lowasa!
x) Redio na tv ni Lowasa
xi) Ukirudi mitaani kila mtu haongei maneno
matatu bila kumtaja Lowasa!
xii) Mtanzania wa leo hapati usingizi mpaka
ataje Lowasa!
xiii) Watu kabla hata ya kupiga mswaki
asubuhi wanaamkia Lowasa!
HITIMISHO!!!
TUKUBALIANE TU KUWA LOWASA NI HABARI
YA MJINI!!!!
 
-Watu walioenda kushangaa drone cameras za azam ni wengi kuliko walioenda kusikiliza hoja,
-watoa hoja wengi walitoka kwenye reli wakawa wazee wa 'kujibu mapigo' kuja kushtuka muda umeenda!
-mtoa hoja mkuu kwa mara ya pili ndani ya wiki HAJAKIDHI matakwa ya umati. Licha ya kudai kaenda kupanda daladala na kwenda kwa mama lishe kusikiliza kero zao na wao kumfahamisha kero zao, bado kashindwa kuwaambia atawatatulia vipi kero zao hivyo wakabaki na viulizo.
HIVYO MKUTANO WOTE ULIKUWA NI FIASCO.
 
Lowassa si presidential material. Tukatae tukubali, mojawapo ya majukumu ya rais ni kutoa speech kwa hadhira mbalimbali. Mfano linapokuja suala la mialiko ya nchi marafiki, jumuiya za kimataifa (mfano UN, AU, nk), etc. Hayo ni majukumu ya wazi kabisa yasiyokwepeka. Rais ni kioo cha taifa. Kwa ule mzaha niliouona jana, UKAWA wamepotea njia.
Sema ana nyota ya kupendwa na 'vibaka na wazee wa viroba'! Hamna mtu mwenye akili timamu akasema Lowassa anafaa!
 
Kama Sera ndo kipimo cha ushindi bas ccm washashinda maana sikusikia cha maana zaidi ya kumtoa Babu Seya na Masheikh wa uamsho.

Misri serikali ilianguka kwa kuonewa na kuuwawa kwa mtu mmoja tu.
Haki haijalishi ni waathirika wangapi
 
Magamba yamenyamaza kimyaaaaaa sasa yameanza ohoooo mgombea jana akuongea sera zinaandikwa na kutekelezwa
 
Kwan kampein zimeisha na mlitaka kila kitu aseme pale hilo lisingewezekana, helewa atakachotamka mtwara kitahusu nchi nzima au kutakuwepo yanayohusu watu wa mtwara tu wala hakuwa na haja ya kuyasema jangwani
 
Watu wameungua jua siku nzima mtu anakuja kutoa kipaumbele cha kutoa gerezani magaidi, majizi na vibaka na kuhakiki kua atafufua na wafu! Sijui huko mikoani ataenda kuongea nn! Labda atumie hiyo site ya chama
 
Kwakweli jana nilifurahi sana, watu walikuwa wengi lakini amani na usalama ulikuwepo wa kutosha.
Hakuna aliyeibiwa wala kuharibiwa mali zake...ulikuwa mkutano wa AMANI NA UPENDO.
Kila aliyekuwepo alionesha furaha na tabasamu la matumaini, huku kila mmoja akionesha shauku ya mabadiliko.
Tofauti na ambavyo nimekuwa nikisikia CCM wanawananga Chadema/UKAWA kuwa mikutano yao inahudhuriwa na wanywa viroba sio kweli maana walikuwepo warembo wa ukweli, gentlemen na wazee.
Hakika vijana ni wengi sana nchi hii.
Hivyo basi, tathmini yangu nawapa ushindi UKAWA kwa 70% kwa yote niliyoyaona jana.
 
Kwa uchangiaji huu sidhani km utapata unachohitaji
Kiukweli ukawa hatukujipanga tufanye nn ktk uzinduzi wa kampeni
Kubwa tulilofanya ni kujibu hoja zisizotuhusu
Wazee waliotukimbia walikuwa na uwezo kuliko uoongoz uliopo sasa
Tumeyakamia sana maji sidhani km tutayanywa
Kauli yetu watz wakasome sera ktk tovuti ni sawa na ile ya maghufuli asiye na nauli apige mbizi
Dar ndo kitovu cha mabadiliko km tumeshindwa kusema sera dar huko mikoani sijui itakuaje
Tuachane na kuwasafisha kina lowasa tuweke sera mezani
Yapo mengi mkuu wachangie na wengne
 
Tathmini yangu ni kuwa wale watu waliohudhuria jana hawakuwepo kabisa katika uzinduzi wa CCM!
 
Tathmini yangu ni kuwa wale watu waliohudhuria jana hawakuwepo kabisa katika uzinduzi wa CCM!

Acha uvivu jaribu kushirikisha kichwa chako japo kidogo tu..... Watu wanaenda mikutanoni kusikiliza Sera za wagombea ili wafanye maamuzi vyema... Pale walikuwepo watu wa vyama tofauti kusikiliza Sera za ukawa unfortunately they were so disappointed.
 
Bangor lingine lilisema,Age MTU abaki mmasai lingune bira kipindupindu kuliko ccm,bora go no kuliko ccm.
 
Magamba tuambieni msimamo wa mgombea wa ccm 2005 ulikuwa ni "maisha bora kwa kila mtanzania" Nyie wapenda misimamo mbona hiyo kauli mbiu hatuisikii tena ! Na hakuna anayethubutu kuisemea! Miaka kumi imeisha dola sh. 2,300/= wakati JK aliikuta ni sh. 1,000/=
SAA hii tunaambiwa kila kijiji sh. 50,000,000/=, wakati Leo hii watoto wa SHULE wanakaa chini, kinamama wajawazito wanalazwa chini!
Walimu wanaambiwa wataboreshewa maslahi wakati hata hayo maslahi duni hawayapati inavyosyahili? Wanadai mabilioni!
Hatudanganyiki tena! CCM hata wakisimamisha malaika tutamnyima kura, achilia mbali magupuli aliyelitia hasara taifa kwa kuuza Nyumba za serikali kwa bei ya kutupa na mbaya zaidi anatuhumiwa kumuuzia Nyumba nanhii wake na hajawahi kukanusha!

Baada ya kusoma umefikia conclusion kwamba mimi ni magamba?
Soma upya labda utapata mwanga mpya. Wengine tuna discuss issues bila kujali magamba au magwanda.
Ccm na ukawa wote wanaweza kuondoka na Tanzania itabaki.
 
Ukawa walijipanga sema mda ulibana,nilitegemea kwa ratiba ilivyokua wangeanza kwenye saa saba au saa nane hivi ili ratiba iende vizuri. Lakini mambo yalikua poa tu. Na kikibwa zaidi ilani ya chama imekaa vizuri sana na inatekelezeka kama watanzania wataamua kuipa ukawa kura.
 
Back
Top Bottom