Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

MC anaua...anasema yule aliyesema picha zinaphoto shop apae kwa helkopta aje aone sunami. Na pia jamaa anasema yule aliyesema sisi ni wapumbavu na malofa aambiwe kwamba rais wa malofa anakuja kuongea na malofa wenzake....tshirt pia zenye neno...malofa katika ubora wetu zinauzwa...nomaaaaa
 
Naomba kuuliza ni kituo gani cha televisheni kinachotangaza mkutano huu moja kwa moja online?
 
hoja nyingine unajijibu mwenyewe. tutajadili nini sasa?
 
Huyu MC anaitwaje??
 
Unazungumzia January? Are you serious?
 

Wewe ni mtanzania au mburundi? Wakati siasa za nchi hii ziko kwenye yransformation wewe umekalia ndoto. Lowassa wa enzi zile alipokuwa chama cha magamba si wa siku hizi. Isitoshe kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo ukiwa umefungua macho na kutumia akilizako sawasawa zikuongoze huyu mheshimiwa katumia wadhifa wake katika kufanya maamuzi magumu na yenye tija kwenye taifa hili. Ni mengi kuliko kiongozi yeyote aliyeko CCM. Narudia, idadi ya aliyofanya ni ndefu kulinganisha na kiongozi yeyote wa CCM.

UKAWA: Huu ni umoja wa Katiba ya wananchi. Wanastahili pongezi badala ya kuanza kuwa na mashaka nao, kazi walofanya so far ni ya kuridhisha. Nyenyere analeta ushabiki wake usio na tija, hivi anataka tuendelee kuwaamini CCM waliompakazia mzee wa watu tuhuma ya Richmond? Aliyehusika na skandali hiyo tunamjua na tunsubiri tuone mchakato wa kura utaendaje ili tuweze kuwawajibisha wote waliohusika na wizi ule. Mapambano dhidi ya ufisadi hayajaisha, tulimtuhumu Lowasa kwamba ni fisadi kwa sababu tuliaminishwa hivyo na tume ya Mwakyembe ambayo ilimung'unya mung'unya wakati inasomwa. Ila bado mafisadi wako wanafaidi keki ya taifa, itakuwa chungu karibuni.

Hapo cha kuomba radhi ni nini? Nyenyere ebu tumia akili kidogo, ruhusu au lazimisha akili yako ifanye kazi ya ziada isumbike kufikiri.

Lowasa si fisadi, magamba walimsingizia akanyamaza tu kulinda heshima ya chama chake ambacho hakikumthamini.... mkiendelea kumchokonoa ataanika mengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…