Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Wanachakachua hata vyombo vya kutangazia,halafu ndio tuwape nchi,hivyo vyombo vimetoka kwa mangi maadamu ni mambo ya ukanda wa kaskazini.

Hahahahahaaaa! yawezekana kweli? Acha utani bhana.
 
Generator yetu ni aina ya Honda, na lita 20 zilivyotumika mbona kuna maelezo. Tumewasha tangu saa nne kuwapa majirani muda wa kusikiliza video ya hotuba ya Mwl Nyerere ya mwaka 1995 (Kilimanjarop Hotel) yenye kuongelea Uzanzibara na Uzanzibari halafu tukaangalia video ya Mwl Nyere ya mwaka 1995 ktk Mkutano Mkuu wa CCM yenye kuongelea Watu wanataka Mabadiliko. Vile vile watu wamesikiliza na kuona cliup za uzinduzi wa CCM na kuwasikiliza Makongoro, Warioba, Shein, Mkapa, Kikete na Mgombea. Yaani watu nilionao hapa wamepata elimu ya uraia tosha sasa wanasubiri hotuba ya Mbowe, Maalim Seif, Slaa, Makaidi, Mbatia, Lisu, Duni na Lowasaa ili wachuje mbichi na zilizoiva.
vipi, kamanda slaa atakuwepo? au umeweka tu kuwafuraisha wana jambi?
 
Tumaini Makene yupo wapi...mbona huu uzi ni wakijinga tu sioni update jamani....
tatizo pia ni Mods kujinyakulia uzi.Mkuu Standalone alianzisha uzi hapa toka sa6 uck.akaahidi Makamanda watatoa updates.Mods wamefuta wakaleta wakwao.upo uwezekano updates zipo katikati humu
 
Last edited by a moderator:
tanesco mnaboa.... nawalaani kwa majina yote ya babu zenu!!!! mlaaaaaniwe kabisa na msirudishe tena umeme wenu, sina shida nao.
 
MC uwanjani anamwambia JK achuke helikopta aje aaangalie kama alikuwa anadangaywa kuwa picha zinatengezwa basi aje aone.

Chama kisicho na adabu kushika hatamu ni mwiko.. you can't tell the president nothing... hakika wasiojitambua wamejaa jangwani leo alafu wanama tshirt MALOFA hahaa
 
Kwanza why hata MC tu awe na last name Mrema?
Hivi hakuna ma MC wengi tu wenye kutoka kanda zingine?
mnalalamikiwa hadi madereva ni Macha na Massawe na Mrema na hata hili hamlioni?
achilia mbali jamaa ni bogus kabisa
hajui kutangaza wala hajulikani katolewa wapi but his last name ni Mrema...
hamna watu wataalam wa kutengeneza image iweje?
 
Habari wakuu,

Leo ni uzinduzi wa kampeni kwa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambazo zinafanyika leo Jumamosi tarehe 29 Agosti 2015 katika viwanja vya Jangwani. Kampeni hizi zitaungwa mkono na umoja wa vyama vilivyo chini ya UKAWA vinavyojumuisha NLD, NCCR na CUF.

Tuwe pamoja hapa (kwenye hii thread) kujuzana yatakayojiri kwenye kampeni za leo.

​

============

View attachment 281698

12:01pm - Jangwani

​
Kwa sasa ni burudani kwa wasanii mbalimbali kutumbuiza na kwa sasa aliemaliza kuimba ni Singo na anaefata ni Juma Nature akiwa na msaga sumu.

9:18 Mchana: Kilichopo kwa sasa bado ni burudani na Sasa inatumbuiza bendi

Tunahitaji picha please
 
Jamani jenereta langu limegoma kuwaka pamoja na maandalizi yote niliyoyafanya kukabiliana na Tanesco.
 
Mama mdogo ccm ahadi zao ni hewa miaka yote madini yameisha gesi ndiyo wanaililia waimalize ndiyo waachie nchi vivutio vya utalii kama tembo wamezing'oa meno bila ganzi hadi wameamua kuzaa bila meno tena twiga wanakunjwa hadi wanaingia kwenye sanduku na unaweza kukutana na kiongozi wa ccm amebeba begi kumbe ni twiga wewe kama Una kitu chako kikubwa Kama twiga usihangaike mwite hata balozi was ccm ataikunja mpaka itaenea hata kwenye pochi make hayo mafunzo ya ujangili wanayo nakushauri achana na hao wanakumaliza mdogo mdogo.

Post of the day!
 
Last edited by a moderator:
Mbona umeme unakatika katika sana leo? Ni hofu ya siri-kali ya CCM juu ya Tsunami la Lowassa? Sisi ambao hatukumudu kujumuika Jangwani itakuwaje? Wanataka kuzuia Watanzania wasione Tsunami?
"Malofa katika ubora wetu!"
 
Back
Top Bottom