Kutoka Mahakamani - 15 Septemba, 2026: John Heche aendelea kutoa ushahidi

Heche kashaanza kukunju Asili yake ya Ukuryani, hataki unyonge kabisa, huyu katuga ilibidi aanze nae vagi toka siku ile ya kwanza kwa cross examination. Katuga ni mpuuzi tu.
Wewe mwenyewe umesababisha asianze na huo moto, si ulikuwa na mashaka mengi juu yake? Akaona kuwa mnyonge ni mbaya, leo ameuwasha moto 🔥
 

KATUGA ukienda pupa ujue anakuja kwako binafsi
Anatumia mbinu
nyingi kukuchanganya
wewe kazi kwako ukitaka sifa kwamba wewe mjuaji wa sheria
Mkali mkali sana
ujue utaumbuka mbele ya watu wale wale wamekusifia‼️‼️
 
Huu ndio ujinga wenu mkipigwa mtaanza kulia, kesi ipo Mahakamani mpendwa wenu kama hana hatia ataachiwa kurudi nyumbani.
Naona umenikuu vibaya sina upande, nimechangia na ni maoni yangu binafsi
 
Hapa Heche amechangamka ameanza kwenda ulalo ulalo na Katunga
 
Hii kesi imeumbua mengi sana
1. Tuliambiwa tecdema ina viongozi waliokula kitabu, badala yake katibu mkuu wa tecdema ni form six na miaka mitatu chuoni (huu ni mfumo mpya wa elimu uliopo tecdema)

2. Mkurya mwenzangu anaitwa john wegesa heche, halafu mwenye vyeti ni wegesa heche suguta

3. Wahasibu si waliosomea uhasibu..

4. Hawa chaso wanaohitimu wanaenda wapi?

NIMEELEWA KWA NINI ALIYEKUWA MGOMBEA MWENZA WA DR. SLAA NI DARASA LA SABA.
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 14

Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination Makam Mwenyekiti Bara John Heche

Katuga: Unamjua Katibu wa Chadema kata ya Mikocheni anaitwa Ishengoma?

Heche: Tuna kata zaidi ya 4,000 kwahiyo siwezi kujua

Katuga: Unajua kuwa huyu Katibu wa Chadema, Ishengoma alisema kuwa mlishiriki vurugu za Oktoba 29?

Heche: Sijui

Katuga: Ni sahihi Lissu asingealikwa kwenye mkutano wa Tarehe 03/04/2025 asingeongea?

Heche: Sijui

Katuga: Unajua maana ya constructive publication?

Heche: Sijui

Katuga: wewe ni shahidi wa nini kama kila kitu hujui?

Heche: Shida unakuja na majibu yako ya uongo.

Katuga: Ni sahihi ulitaja ripoti nyingi za nje kuhusu uchaguzi wa mwaka jana?

Heche: Sahihi

Katuga: Unajua kuwa opinion ya EU sio binding kwenye mahakama hii?

Heche: Najua

Katuga: Ulieleza kuwa umezilete hizo ripoti hapa mahakamani?

Heche: Sikueleza

Katuga: Njia ipi ulitumia kubadilisha jina kutoka Wegesa Charles Heche kwenda John Wegesa Heche

Heche: Kiapo na Deedpoll na zilitangazwa kwenye gazeti la Serikali

Katuga: Ni ushahidi wako kuwa kwenye kubadilisha jina ulitangaza kwenye gazeti la Serikali?

Heche: Ndio utaratibu

Katuga: Ila wito wa Tume ya Chande hukuona kwenye gazeti la Serikali

Heche: Kwani mimi naona magazeti yote ya serikali? ndio sikuliona hilo tangazo.

Katuga: Nilikusikia uliirejea taarifa ya Thabo Mbeki Foundation

Heche: Ni sahihi

Katuga: Unajua ama hujui kuwa sio Foundation ya kimataifa?

Heche: Mi najua ya kimataifa.

Katuga: Iko chini ya umoja gani wa kimataifa?

Heche: Mi najua ni ya kimataifa.

Katuga: Mwalimu Nyerere Foundation iko chini ya kimataifa?

Heche: Sijui.

Katuga: Unajua au hujui kama walichokitoa foundation ni maoni?

Heche: Ni maoni yao.

Katuga: Unajua au hujui kuwa Thabo Mbeki Foundation walichukua maoni kutoka UN na SADC?

Heche: Najua walichukua AU na SADC sio UN

Katuga: Unajua Thabo Mbeki hawakuwa waangalizi wa uchaguzi?

Heche: Nalijua hilo

Katuga: Kwa vile umesema ya Thabo Mbeki ni maoni, Je mahakama inapokea ushahidi wa maoni?

Heche: Sijui

Katuga: Waheshimiwa majaji naona mimi niishie hapa.

Sasa ni zamu ya Tundu Lissu kuuliza maswali ya Re Examination.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Uchawini ndo wapi mzee mayanza
Kuna huu uzi Mkuu

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…