Kutoka Mahakamani - 15 Septemba, 2026: John Heche aendelea kutoa ushahidi

TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1.

Mhe. Lissu ameanza kumfanyia Re- examination Makam Mwenyekiti Bara John Heche.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa uko tayari? Na tunaamini utakuwa na maswali machache.

Mhe. Lissu: Niko tayari Waheshimiwa majaji ila inategemea na speed ya nyie kuandika pia maana mimi ndo niko Gerezani kule sio Sheraton hotel Waheshimiwa majaji.???

Jaji Ndunguru: Bado una mashahidi watatu tutamaliza within time mshtakiwa maana tulitegemea Ijumaa mngewasilisha final submissions

Mhe.Lissu: Kwanza hao mashahidi wangu nahitaji kuonana nao ili tupange mkakati wa kesi yetu.

Watu wamecheka sana mpaka Majaji, kuhusu Mkakati wa Lissu na mashahidi wake yaani IGP Wambura, CDF Mkunda, na DCI Kingai.😂😂😂

Tunaendelea na Re Examination

Mhe. Lissu: Wakili Mwinuka alikuuliza yale matatizo yanayohusiana na fomu ulisema hukupata shida ya kuambiwa ulijaza fomu vibaya ila ulisema ujazaji fomu ni moja ya kigezo.

Heche: Ni kweli nilisema suala la ujazaji fomu ni sehem ya matatizo ya uchaguzi yanayotumika kuengua wagombea hasa wa upinzani kuna wakati mtu anaambiwa CDM badala ya CHADEMA.

Wakili wa Serikali Mwinuka: Jibu la shahidi lina attract sisi kuja kufanya cross examination yeye atoe tu clarification

Mhe. Lissu: Fafanua bila kutoa mifano

Heche: Kuna vigezo vingine vingi ambavyo vinatumika kuengua wagombea na vinatumika kwa wagombea wa upinzani tu hasa Chadema.

Mhe. Lissu: Umejibu vizuri

Mhe. Lissu: Uliulizwa kuwa kwavile wewe hukuenguliwa na ulishinda, ukaulizwa kwa vile ulishinda badi Uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Heche: Uchaguzi niliochaguliwa haukuwa huru na haki kwasababu kuna watu waliouwawa.

Wakili Mwinuka: Waheshimiwa majaji hii kwasababu watu waliuwawa ina attract nafasi ya sisi kufanya cross.

Mhe. Lissu: Hilo hapana Wakili wa serikali hayuko sawa sawa, shahidi katika ushahidi wake aliulizwa kuhusu mauaji na alisema alishuhudia wakati wa kampeni kulikuwa na mauji Nyamongo na alishuhudia

Jaji Ndunguru: Endelea Heche

Heche: Waheshimiwa Majaji kampeni zetu ziliingiliwa na Polisi, watu waliuwawa lakini pia hata Mawakala wetu walienguliwa.

Mhe. Lissu: Uliulizwa kama Makamu wa Rais alikuja wakati nikiwa Nairobi Hospital ulisema alikuja na alikuwa kwenye mkutano.

Heche: Ni kweli Makamu wa Rais alipoenda Nairobi kwenye kikao na baada ya kumaliza kikao ndo alienda kumuona Lissu Hospital.

Mhe. Lissu: Uliulizwa kama nilikupa jukumu la kufuatilia mafao yangu ya Hospital ulijibu sikukupa jukumu ila ulikuwa kwenye Kamati ya Chama ya matibabu yangu, fafanua.

Heche: Mhe. Lissu aliposhambuliwa iliundwa kamati na Chama na mimi nilikuwa sehemu ya kamati ya kufuatilia na hakulipwa.

Mhe. Lissu: Uliulizwa kama Chadema mlikuwa na imani na Tume ya Chande, ulijibu hamkuiamini na tuliamini itaficha mauji na kulinda waliouwa.

Heche: Ni kweli hatukuwa na imani kutokana na jinsi ilivyoundwa kwahiyo tuliamini ingeficha ukweli wa kilichotokea na kusafisha watu waliohusika.

Mhe. Lissu: Shahidi wakili Katuga alikuuliza kuhusu Tone tone na michango ya chama uliyopokea, ulijibu suala la michango ya chama sio la Makamu Mwenyekiti, fafanua.

Heche: Suala la michango yote ya chama linasimamiwa na Katibu Mkuu ambaye ni accounting officer na linapita kwenye account rasmi za kichama, haiwezekani kwa vyovyote vile Makamu Mwenyekiti akahusika na michango ya chama.

Mhe. Lissu: Kwenye masuala hayo hayo ya pesa za michango uliulizwa kuhusu Salman na Nilesh, na uliambiwa kwenye account yako umekewa M10 na 20M, ulisema huwajui.

Katuga: Jibu lilikuwa siwajua kuna ufafanuzi gani? Sisi tunapinga kuanzia swali kwasababu jibu litaleta majibu mapya.

Mhe. Lissu: Wakili wa Serikali anapaswa kujua kuwa kabla ya shahidi hajajibu hapaswi kutabiri jibu. Hoja ni kwamba suala la 10M na 20M lilikuwepo hivyo lazima liwe re examined.

Jaji Ndunguru: Haya shahidi fafanua

Heche: Siwajua na sijawahi kuwaona.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 2.

Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Re- examination, Makam Mwenyekiti Bara John Heche.

Mhe. Lissu: Ulionyeshwa video ukaulizwa kama ni wewe na kama hayo maneno yanaelekea kuwa ni ya kwako na ukasema hukumbuki kutoa hotuba ya aina hiyo.

Heche: Sikumbuki kutoa hotuba hiyo, wametumia akili mnemba kuitengeneza.

Mhe. Lissu: Fafanua Akili Mnemba

Watu kicheko😂😂😂😂

Heche: Akili Mnemba ndio Artificial Intelligence (AI)

Mhe. Lissu: Uliulizwa kuhusu magari manne ya bei mbaya ukasema una magari mawili, fafanua.

Heche: Nilimaanisha nina Prado na Hilux ambazo ndo huwa nazitumia, hiki ndo nilichomaanisha.

Mhe. Lissu: Unakumbuka kuhusu kukamatwa kwako nje ya Mahakama na kuwa unapelekwa Tarime, Uliulizwa ulienda Kenya? Ukasema nilizuliwa, fafanua.

Heche: Nilizuiliwa na immigration kwenye mpaka wa Sirari.

Mhe. Lissu: Unakumbuka uliulizwa na mawakili wa Serikali kuhusu wewe kukutana nao Oysterbay Police na walisema kwamba 70% ya waliokamatwa walikutaja wewe kuwa unahusika na kuratibu wewe hizo vurugu, ukasema hujui , fafanua.

Heche: Nilikuwa ndani tangu tarehe 22 Oktoba 2025 kwa vyovyote vile siwezi kuhusika na yaliyotokea Oktoba 29, 2025.

Mhe. Lissu: Uliulizwa kuhusu matibabu yangu hasa kuhusu matibabu nje ya nchi, ulijibu kwamba wakili wa Serikali alikuwa sahihi nusu na sio sahihi nusu, Fafanua

Heche: Kuna mazingira ambayo Mbunge anaweza asifuate utaratibu wa kawaida, mfano mazingira kama ya dharula.

Mhe. Lissu: Uliulizwa ni lazima Mbunge mpaka apate referral kwenda nje ya nchi? Ukasema sio lazima apate refferal

Heche: Mbunge akiwa mahututi sio lazima apewe referral

Wakili wa Serikali: Waheshimiwa Majaji muda umeisha hivi sasa ni saa kumi na moja tunaomba ahirisho hadi kesho saa tatu kamili asubuhi.

Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji huyu John Heche ndio shahidi wangu wa mwisho kwa ambao ni raia, Kwahiyo kesho tutamaliza sio zaidi ya lisaa kwahiyo naomba kesho mashahidi wengine kesho waje ili niongee nao kujua namna tunavyoenda na ushahidi uliobaki.

Watu kicheko😂😂😂😂😂😂

Jaji Ndunguru: Shauri linaahirishwa hadi kesho saa tatu kamili asubuhi, shahidi bado hujamaliza kutoa ushahidi wako.

Imepigwa High Cooooouuuuuurrrrrtttt

Majaji wanatoka

Tukutane kesho saa tatu kamili asubuhi✌️

TUKUTANE KESHO ASUBUHI MAHAKAMANI.
 
Wambura, kingai na Mkunda kesho asubuhi na mapema wanatakiwa wawepo ndani ya mahakama. Lissu akae nao kufanya nao mkakati wao was utetezii.
Tafadhari sana asitokee kwa yoyote kukosa na kusingizia udhuru. Hatutakubaliiii.
kesho udhuru ni kwa wote mkuu, hakuna atayekubali kupanda kizimbani.
 
Kweli kabisa, hawa wengine jau kabisa. Huyo sasa anaanza kupanick kitu ambacho kinamuondolea credibility. Mnyika anastahili kuwa Mwenyekiti
Nani alikwambia ukipaniki inakuondolea credibility. Una mambo !

Paniki haina kwensekwense kisheria isipokuwa kama paniki imeleta inconsistency + contradiction kwenye ushahidi.

Kwenye ushahidi halikuwa jukwaa la kuchagua mwenyekiti/makamu mwenyekiti bora, huo sio mdahalo wa wagombea, excuse us.
 
Pamoja na maneno hata reaction yako ni inaangaliwa, facial expression na hata mdomo wako. Ndo maana hata kwenye mpira wa miguu wachezaji wamezuiwa kuongea wamefunika mdomo. Ukipanick ina maana kuna kitu hakiko sawa kwako kwa hiyo unatumia ukali kama defence. Sijawahi kwenda mahakamani nahisi ni moja ya sehemu ambayo unatakiwa uwe vizuri sana kiakili, kimwili na kimawazo.

Nimejifunza na naendelea kujifunza masuala ya mahakama hayahitaji mihemko wala kukurupuka.
 
Mnyika yupo vizuri sana kiakili sikuwai kumwelewa vizuri kama ile siku na katuga 🤠

John Mnyika alifanya kazi ya ziada kumuokoa Boss wake✍️
Wanafiki nyie tunawajua tabia yenu, mnyika alifanya kazi nzuri ndio, mbona hamkumsifia siku ile mnamsifia leo?

Sio wewe uliyeshikia bango elimu ya mnyika ile siku?

Unataka nikutafsirie unachojaribu kufanya hapa? Manipulation za kitoto.

Ukweli ni kwamba mlikuwa mmemkamia Heche, and so far mpaka hapa hajawapa mnachotaka, you are all dissapointed, mnaokoteza vi kitu kitu kumdiscredit.
 
Heche big Brain! Katuga amekosa alichotaka kukipata 😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…