Wao walipokuwa wanawapelekesha wavulana enzi wapo vigoli na wanalipa walikuwa wanaona raha sana na waliinjoy game ila now umri umewatupa mkono wanataka waendelee kupelekesha watu.
Sema NO kwa demu anayekupangia maisha kama anaharaka mwambie apite hivi akatafute ndoa ya fasta sio akuingize katika commitment zisizo na kichwa wala miguu wakati sio sehemu ya mipango yako mkaenda kushindwana huko ndani.
Me niwaambie tu vijana. Jamii kwa muda mrefu imetuvalisha ujinga kuwa Ndoa inatufaidisha au ina manufaa kwetu but utafiti nimefanya ndoa ni kitu kizuri sana kama ukikutana na wanawake walioandaliwa kuwa mke wa mtu kwa kutii maelekezo, maagizo, kushika mafunzo, kufuata muongozo, kusimamia utaratibu na kusimama na mwanaume ambaye amekula kiapo kuwa ndie mume wake.
Ila kwa bahati mbaya na huu ni ukweli sote tunajua ni kuwa ndoa kwa sasa zinakwenda mrama sababu hatuna wanawake wenye home trainings wengi wapo Street trained na corporate trained. So huwezi jenga maisha na familia na mwanamke ambaye anatumia zaidi ya masaa 12 nje ya familia akipuyanga mitaani na kuhangaika na dunia, mitaa na makampuni au biashara za watu.
So save you the headache. Ukiona anakupa mashaka usikaze saba ubongo, wewe apply safe mode fasta jenga life lako binafsi. Achana na maisha ya kufosi yatakupa magonjwa.
Wazee wetu walihitaji ndoa sana kwasababu miaka yao si sawa na yetu. Walikuwa ni lazima wale home maana migahawa haikuwapo kama leo, leo kuna migahawa inapika vizuri kuliko chakula cha home.
Kulikuwa hakuna wafanya usafi, madobi, leo hii wapo tena very cheap utafuliwa nguo zako, utasafishiwa nyumba unapoishi kwa hela ndogo sana.
Zamani ukiwa haujaoa by 20 jamii inakuona tatizo na watakutazama kwa jicho la umakini na mashaka kuwa ni mharibifu ila now days wanawake wenyewe ndoa hawataki wanagawa gemu unaweza lala na wanawake tofauti kila wiki kwa mwaka mzima bila kumrudia wa kwanza hadi mwaka unaisha, na ni kwa gharama kidogo au bila gharama kabisa.
So sisi wanaume ndio tunang'ang'ania ndoa kwasasa kitu ambacho kwa miaka hii hakina maslahi kwetu tena kama zamani. Unakwenda kumlazimisha mtu uishi nae , umlipie mahitaji yake, tena aje ajimilikishe mali zako na anakuombea kila siku ufe yeye atawale. Ndio maana maisha yanakuwa mafupi sana kwa wanaume sababu ya kujikumbatisha ujinga.
Kuna maisha kwa mwanaume nje ya hizi ndoa feki za kisasa. Ukiweza kujenga uchumi wako ambao kipato chako kitazidi matumizi yako brother am telling utaona how scammed we are kwenye issue ya ndoa.
Si unakumbuka hata kipindi tukiwa wadogo walituambiaje kuhusu Elimu. Kuwa tukisoma sana na kufaulu, guaranteed tutatoboa Maisha, ni kweli tumetoboa maisha kwa mujibu wa maneno ya wanajamii?
Si unaona tofauti ya kutumia akili na kutumia hofu?
MUNGU anajua kuwa vijana/wanaume ndio tunaipambania ndoa na tunaitaka kwa 100% kinyume na wenzetu, mabinti /wanawake ambao wameamua kuhasi kwa makusudi taasisi hii nyeti na kuishi kwa uhuru halafu wakianza kuchoka wanataka tuwapokee na historia zao za kuruka na wanaume tofauti tofauti wakiwa na majanga kibao.
So tujenge tu mfumo nje ya Ndoa ikija sawa isipokuja usitetereke kuna Maisha nje ya Ndoa young Kings, msiwaze.