Kutoka na mwanamke mwenye kiu ya kuolewa ni balaa zito

Kutoka na mwanamke mwenye kiu ya kuolewa ni balaa zito

Mimi ilinitokea nikamwambia siwezi kuoa kwa sasa tuwe wote kama miaka 2 tukisomana lakini mwezi mmoja ndio nisema Nitakuoa nitakuwa mwongo akaniambia yeye NI mzuri na anaweza pata mtu mwingine,nikamwacha baada ya mda anaanza maneno ooh Yale niliongea tu sababu umri Naona unaenda na blabla kibao wakati huo nimeshapata chombo ingine nikamkaushia mpk Leo anataka tuwe wote mara sijui mwanangu amekukumbuka nk.
Na alikuwa na mtoto dah kudadadeki, wanawake wana balaa hawa khaaaaaah?
 
Usahihi wa mwanamke ni kujitunza na kumtii mwanaume wake basi. Hayo mengine ni ya kwako. Wewe umekwenda kuliwa huko tumekutana uanze nipush kukuoa na sijajua una tabia gani za mazoea na sijui unajimudu vipi kitabia.
Kuna vitu unachanganya hapa.
Suala la kujitunza linawahusu watu wote, mwanamke na mwanaume. Hivyo sio issue ya upande mmoja tu wa mwanamke.


Issue inayojadiliwa hapa ni kuhusu wanawake wanaohoji na kushinikiza mahusiano yao yabadilike kuelewa kuwa ndoa.

Kama umekutana na msichana, ukampenda na kuanzisha mahusiano, na katika mahusiano yenu ukagundua binti anawaza ndoa tu na wewe haujawa tayari kwa hilo kwa sasa, basi achana na huo uhusiano mara moja kwa kuwa malengo ya uhusiano wenu hayaoani na hupaswi kumlaumu kwa msimamo huo.


Ni sawa tu na wale wanaume waliojenga mahusiano (ya kutaka kuoa) na wanawake ambao wanawaza kutafuna pesa zao na sio kuelekea kuolewa, mwanaume ukigundua hilo ni vyema ukaachana na huyo mwanamke mara moja kwa sababu malengo yenu hayaoani.
 
Wakati naendelea na KAMPENI ya KATAA NDOA kama kawaida nilikutana na MWANAMKE mmoja hivi KISU vibaya mno, huyu kwa kweli kama angeelewana na Mimi vizuri ningeoa.

Akawa analeta Maringoo meeengiii nikamkaushia nikaendelea kupata KOZI ya KATAA NDOA na kwa kweli SOMO la KATAA NDOA limeniingia vilivyo.

Huyo MWANAMKE kwa sasa ana umri wa 24/25 hajui kama kabakiza miaka 4 sokoni, na ndio kwanza anampango wa KUSOMA Chuo ngazi ya DEGREE.. so, kama atatumia miaka 3 huko chuoni atabakiza Mwaka 1 Sokoni..

Kama namuona vile atakavyochuja kwa GHAFLA sana.. muda huo mimi ndio nazidi kuwa MTAMU yaani.. na wakati huo ile KOZI ya KATAA NDOA nitakuwa tayr nishahitimu kwa GPA ya juu sana.
 
Tatizo la nguvu za kiume chanzo chake kikuu ni kipi?

Wanaume tunajiua tartibu kwa kudhani kushughulika kingono na wanawwke ndiyo urijali. Kisaikolojia kuna damage kubwa sana kwa mwanaume ambye huruka na wanawake wengi kuliko mwanamke anayeruka na wanaume wengi.

Kuchomeka na kupush agenda kunahitaji stability, stamina na energy ambazo kadiri unavyojianika kwa kasi ndo unavyosinyaa.

Namshukuru Mungu, nilijitunza na mpaka sasa utu uzima wangu nacharge kama nilivyokuwa twentieth. Rika langu wengi nawaona wanavyohaha na madawa ya kuongeza nguvu.

Wanawake ni reciprient, tatizo lipo kwa sender
Sio kweli unachosema ni kitu kingine kabisa. Unajua wanaume wanalala na wanawake kwa sababu tofauti.

Kuna ambaye anapenda kulala na mwanamke mpya ndipo anapata msisimko. Kuna ambaye anatabia ambazo wanawake hawawezi kudumu na yeye ameshajua hilo so kila mwanamke anayelala nae anajua hataweza kuishi nae anatafuta mpya.

Kuna ambao wanalala na Wanawake tofauti sababu wana sexual drive kubwa yaani moto ambao mwanamke wa kawaida hataweza kuumudu hata iweje so ni lazima awe na kazi za kando.

Kuna ambao wanataka kufurahia kufanya mapenzi (sio mahusiano)jambo ambalo haliwezekani kufanikiwa na mwanamke m'moja kutokana na ile kanuni ya maozea, kwamba mwanamke ukishamzoea hata yeye atapunguza excitement anapokuwa na wewe na hapo ndipo shida huanza.

Sasa wewe utakuwa unaongelea scenario ya mtu ambaye alikuwa anafanya ngono bila msukumo kutoka ndani, aidha alikuwa anataka jamii imuone kidume, au wanaume wenzake wamuone ana idadi kubwa ya mademu. Na wengi wa hawa huwa wanatumia sana dawa za kuboost. Ila nikwambie tu, mwanaume the more anafanya mapenzi na wanawake katika mazingira ya kufurahia huwa anazidi kupata stamina na ujuzi sababu anakuwa akijifunza jiografia ya wanawake na kuwaelewa namna na maeneo gani ambayo ni very common katika kumfanya afurahia na kutoa mrejesho mzuri wakati wa gemu.
 
Hataki kurudia makosa. Kama kakaa miaka 3 na kumpa mwanaume kila kitu na hakumuoa kwanini arudie tena kufanya hivyo ilihali anataka kuolewa?
Kwahiyo unadhani wakati anafanya hivyo yeye alikuwa hajui kuwa anafanya kosa?

Wewe unawajua wanawake au unawaongelea tu hapa?

Mwanamke anaweza zaa na baba yako na akakupa sababu ambayo yeye anaona ni ya msingi. Unachotakiwa kujua ni kuwa wanawake huwa hawatafuti unachotaka wewe wanatafuta wanachotaka wao kwanza.
 
Age 33 unategemea kama anahitaji kuolewa asiulize hayo maswali? Binafsi naona kama kijana huna malengo ya ndoa fanya ngono na binti asiye na malengo ya ndoa.
Unakuta hao age goo nao wanakuvutia kufanya nao ngono ijapokuwa wengi michosho kwenye ndoa

Ogopa mwanamke mpaka anagonga 30s hajaolewa jiulize hiyo miaka 20s yote hakupata mume shida ilikuwa nini

Wametumika sana sasa wanatafuta wa kuja kuzeeka naye.
 
Nani kasema mwanaume ndio anatangaza ndoa?
Kuanzia kwenye dini, sheria na jamii ndoa ni patano la watu wawili waliopendana na kupatana kutaka kuishi pamoja. Mmoja hawezi na hapaswi kumlamisha mwingine.

Kila mahusiano lazima yawe na malengo (objectives) na hitimisho (conclusion). Sasa binti anayejitambua (haijarishi umri wake na tabia zake) atataka kuhoji malengo ya huo uhusiano na hitimisho lake ni nini mapema sana. Sasa wewe mwanaume ukiwa ndio wale akili ndogo na fupi za kutoka kubalehe na ndio unajifunza uhuni wa kingono ni lazima utamchukia na kumuona huyo binti sio, kumbe shida ni upeo wako mdogo wa kimakuzi.
Kila la kheri katika hili
 
Tena unaachana nae kabisa ukiona anataka ndoa na huna nia ya kumpa hilo hitaji. Usitembee na binti wa watu kuanzia ana miaka 27 mpaka 32 halafu unamkimbia kuwa hafai na ukute na mimba ushampa.
Unaweza ukatazamia upande m'moja kwa kumuona huyo mwanamke innocent na huyo mwanaume ni tatizo.

But most of the time ni mfumo wa maisha aliyoishi sasa yameanza kuzaa matunda. Sote tunapoanza mahusiano kwa mara ya kwanza huwa tunafahamu kuwa kuna good side na bad side of things. Na tunatakiwa kuchagua kwa umakini na kuzingatia mafunzo ya maadili.

Sasa kama mtu alifanya bad choices tena kwa makusudi huko utotoni then automatically unategemea akija kubungua maisha yake hadi miaka 30 then aje kutegemea sympathy ya wanaume wastaarabu tena awe exonerated na nature?

Haiwezekani.

You do the crime u do the time. Hakunaga easy escape kwenye maisha, everything you do with your own energy and Force will have reciprocating force and energy from nature.

Ukiruka ruka na wanaume bila utaratibu tegemea by the time umechoka utakutana na wanaume wenye misimamo yao ambao nina uhakika hautaqualify vigezo vyao hata 10% ya wanachotaka. Na utakuwa na option ya kuchagua aidha kufuata maelekezo na muongozo wake ama upite hivi ukafie mbele na wale wanaume ambao ni dead beat.

Kumbuka kuna mabinti wamejitunza, wanajiheshimu, wanajilinda na wana adabu, hawa ndio wanastahili kupewa first priority, mimi nikikutana na binti bikra lazima nimpe respect sababu kajitunza.
 
Wewe unawajua wanawake au unawaongelea tu hapa?
Boss,
Mitazamo hutegemeana na historia,
Nimeoa miaka ya nyuma, nina watoto na wa kike pia, nililelewa na mama aliyekuwa mke wa baba yangu.

Binafsi Mwanamke simtazami kama adui ila naheshimu mtazamo wako sababu inategemeana na uliyoyaona au uliyopitia.
Mwanamke anaweza zaa na baba yako na akakupa sababu ambayo yeye anaona ni ya msingi.
Ni kweli, Binadamu anaweza kufanya unyama na akakupa sababu ya msingi. Mwanamke ni binadamu.
Unachotakiwa kujua ni kuwa wanawake huwa hawatafuti unachotaka wewe wanatafuta wanachotaka wao kwanza.
Ni sawa, kama siwezi kumpa anachotaka, na yeye hawezi nipa ninachotaka sasa wa nini kwangu? Matatizo huanza pale ushindani wa kukomoana unapoingia.
 
Sasa mwanaume ulifuata nini kwa huyo binti unayedhani tabia yake sio njema, umri wake umekwenda na amejipanga kuolewa?
Kwani ulilazimishwa kuanzisha naye uhusiano?

Kwa kifupi sana, haijarishi binti ana tabia gani mbaya, amechezewa kiasi gani na umri wake umekwenda, bado yuko sahihi kwa 100% kutamani kuolewa, kujali hatima yake ya kuolewa na kuolewa na mtu anayeeleweka.
Watu tunafata mzigo kama wao wanavyotaka hela zetu we vipi wewe?
 
Back
Top Bottom