Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Ndani ya wiki moja amejitengenezea rekodi mbili
1. Kujiuzulu nafasi yake ya kuteuliwa na rais Kama balozi nje ya nchi... Imeichukua Tanganyika miaka 62 na ushee kupata tukio Kama hili
2. Kuwa mkimbizi wa kisiasa akitokea kwenye nafasi ya ubalozi.. Mwenzake aliyejiuzulu nafasi hiyo miaka 62 iliyopita marehemu Christopher Kassanga Tumbo yeye alirejea nchini Tanganyika na kuendelea na maisha yake
Huyu kaachia ngazi kakimbilia mafichoni kisha kawabagaza viongozi wake vilivyo.. Si kwa matusi wala kejeli bali kwa ukweli wengi walioshindwa kuusema hadharani Kama yeye
Wabezaji watakuja.. Na mijadala kumhusu itachukua muda kupoa.. Lakini vyovyote iwavyo kajitwalia rekodi nyingine adhimu
Swali muhimu la kujiuliza kwanini kafanya hivi sasa na katumwa na nani.. Na je kwenda kuwa Mwambata Cuba ilikuwa ni project ya siri iliyoendeshwa kwa ustadi na umakini mkubwa?
Kuna kitu hapa wengi hawajakiona!
Kuufubaza upinzani (CHADEMA) kwa njia za kikatili na kibabe haya ndio matokeo yake... CHADEMA ingeachwa na harakati zake si Polepole wala Gwajima wangejitokeza hivi walivyojitokeza.. Sana sana wangejikltokeza kujibishana na upinzani
Unapodhibiti upinzani upande mmoja fanya kwa akili kubwa ili uasi usije ukainuka upande mwingine
Uasi na upinzani viko ndani ya nafsi ya binadamu.. Ni lazima kuwasikiliza watu wanataka nini.. Ni ngumu kuwapa vyote lakini hakikisha unawapa vile vya muhimu na vya lazima ili kuweza Ku "control" upinzani kwa upande mmoja na uasi kwa upande mwingine
Ukishindwa kufanya hivyo halafu muasi na mpinzani wakatengeneza uswahiba .. Umekwisha !
Kwassaa kuna tukio moja tu litakaloweza kumfifisha Polepole.. Nalo ni kumwachia huru mwenyekiti wa CHADEMA na kuifutia CHADEMA kesi za kutunga pamoja na viongozi wake.. Kwa kufanya hivi.. Pole pole atasahaulika misa ya kwanza
Kwa hali ilivyo ni wazi sasa "aliyeasi" ana uungwaji mkono nyuma yake tena mkubwa tuu na mpinzani CHADEMA ndio kabisaa... Ikitokea wakaamua kufunga ndoa hata ya mkeka.. Mengine yatabaki historia
Kwakuwa bado kuna mengi bado ya kuandika naomba niishie hapa..
LA mwisho IFIKE MAHALI JF IPEWE MAUA YAKE! Kuna information nyingi muhimu sana humu.. Yanayotokea sasa ni yalisemwa kwa lugha kificho tangu January... Je walijuaje na system isijue!? Ama ni system yenyewe ndio mkandarasi?