Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Kuna tatizo kwa watia nia wote wa CCM kuhusu swala la muungano! Hapa kwenye misingi mikuu ya muungano pengine wamelazimishwa kusema kitu kimoja!
 
Kama huyu Membe angekuwa na ufahamu sahihi, asingekubali kurusha live hiki kipindi. Ni bora angeongea na watu wa lindi kimya kimya maana wahenga walisema "Ukimya nihekima ya mpumbavu"

Sasa huyu .............
 
Huhuhuuuuuuuu!, nikiwa rais wa nchi hii nitahakikisha kina baba wote wanaheshimu wake zao, Ndio Mzee!!!.
 
Hapo nimempenda kwenye VETA/UFUNDI ana idea nzuri,kuongeza na kufufua viwanda kutaongeza ajira,pia vijana wataweza hata kujiajiri,ila je atayaweka kwenye VITENDO?
 
Hivi Watanzania mnajua kuwa Membe amekuwa shushushu kwa miaka zaidi ya 20? Tangu enzi za mwalimu Nyerere.

Na mchango wa hiyo kazi yake ni nini? kwa maendeleo ya taifa?
 
Hana uwezo wa kushawishi kabisa

Hana uwezo wa kushawishi hana mvuto hana plan, mikakati ya kukuza uchumi zaidi ya kupiga blah! blah vitu vingi anaongea juuu juu (zilipendwa) infact sijaona mtu anaefit kwenye kiti cha urais mpaka sasa
 
Mbona anaongea kama kampeni as if meshapitishwa tayari kugombea uraisi na chama chake?? " mkinichagua kuwa raisi mwezi october".

Bt ndio mambi ya siasa yana raha yake na kila unaemuona unaona kama vile tayari kawa raisi, watu weeeeengi wanaitaka nafasi na mtarajia ni mmoja tu.
 
Huyu Jamaa ni bonge la Mbinafsi.. Mimi mimi kibao... angalia mikono yake anavyojisifia ...
 
Tatizo lenu wengi hamjui siasa. Hilo ndilo linalo wasumbua. Hivi unadhani hapo anaomba kura za Watanzania? Mwenzako hapo anataka chama kimpe ridhaa tu. Sasa ukijipeleka peleka bila kuwataja viongozi wa chama hiyo ridhaa utaipata wapi!?!

Membe kichwa wewe...usimuone mjinga.

Sasa nani kasema anaomba kura hapo kwahyo hapo akichaguliwa kuwa rahisi atakua anatumikia chama au? Kujenga hoja bado sana huo ndo ukweli.
 
Membe mbona unatuacha kimya kimya sisi Diaspora uraia pacha.
 
Back
Top Bottom