Wengi wa wanaCCM wanaotangaza kugombea uraisi wamekuwa wakijigamba kutaka kuleta mabadiliko.
Wengi wameonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa serikali ya sasa, hivyo kujinadi kuleta mabadiliko..
Wote ni wanafiki, na wasanii. Wapo humohumo ndani ya CCM, na wengine hata serikalini. Wamekumbatia yote yanayoendelea sasa. Wameshindwa kuyataka hayo mabadiliko hata kwa maneno tu, leo wanatuhadaa kuleta mabadiliko
Wapo wanaCCM wawili tu waliodhihirisha kweli kutaka mabadiliko kwenye mienendo mibovu ya chama chao
Hao sio wengine bali ni Mansoor Himid na mzee Moyo.
Wengine wote waliokumbatia system ya kifisadi ya hicho chama, wakistawishwa kwa matunda ya wizi na ubadhirifu wa mali na haki za watanzania masikini, kisha leo wanasimama hadharani kusema eti wanataka kugombea ili walete mabadiliko ni waongo na wasanii
Hamkuaminika kwa madogo, tuwaaminije kwa makubwa?!!!