Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Membe ongea utawafanyia nini Watanzania hayo ya kaburi sijui nini yana nafasi gani kwa mwananchi.
 
"Nilialikwa na chifu wa Zanaki na nilienda na kutambuikia kaburi la Mw. Nyerere, na niliongea na Mw. Nyerere kwenye kaburi lake na kumueleza kuwa aniruhusu nivivae viatua alivyomwachia Mwinyi,Mkapa,na JK."

By. Membe.
 
Hapa naona nguo tu...huyu jamaa wala hafai kuwa rais wa TFF
 
Eti kaenda kusali kenye kaburi la mwalimu,jamani sasa mwalimu hana uhai tena,jamani Membe vipi huyu jamani tunadanganywa kweli,conspiracy theory at work
 
Sala yake kwenye kaburi la Mwalimu imeniacha hoi. CCM kwa vituko ni mwisho. Aisee.
 
Mpaka sasa hakuna sera yoyote ya maana zaidi ya historia na majigambo!
Kazi kwelikweli.

Acha haraka mamie...twende mdogo mdogo. Muda bado tunao, ilani ya chama bado haijatoka. Sera utazisikia tu.
 
Mpaka sasa hakuna sera yoyote ya maana zaidi ya historia na majigambo!
Kazi kwelikweli.

Mii nimeamua kuwaangalia wadada waliovaa green and yellow wanavokatika.
 
Naona wazungu wapo bize kumpiga Membe picha tu. Sijui kama babu Slaa atapata heshima hiyo.

Babu Slaa amebaki kulalamika kusalitiwa na Ngwajima...
 

Attachments

  • 1433670881487.jpg
    1433670881487.jpg
    25 KB · Views: 187
"Hakwenda Ikulu kwa kuhonga, Membe nae hana magunia ya pesa kuhonga"
 
Kweli Membe hujui kujenga hoja kabisa wenzako wamekufunika vibaya mno. Tangu uanze hujaongea Sera ya maana. Jinadi acha kuwasifia Jk na Mkapa.
 
Bado sielewi kwa nini Membe na Lowassa wamekuwa gumzo ccm ilihali wote weupe tu. Mmoja mwizi mwingine mnafki.
 
Membe anasema alienda kuomba kwenye kaburi la nyerere ili amruhusu awe rais na anasema ameshapewa majibu kuwa anafaa... huu ni uhuni sana sana. huyu mwalimu mwaka huu atatumika sana kisiasa na watu naona hawana jambo jipya la kuongea isipokuwa kusingizia nyerere. membe anasema pia kuwa kuna wajumbe wa halmshauri kuu wamenunuliwa. hii ni hoja ambayo wajumbe wa halmashaur kuu nadhan itawakwaza sana. hawa wazee wangeachwa wapumzike tu kwa kweli maana naona wanatumika vibaya. hasa nyerere kila mtu atakuja kusema ameruhusiwa na nyerere wakati tunajua nyerere ni marehemu.
 
anaongea kama kanywa kiroba aina ya EMPIRE....naombeni mwamvuli.....anaapa kumlinda jk na familia yake
 
Back
Top Bottom