Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Aisee. Sasa hapo Membe anapambana na UKAWA? Membe anatakiwa acheze mechi tatu ndo aingie fainali na UKAWA.Mechi na CC, Mechi na NEC na Mechi na CCM GA.

Msome vizuri, utamuelewa tu.
 
Membe uongozi zaidi ya miaka 20 zero accomplishment zaidi ya kuwa na title nyingi
 
Anatafuta kubebwa na watawala

Tena mbona haeleweki anaongea kama miwanaukawa vile ati akichaguliwa atakomesha mauaji ya albino. simwelewi huyu bwana mtangaza nia. yeye kama mtawala ameshindwa kukomesha anangoja mpaka awe rais. kazi kweli kwelio
 
Kuna fununu kuwa tayari amishaaminishwa kuwa yeye ndiye atakayeteuliwa na CCM kugombea Urais...ndiyo maana jamaa akawa na kiburi kile kwa kutamka mambo hovyo hovyo na kushindwa kujieleza vzr...hata hivyo kujieleza hajui kabisa naamini CCM watatumia nafasi hiyo kumuengua moja kwa moja.
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, ametangaza rasmi nia ya kuutaka urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2015 akisema anatosha na kwamba Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere huko aliko atafurahi endapo atakuwa rais.
Membe aliyasema hayo jana kwenye Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa wa Lindi katika hotuba yake ya saa moja kutangaza nia yake hiyo huku kwa kujiamini kabisa akisema kuwa yeye ndiye Rais wa Tanzania kwa miaka 10 ijayo. Alisema katika urais wake, ataboresha elimu, ataweka msisitizo katika utawala bora, maendeleo ya jamii, uchumi na masuala mbalimbali ya kisiasa na kidiplomasia.

Huku akishangiliwa na maelfu ya watu waliofika kumsikiliza, alisema amejipima na kuona anaweza. “Nimetafakari sana, nimeona ninatosha kwa nafasi hii nyeti…, nafasi adhimu na si ya mzaha japo naona wapo wanaofanya mzaha. Nimeangalia nikaona hakuna mwingine wa kufanana na mimi. “Sikukurupuka, zipo nafasi za kukurupuka na wapo wanaokurupuka, lakini si vyema kukurupuka kwa nafasi ya urais,” alisema.Membe aliyesindikizwa na mkewe Dorcas, alisema Machi mwaka huu alikwenda Butiama na kuzuru kaburi la Mwalimu na kupiga goti na kumweleza nia yake ya kuutaka urais.“Nilipiga goti nikamwambia Mwalimu, navitaka viatu vyako, alivivaa Mzee Mwinyi (Ali Hassan), Mzee Mkapa (Benjamin) na Kikwete (Jakaya), sasa nataka kuvaa mimi na nina hakika vinanitosha.“Ninaamini vitanitosha. Nikamwambia chondechonde, kama havitanitosha, niambie… timu yangu ya mikoani ikawahi kuniambia unatosha,” alisema Membe. Alisema alialikwa na Mzee Mwinyi katika ‘birthday’ yake ya miaka 91 na kati ya mambo aliyomwambia ni kwamba ameongoza nafasi mbalimbali, lakini hakuwahi kununua uongozi.“Mzee Mwinyi aliniambia kuwa alipata vyeo bila kununua, alisema sikuwa na magunia ya pesa miee…, sikununua wajumbe. Sasa, utajisikiaje kununua vyeo? Utawaangalia kwa jicho gani wanapokosea na utachukua hatua gani kuwawajibisha? Kuna vitu vya kununua lakini si Ikulu. Ikulu hainunuliki.”

Utawala bora
Akizungumzia utawala bora, alisema kuwa hawezi kukaa kimya kuona rushwa, ubadhirifu, ufisadi vikichukua nafasi katika utawala wake.“Ninawatumia salamu mapema, sitakuwa na kigugumizi kwa wanaotesa Watanzania. Nitahakikisha Watanzania wanachukia rushwa na kutakuwa na sheria kali dhidi ya mtoa na mpokeaji rushwa. Kama ni watumishi wa umma,watakwenda na maji... “Nitalinda mipaka yetu, polisi itakuwa ya kisasa na viongozi lazima wawe wanaosikiliza watu…”

Elimu na afya
Kuhusu elimu, Membe alisema ataweka mkazo mkubwa katika elimu ya ufundi na kazi itakayofuata ni kufufua vyuo vya ufundi ili wanafunzi wawe na uwezo wa kujiari au kuajiriwa kutokana na ufundi wao. Katika sekta ya afya, alisema kuwa atahakikisha huduma za afya ya mama na mtoto zinamfuata mhusika na si kina mama kuwafuata watoa huduma.

Muungano
Alisema ataulinda Muungano kwa kuwa ni heshima ya Tanzania kimataifa kwani mpaka sasa ndiyo inayochukuliwa kama mfano kwa kuwa na Muungano imara... “Sitawavumilia watakaovuruga Muungano, nasikia kuna wanaoukebehi, nawaambia waache.”

Uchumi
Membe alisema atafanya kazi ya kuzishirikisha sekta binafsi na umma katika kuendesha uchumina zaidi ni kuziwezesha sekta binafsi kupata mitaji mikubwa.Alisema ana mpango ni kuwarudisha Watanzania katika uchumi wa viwanda kwa kufufua viwanda na kuboresha kilimo, ili mazao yanayozalishwa yanunuliwe hapahapa nchini na kusafirisha bidhaa. “Hatutaki tena kusafirisha malighafi nje halafu tunaletewa bidhaa zilezile zilizosindikwa, haya mapinduzi ya viwanda ni lazima, mara tu nikiingia Ikulu Oktoba mwaka huu,” alisema.
Kadhalika, alisema kasi kubwa ya kufufua viwanda itashinikizwa na uwepo wa gesi asilia iliyovumbuliwa mikoa ya Kusini na itasaidia kupunguza gharama za upatikanaji wa nishati yaumeme.

Vyombo vya habari
Membe alitaka vyombo vya habari kuvumbua uovu katika jamii kwa kuwa vinafika katika kila eneo na serikali yake itatumia taarifa hizo kufanyia kazi kikamilifu. Alibeza muungano wa vyama vinne vya upinzanichini ya mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa) akisema kuwa utaendelea kushindwa na hata mwaka huu, upinzani hauna nafasi na akaushangaa kwa tabia yao ya kudai wameibiwa kura mara zote wanaposhindwa.

Chanzo: Mwananchi
 
katika Hotuba Dhaifu kuliko zote zilizotolewa Ya MEMBE imeongoza. AIBU SANA , NI TOFAUTI na NILIVYOKUWA NAMCHUKULIA .


huwa tunawaambia kuwa...Membe hawezi kupigana yeye kama yeye..huwa anahitaji kubebwa na bila kubebwa hawezi kitu...eti anasema " Wanaume mkome....." anarudia zaidi ya mara moja....nimeamini dhaifu ni dhaifu tu...
 
Na mashaka na wale aliowatuma kuuliza kama anakubalika au la?

Mkuu hivi wewe ukinipa fedha niende mikoani kufanya utafiti kama unakubalika au lah...unadhani mimi nitarudisha majibu yapi kwako?.....fungua akili yako...chakula wewe ndiye uliyenigharamia, malazi wewe, usafiri wewe, posho wewe... lazima nikuridhishe...
 
akalaghe bhao bhaaa!!
hatufai haipendezi ndg kupokeza nchi bhana / rais alishatoka kusini ,
alishatoka kanda ya ziwa,alishatoka znz,na sasa atoke kanda ya kati tabora au kanda ya kaskazini ARUSHA./ TANZANIA NI YETU SOTE NA SOTE TUNAHAKI NAYO/
 
Nilichoona ni wasanii tu kwenye mkutano,kumbe ccm bila wasanii haiwezekani!!!
 
Chenga nyingine hiyo...huyu hata kibajaji ana afadhali..
 
Anataka urais ili amfurahishe nyerere?

Daaaah what a waste!!
 

Attachments

  • 1433744385379.jpg
    1433744385379.jpg
    75.8 KB · Views: 386
Back
Top Bottom