Kutokana na hii story yangu hauwezi nikuta humu nashabikia kutoa watoto EMs na ISs na kuwapeleka kayumba

Kutokana na hii story yangu hauwezi nikuta humu nashabikia kutoa watoto EMs na ISs na kuwapeleka kayumba

Financial Analyst

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2017
Posts
1,849
Reaction score
3,506
IT IS A SIMPLE STORY BUT VERY MEANINGFUL....

Kile kipindi cha shule za EM zimeanza kuingia bongo kiliwakuta wazazi wangu wamejaliwa na Mungu uwezo. Wakaamua wanitoe kayumba na kunipeleka EM.

Kufika kule wale walimu walishangaa ni namna gani napaswa kuwa darasa la sita, wakati hakuna ninachokijua cha msingi. Kwa hio nikawa recommended nirudie la tano.

Aisee nilipigwa msasa, nakumbuka nilikuwa the slowest kid in class lakini nakuja kumaliza darasa la saba, ndio nilikuwa the best of the best student, kunyakuwa zawadi zote na pia kupata fursa ya kwenda special school ya serikali, kwenda special school za serikali ndio kipindi hicho zimeanza kupoteza uimara nikakutana ufundishaji mmbovu sanaaa.

Hadi hii leo kuna namna maisha yangu yalikuwa postively affected kutokana na malezi bora niliopata pale EM. Ninachokumbuka kayumba ni mwalimu aji darasani ni kupiga stori mkisubiria kengele, kutoroka shule kwa kuruka madirishani na kuingia mtaani kutafuta maembe, kuogelewa mtoni, etc, wenginne ndio walitekwa na kuchunwa ngozi, kuanza kuvuta bangi/madawa, etc

So mtu anaeponda EMs namshangaa sanaaaaa!!!

SO TUFANYEJE!!!
Kutokana na ongezeko la uhitaji wa elimu bora, shule za EMs zimekuwa nyingi huku nyingi zikishusha bei ili uje tu for the sake of "ninasomesha mtoto EM" , kwa hio tafuta shule yenye record nzuri ya malezi na matokeo bila ya kujali ada.

Kwa issue ya employment: ni aibu sana elimu aliopata mtoto wako unaipimia pale tu atapopata ajira. Unemployment nj global issue. Ni aibu unakuta unakunywa bia kila jioni, umepangishia kahaba au una suka misuko ya 50k kila baada ya wiki 1 na nusu alafu unasema kusoma EM ni kupoteza muda kwa maana hatakuja kupata ajira.
 
Binafsi sijaelewa hii kampeni ni ya nini na ni kwa maslahi ya nani.

Je inaendeshwa na victims (watoto waliosomeshwa EMs wakalost kwenye maisha) au inaendeshwa na wazazi (wenye kupenda watu wafanane/wafuate mitazamo yao)
 
Hapana dada ni watu waliofanya uamuzi kutokana na ukata wao basi wna taka wengie wawafate ili wawafariji.
 
IT IS A SIMPLE STORY BUT VERY MEANINGFUL....

Kile kipindi cha shule za EM zimeanza kuingia bongo kiliwakuta wazazi wangu wamejaliwa na Mungu uwezo. Wakaamua wanitoe kayumba na kunipeleka EM.

Kufika kule wale walimu walishangaa ni namna gani napaswa kuwa darasa la sita, wakati hakuna ninachokijua cha msingi. Kwa hio nikawa recommended nirudie la tano.

Aisee nilipigwa msasa, nakumbuka nilikuwa the slowest kid in class lakini nakuja kumaliza darasa la saba, ndio nilikuwa the best of the best student, kunyakuwa zawadi zote na pia kupata fursa ya kwenda special school ya serikali, kwenda special school za serikali ndio kipindi hicho zimeanza kupoteza uimara nikakutana ufundishaji mmbovu sanaaa.

Hadi hii leo kuna namna maisha yangu yalikuwa postively affected kutokana na malezi bora niliopata pale EM. Ninachokumbuka kayumba ni mwalimu aji darasani ni kupiga stori mkisubiria kengele, kutoroka shule kwa kuruka madirishani na kuingia mtaani kutafuta maembe, kuogelewa mtoni, etc, wenginne ndio walitekwa na kuchunwa ngozi, kuanza kuvuta bangi/madawa, etc

So mtu anaeponda EMs namshangaa sanaaaaa!!!

SO TUFANYEJE!!!
Kutokana na ongezeko la uhitaji wa elimu bora, shule za EMs zimekuwa nyingi huku nyingi zikishusha bei ili uje tu for the sake of "ninasomesha mtoto EM" , kwa hio tafuta shule yenye record nzuri ya malezi na matokeo bila ya kujali ada.

Kwa issue ya employment: ni aibu sana elimu aliopata mtoto wako unaipimia pale tu atapopata ajira. Unemployment nj global issue. Ni aibu unakuta unakunywa bia kila jioni, umepangishia kahaba au una suka misuko ya 50k kila baada ya wiki 1 na nusu alafu unasema kusoma EM ni kupoteza muda kwa maana hatakuja kupata ajira.
Usiombe yakukute kwenye Presentation za Chuo pale mbele 😅😅😅
 
Yani Dunia inakuelemea ukiwa katikati ya wanaojua Kingereza 😅😅😅sa hiyo huna wa kumlaumu. Uko peke yako, hujiwezi. Hadi Tell us about yourself inakutoa Jasho 😜😜😜😜😅😅
 
Make Kayumba schools great again.

Usijitese kusomesha watoto huko EMs, walete shule za jamii wapate Elimu bora huku ukiishi bila stress.

Binafsi nimesoma Taasisi za Serikali mwanzo mwisho, hata nilipokutana na hao waliosoma EMs hakuna walichonizidi zaidi ya kiingereza cha hapa na pale ila darasani hakuna walichonizidi.

LIKUD
 
Bottom line is, usifanye chochote kilicho nje ya uwezo wako.

Ikiwa una uwezo wa kulipa private school, ni busara kumpeleka mtoto huko. Hakuna faraja kwenye ufukara.
Kuna tofauti kubwa sana ya uelewa baina ya mtoto wa darasa la watoto 20 (Private school) na watoto 120 (Kayumba).

Mimi nashukuru Mungu ni product ya English Medium (Olympio ya 90's, St. Mary's ya late 90's, early 2000's na mwisho Uganda).

Ukiwa na chimbuko zuri la Primary, secondary unatoboa shule yeyote. Hili nililiona baada ya kuhamishwa toka St. Mary's na kupelekwa Uganda. Ilikuwa nikilinganisha baina yangu na wenzangu wa Tz waliotoka shule za kawaida, nilikuwa na advantage kubwa ya kuelewa ikizingatiwa mtaala wa Uganda ni wa kiingereza toka chekechea.

Mtoto wangu wa kwanza yupo Secondary (Form 2), toka nursery amesoma English medium na sekondari nimempeleka shule ya Serikali, so far hakuna gumu lolote analopitia kwa swala zima la uelewa.

Kiuhalisia kinachoangusha elimu ya Tz hasa primary ni lugha. Ni ngumu kwa mtoto kufundishwa kwa kiswahili toka chekechea halafu ghafla form 1 unabadili kila kitu kwenda kwa Kiingereza. Hatma ya huyo mtoto ni kukariri definitions kuliko kuelewa hasa kinachofundishwa. Na hii huendelea mpaka kwenye ajira.

Ni kawaida kukutana na mtu mwenye masters lakini uwezo wake wa kujielezea ni mdogo mno japo anajua kile anachopaswa kukielezea.

Ifike wakati serikali iende na wakati na kubadili mfumo wa lugha ya kufundishia na kuwa Kiingereza toka mwanzo. Na wale wanaojimithilisha na China kusema kuwa Kiingereza hakina umuhimu basi pia wamithilishe na uchumi wao.

For as long as sisi ni nchi maskini, kiingereza hakiepukiki katika kutafuta fursa za kidunia.
 
Kila mzazi apeleke mtoto anapoona panafaa kulingana na kipato chake!!!! Binafsi wa kwangu nitaangalia sehemu ambayo watasoma huku nikiwaandalia future yao....
Usome kayumba, Ems , International
Inatakiwa upate elimu ambayo ukiileta mtaani ikupe matokeo chanya. Elimu utajayopata popote inatakiwa ui apply kazini, kwenye biashara, kilimo, na hata hapo ulipo kwa maana ya familia, Elimu hiyo itupe utofauti wenye tija.
 
Hapana dada ni watu waliofanya uamuzi kutokana na ukata wao basi wna taka wengie wawafate ili wawafariji.
Ohh now i know! Lakini. Wasaidiwe… Kuna kitu kinaitwa acceptance, Ukiona mtu anahubiri sana kuungwa mkono kwenye situation yake ujue kuna tatizo.

Na atapona kama atakubali duniani si lazima tufanane..
 
Unajua Kuna mdau humu alisema "vazi la umaskini halijawahi kumfaa mtu hata kama ni suti"

Sasa Kuna watu wanajaribu kulipamba lionekane ni joho la kifalme.
Ngoja niseme Kwa Mb zangu hzi za 75%
-
Umaskini ukikukumba una tabia ya kukutpa hofu ya kuadhirika na kusababisha kutengeneza fact zisizo kuwa na uhalisia Kwa watu wa kitanzania.

Kama Mimi hapa sina hela sijala Toka asubuhi ila najipa moyo kuwa me ni kijana siwezi kuendeshwa na njaa ya siku Moja.

Tutafute hela wakuu umaskini mbaya.
 
Back
Top Bottom