Bottom line is, usifanye chochote kilicho nje ya uwezo wako.
Ikiwa una uwezo wa kulipa private school, ni busara kumpeleka mtoto huko. Hakuna faraja kwenye ufukara. Kuna tofauti kubwa sana ya uelewa baina ya mtoto wa darasa la watoto 20 (private school) na watoto 120 (Kayumba).
Mimi nashukuru Mungu ni product ya English Medium (Olympio ya 90's, St. Mary's ya late 90's, Early 2000's na mwisho Uganda).
Ukiwa na chimbuko zuri la Primary, secondary unatoboa shule yeyote. Hili nililiona baada ya kuhamishwa toka St. Mary's na kupelekwa Uganda. Ilikuwa nikiliganisha baina yangu na wenzangu wa Tz waliotoka shule za kawaida, nilikuwa na advantage kubwa ya kuelewa ikizingatiwa mtaala wa Uganda ni wa kiingereza toka chekechea.
Mtoto wangu wa kwanza yupo Secondary (Form 2) toka nursery amesoma English medium na sekondari nimempeleka shule ya Serikali, so far hakuna gumu lolote analopitia kwa swala zima la uelewa.
Kiuhalisia kinachoangusha elimu ya Tz hasa primary ni lugha. Ni ngumu kwa mtoto kufundishwa kwa kiswahili toka chekechea halafu ghafla form 1 unabadili kila kitu kwenda kwa Kiingereza. Hatma ya huyo mtoto ni kukariri definitions kuliko kuelewa hasa kinachofundishwa. Na hii huendelea mpaka kwenye ajira.
Ni kawaida kukutana na mtu mwenye masters lakini uwezo wake wa kujielezea ni mdogo mno japo anajua kile anachopaswa kukielezea.
Ifike wakati serikali iende na wakati na kubadili mfumo wa lugha ya kufundishia na kuwa Kiingereza toka mwanzo. Na wale wanaojimithilisha na China kusema kuwa Kiingereza hakina umuhimu basi pia wamithilishe na uchumi wao.
For as long as sisi ni nchi maskini, kiingereza hakiepukiki katika kutafuta fursa za kidunia.