Kutokana na hii story yangu hauwezi nikuta humu nashabikia kutoa watoto EMs na ISs na kuwapeleka kayumba

Kutokana na hii story yangu hauwezi nikuta humu nashabikia kutoa watoto EMs na ISs na kuwapeleka kayumba

Naona wamiliki wa shule za EM's baada ya kuona mnaharibiwa soko la biashara zenu mmeamua kujibu mapigo
🤣🤣🤣🤣🤣

Wabongo wamestuka now Kayumba ndio habari ya mjini. Hadi Naibu Waziri WA elimu last month aliongea
 
Bottom line is, usifanye chochote kilicho nje ya uwezo wako.

Ikiwa una uwezo wa kulipa private school, ni busara kumpeleka mtoto huko. Hakuna faraja kwenye ufukara. Kuna tofauti kubwa sana ya uelewa baina ya mtoto wa darasa la watoto 20 (private school) na watoto 120 (Kayumba).

Mimi nashukuru Mungu ni product ya English Medium (Olympio ya 90's, St. Mary's ya late 90's, Early 2000's na mwisho Uganda).

Ukiwa na chimbuko zuri la Primary, secondary unatoboa shule yeyote. Hili nililiona baada ya kuhamishwa toka St. Mary's na kupelekwa Uganda. Ilikuwa nikiliganisha baina yangu na wenzangu wa Tz waliotoka shule za kawaida, nilikuwa na advantage kubwa ya kuelewa ikizingatiwa mtaala wa Uganda ni wa kiingereza toka chekechea.

Mtoto wangu wa kwanza yupo Secondary (Form 2) toka nursery amesoma English medium na sekondari nimempeleka shule ya Serikali, so far hakuna gumu lolote analopitia kwa swala zima la uelewa.

Kiuhalisia kinachoangusha elimu ya Tz hasa primary ni lugha. Ni ngumu kwa mtoto kufundishwa kwa kiswahili toka chekechea halafu ghafla form 1 unabadili kila kitu kwenda kwa Kiingereza. Hatma ya huyo mtoto ni kukariri definitions kuliko kuelewa hasa kinachofundishwa. Na hii huendelea mpaka kwenye ajira.

Ni kawaida kukutana na mtu mwenye masters lakini uwezo wake wa kujielezea ni mdogo mno japo anajua kile anachopaswa kukielezea.

Ifike wakati serikali iende na wakati na kubadili mfumo wa lugha ya kufundishia na kuwa Kiingereza toka mwanzo. Na wale wanaojimithilisha na China kusema kuwa Kiingereza hakina umuhimu basi pia wamithilishe na uchumi wao.

For as long as sisi ni nchi maskini, kiingereza hakiepukiki katika kutafuta fursa za kidunia.
Kwa hizi busara wewe ungefaa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA. HAKUNA FARAJA KWENYE UFUKARA. Pia shule za msingi za zamani zilikuwa zina unafuu kutokana na uchache wa wanafunzi na waalimu wenye wito. Hata kama kiingereza hatukujua lakini angalau tuliweza kuwa na miandiko mizuri na mambo kama kuandika barua ya kikazi kwa kiswahili tuliweza. Sasa hivi ukimwambia mtoto wa darasa la 7 andika barua ya kikazi hawezi. Mimi naunga mkono hoja yako kuwa kiingereza kianzie darasa la kwanza.
 
Wazazi tutafuteni pesa

Money is better than education
Wenzako " education" is better than money ndio maana wana jikamua vimilioni wanavyo vipata Kwa tabu halafu eti wanaenda kuvichoma shule za EMs . Utoto raha Kweli u just think anyhow
 
Kwa hizi busara wewe ungefaa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA. HAKUNA FARAJA KWENYE UFUKARA. Pia shule za msingi za zamani zilikuwa zina unafuu kutokana na uchache wa wanafunzi na waalimu wenye wito. Hata kama kiingereza hatukujua lakini angalau tuliweza kuwa na miandiko mizuri na mambo kama kuandika barua ya kikazi kwa kiswahili tuliweza. Sasa hivi ukimwambia mtoto wa darasa la 7 andika barua ya kikazi hawezi. Mimi naunga mkono hoja yako kuwa kiingereza kianzie darasa la kwanza.
Shule nyingi za Kayumba wanafundisha English kuanzia chekechea japo rasmi ni kuanzia darasa la 3.


Halafu utajiri wa mtu haupimwi kwa kutazama shule ambayo mzazi unasomesha mtoto wako
 
IT IS A SIMPLE STORY BUT VERY MEANINGFUL....

Kile kipindi cha shule za EM zimeanza kuingia bongo kiliwakuta wazazi wangu wamejaliwa na Mungu uwezo. Wakaamua wanitoe kayumba na kunipeleka EM.

Kufika kule wale walimu walishangaa ni namna gani napaswa kuwa darasa la sita, wakati hakuna ninachokijua cha msingi. Kwa hio nikawa recommended nirudie la tano.

Aisee nilipigwa msasa, nakumbuka nilikuwa the slowest kid in class lakini nakuja kumaliza darasa la saba, ndio nilikuwa the best of the best student, kunyakuwa zawadi zote na pia kupata fursa ya kwenda special school ya serikali, kwenda special school za serikali ndio kipindi hicho zimeanza kupoteza uimara nikakutana ufundishaji mmbovu sanaaa.

Hadi hii leo kuna namna maisha yangu yalikuwa postively affected kutokana na malezi bora niliopata pale EM. Ninachokumbuka kayumba ni mwalimu aji darasani ni kupiga stori mkisubiria kengele, kutoroka shule kwa kuruka madirishani na kuingia mtaani kutafuta maembe, kuogelewa mtoni, etc, wenginne ndio walitekwa na kuchunwa ngozi, kuanza kuvuta bangi/madawa, etc

So mtu anaeponda EMs namshangaa sanaaaaa!!!

SO TUFANYEJE!!!
Kutokana na ongezeko la uhitaji wa elimu bora, shule za EMs zimekuwa nyingi huku nyingi zikishusha bei ili uje tu for the sake of "ninasomesha mtoto EM" , kwa hio tafuta shule yenye record nzuri ya malezi na matokeo bila ya kujali ada.

Kwa issue ya employment: ni aibu sana elimu aliopata mtoto wako unaipimia pale tu atapopata ajira. Unemployment nj global issue. Ni aibu unakuta unakunywa bia kila jioni, umepangishia kahaba au una suka misuko ya 50k kila baada ya wiki 1 na nusu alafu unasema kusoma EM ni kupoteza muda kwa maana hatakuja kupata ajira.
Kama wazazi wako hawakukusomesha kwenye shule zinazo fuata mtaala wa Cambridge za kulipa kuanzia walau milioni 25 Kwa mwaka basi they have just wasted their money for nothing
 
Mtoto wa EM hana chochote za ziada anachomzidi mtoto wa Kayumba ukiangalia kwa jicho la 3, hana. Mimi sio muumini wa matokeo ya As ama Bs ambazo zinapatikana EM kwa kuiba mitihani na mambo kama hayo. Mimi ni muumini wa analytics, watoto hawa wa EM zaidi ya matokeo hana kingine anachomzidi wa Kayumba.
Ukweli kabisa
 
Mimi ni product ya kayumba..from scratch Nina rafiki yangu yeye ni Yorke Mimi ni cole

Yeye ni rivaldo Mimi ni Ronaldo wa Brazil world cup 2002....yeye alisoma EMS Mimi kayumba.. yeye primary alisoma EMS na secondary ya private..Mimi nilisoma kayumba both level secondary thanksgiving kwa rafiki zangu wa Tano hk,omy,Kim,salva,jm,gnk na e.t.c mwaka juzi salva Ali ibuka mfanyakazi Bora kitaifa...Kuna mwaka nikiwa form one...
Mtiani ulikua mgumu nikataka kumwangalizia...akaniambia sm Mimi sipati shida kwenye mtiani huwa nasoma..
Ili usipate shida kwenye mtiani uwe unasoma... after that nilikua naweka syllabus yote kichwani kabla ya mtiani.... Kwa kila somo nikawa book monger's

Mimi nili kariri nili tumia nguvu miaka ya ELIMU ya form one mpaka four nikaenda shule ya vipaji maalum
 
Hapo ndiyo shida inapoanzia. Timedaganywa kwamba kujua kingereza ni kuwa na Akili nenda China utashangaa waafrica bado tu watumwa wanl wazungu 100%
Mkuu sio kwamba kujua kingereza ndo kuwa na akili, bali kujua kingereza kunasaidia sana kwenye elimu na maisha ya kawaida.
Inshort hakikwepeki
 
Yani Dunia inakuelemea ukiwa katikati ya wanaojua Kingereza 😅😅😅sa hiyo huna wa kumlaumu. Uko peke yako, hujiwezi. Hadi Tell us about yourself inakutoa Jasho 😜😜😜😜😅😅
Akili ndogo.
 
Sahihi kabisa mkuu. Halafu mtoa Mada hajui hata Nini maana ya private school.

What is private about EMS kama hawatumii mtaala wao wenyewe wana tumia mtaala wa NECTA?

Unaposema wewe ni private school maana Yake hata mtaala wako pia unapaswa kuwa private.

Sio unasema wewe ni private halafu mtaala unatumia wa public

The only private thing about shule za EMs za kibongo ni majengo Yao lakini everything about them is public

Hata English yenyewe hazifundishi isipokuwa kinacho fanyika ni just mentioning. Yani masomo kwenye shule za EMs yanakuwa mentioned in English na Sio kufundishwa in English.

Mtu ambae Sio mzungumzaji WA lugha ya kiingereza Kwa kuzaliwa hana uwezo WA kufundisha somo lolote lile Kwa lugha ya kiingereza but he can mention it in English.


Kama Kweli mzazi upo serious na hiyo unayoita elimu Kwa kiwango hicho Basi shule zinazo fundisha Kwa mtaala wa Cambridge ambazo ada zake ni walau kuanzia milioni 25 Kwa mwaka.


Lakini hizi za kumilikiwa na wakina Muggetta za kulipa milioni 2, 3 au 4 Kwa mwaka ni upuuzi mtupu
Kuna tofauti kati ya kusoma/ kufundisha kwenye darasa lenye wanafunzi 130 na darasa la wanafunzi 30/40. Kuna utofauti mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom