Kutokujua Kiingereza kunatukwamisha Watanzania kuingia Soko la ajira duniani

Kutokujua Kiingereza kunatukwamisha Watanzania kuingia Soko la ajira duniani

aya mambo sometimes adi uyaexperience ndo unaweza kuelewa kwann tunakwama.

unaeza kwenda kwenye vikao muhim uko duniani hlf mwenyewe upo na bosi wako mkongwe unayemwamini lakini utashangaa mwanzo mwisho bosi akinyanyua mdomo basi anatafuna karanga au korosho wala hasubutu kunyanyua mdomo kuongea na equals wenzake adi kikao kinaisha
Boss anaenda vikao kupata posho na kushangaa mazingira tu🤣
 
Si suala la IQ, kwa kiasi kikubwa sana ni suala la utamaduni.

Wabongo wengi hawana uwezo wa kufanya abstract na critical thinking, hata kufanya mawazo mapya tu ni kazi.

Kabla ya kufika kwenye Kiingereza. Hata kwa Kiswahili tu.

Hili ni suala la utamaduni na nurture. Si IQ na nature.

Haya si matatizo ya Kiingereza, kwa sababu hata hapa JF tunapotumia Kiswahili wenyewe kwa wenyewe tunayaona vizuri tu. Kiingereza kinayaongeza matatizo yaliyopo tayari.

Na tupo wabongo kibao tuliotoka kwenye mifumo ya Bongo, au ambao tulikuwa na misingi mizuri majumbani huko, tumeepuka matatizo hayo kwa kiasi kikubwa tukajiongeza kuja nje na tumeweza kufanya kazi vizuri tu.

Mimi tangu shule ya msingi nilikuwa napenda Kiingereza. Kwa sababu nilikuwa napenda kusoma halafu nilikuwa naona vibaya sana kuna vitabu vingi sana vimeandikwa Kiingereza halafu mimi siwezi kuvisoma. Nikawa navisoma kwa kutumia kamusi ya Kiswahili na Kiingereza kwa ubishi. Ilikuwa ngumu kwanza, lakini ilinisaidia kujenga msamiati na kuanza kuelewa polepole.

By the time nafika sekondari nikawa ndiye mtu wa kufanya presentation kwa Kiingereza watu wakitegeana.

Msingi huo ulinisaidia sana baadaye kwenda kufanya presentations Wall St, Canary Wharf, Exchange Place na online leading global projects daily kwa watu wa mabara yote ya dunia nikiongoza very complex na technical projects.

Na mimi sijihesabu kama mtu mwenye uwezo mkubwa sana wa asili (IQ). In fact napinga hoja nzima ya IQ. Najihesabu kama mtu ambaye nilipata bahati ya kuzaliwa sehemu fulani ambayo watu walianza kusoma mapema kwa standards zetu, wakajenga utamaduni wa kusoma, na mimi mwenyewe nikajiongeza kwa kuwa na passion ya kujifunza, kusoma, kuongea, si Kiingereza tu, bali mambo mapya mengi kama teknolojia.

Hili ni suala la maandalizi, mazingira na utamaduni kwa kiasi kikubwa sana, kuliko habari za IQ ambazo wasomi wa mambo ya clinical psychology wanapingana nayo.
Lakini Mkuu Uwezo wa kujifunza Lugha Mpya na kuielewa nao una determine IQ ya mtu
 
Asilimia kubwa ya wachina hawajui kiingereza lakini uchumi wao uko wapi?

Kazi kubet unadhani utapata mendeleo ya kiuchumi?
Mnaosemaga " wachina hawajui kingereza" ujinga huu mnasikiaga wapi?? Hamjasikia Sasa hivi vyuo vya marekani vinaleta ugumu Kwa wanafunzi wa kichina kujiunga na vyuo vyao??Google Taasisi yeyote ya China ambayo Ina wasomi wengi,60% utaona wamesoma Marekani hasa top scientists..

Na waliosoma China degree ya kwanza,ya pili or Masters wamesoma Ulaya au Marekani...

Kingereza wanajua vizuri ila wazalendo nyumbani hawaongei kingereza KABISA
 
Mnapendaga wabongo waendelee kuwa wajinga kwa kuwapa mifano ya kipumbavu kama hyo wasioendana nayo mapimbi nyie

Wakija maofisin kwenu kuomba kaz mnawainterview kwa kidhungu badala ya kiswahili pambafu
pimbi pumbaf mwenyewe kwani ulikatazwa kusoma kiingereza? nimetoa mfano wa wachina kwa vile wao huwa wanajifunza wenyewe.

na wewe wacha kubeti na kushabikia yanga na simba usiku na mchana nenda ukajifunze kiingereza huko.
 
Hiyo ni shida yako wewe binafsi unayetaka kwenda huko BRITAIN ndo ujifunze kiingereza...
Jifunze hiyo lugha yao il upate hizo pints...
daah 😤
tatizo apa jf hatujuani
unaeza kukaza shingo kumbe unabishana na mjasiriamali mdogo mfuga kuku wa uko igangabilili wilaya ya itilima
 
Twende mbele turudi nyuma haa basi tuende mbele.

Tukiacha siasa hii kitu inatuangusha sana kwenye majukwaa huko duniani. no wonder ndio maana wakenya wanatupiga gepu sana huko kwenye mashirika makubwa ya kimataifa

Huu ndio ukweli
Wachina hawajui ngeli na wameingia...
 
licha ya kutojua kiingereZa Pia Akili zetu watanzania ni ndogo sana tuna average IQ, mbongo na Mkongo man elewa zao haziachani sanaa, wale wanawaza muziki sisi tunawaza mpira na bongo freva.
Lugha inachangia sana kukuza IQ ya mtu. Kiswahili ni lugha maskini, haina misamiati mingi.

Angalia arguments za mtu anaye ongea kiingereza na ambaye anaongea Kiswahili, utagundua, anaye ongea Kiingereza Yuko deep zaidi ya yule anaye ongea Kiswahili kwa topic hiyo hiyo.
 
Ni ukweli mtupu, kulikuwa na mashindano ya Coca-Cola Africa mashariki kati ya vyuo vikuu, Tz tulianguka kwa swala la lugha ya malkia. Tujitahidi, Mkapa alijitahidi kufufua shule za medium ili tujikomboe. Tunataka watu kama professor Jonabi, alivyokuwa anajieleza sikuamini kama ni Mtanzania!
 
Lugha inachangia sana kukuza IQ ya mtu. Kiswahili ni lugha maskini, haina misamiati mingi.

Angalia arguments za mtu anaye ongea kiingereza na ambaye anaongea Kiswahili, utagundua, anaye ongea Kiingereza Yuko deep zaidi ya yule anaye ongea Kiswahili kwa topic hiyo hiyo.
Pia mfumo wa elimu wa kwetu hauyufindishe kua critical thinkers.
 
Wachina hawajui ngeli na wameingia...
Shida unajifananisha na Taifa lililopiga hatua kimaendeleo I.e Uchumi, Technolojia, miundombinu na Elimu.

Sisi tunahiihitaji sana Lugha ye Kiingereza ili ku break hii sintofahamu ya akili zetu duni.

Mbayw zaidi kila kitu tunachojifunza kiko katika Lugha ya Kiingereza, kutokujua kwetu lugha hii inatulimiti katika kujieleza katika ushindani, ubunifu na hata elimu
 
daah 😤
tatizo apa jf hatujuani
unaeza kukaza shingo kumbe unabishana na mjasiriamali mdogo mfuga kuku wa uko igangabilili wilaya ya itilima
Niko hapa hapa mjini ndugu yangu, pamoja na ajira ya kudumu niliyonayo lakini ni mjasiriliamali mdogo kweli ila si wa kuku , halafu ALUMNI wa MUCHS chini ya Pallangyo enzi ya Kikwete..
Tatizo wadanganyika na waafrika wengine bado tunaishi kwenye mind-set za kitumwa, tunapenda kuambiwa vitu laini vinavyozidi kutulemaza ufahamu , hatutaki kuambiwa vitu vya kutufikirisha nje ya tulivyomezeshwa na mifumo legevu ya Elimu iliyotukaririsha.
Lugha ni shida yako binafsi mzee, ukiona hiyo TOEFL score kwako ni mtihani kuna vyuo vipo kwa kazi hiyo ya kukupiga brush.
Taifa linalojielewa haliwezi kulazimika kutengeneza mtaala wa kutengeneza manamba mzee...
 
Lakini Mkuu Uwezo wa kujifunza Lugha Mpya na kuielewa nao una determine IQ ya mtu
Nakwambia suala zima la IQ ni hadithi kuliko ukweli.Wasoni wa clinical psychology wengi wanaikosoa dhana nzima ya IQ measurement.

Tafuta kitabu cha Jared Diamond "Guns, Germs, and Steel : The Fates of Human Sociesties".

Diamond kaandika kitabu kizima kuhusu kwa nini jamii fulani zinafanikiwa na nyingine hazifanikiwi. Kuna sura moja kachambua sana hoja ya IQ akakuta kuwa hoja haina mashiko kama watu wanavyofikiri, na mambo kama utamaduni na bahati ya kijiografia yana umuhinu zaidi.

Kuna siku nilikuwa nimekaa na wenzangu natamba kuwa mimi nilifanya jitihada binafsi tangu nikiwa mdogo kusoma vitabu vya Kiingereza kwenye library ya nyumbani, Tanganyika Library, Tambaza Secondary School Library, United States Information Services Library (Peugeot House), British Council (Samora Ave and Ohio St) etc. Kuna mtu akaniambia hayo ni matokeo ya kuwa na privilege kwenu mna library yenye vitabu, umezaliwa na wazazi waliosoma wamekuonesha library tangu mdogo, ulikuwa Dar kuna libraries zote hizo. Kwa hivyo hapo utaona mambo hayo yana umuhimu kuliko hiyo mnayoiita IQ.

Sasa mtu akiwa na uwezo mkubwa lakini kazaliwa kijijini huko hata kuongea Kiswahili ni tabu, unafikiri atajua Kiingereza?

Wewe unafikiri kwa nini wasomi wa zamani kina Nyerere, kina Kambona, kina Malecela, kina Mang'enya, kina Makani wale, kina Makwaia, baba zao kama si machifu basi ni wachungaji au walikuwa katika familia za karibu na machifu au kanisani? Unafikiri familia hizo tu ndiyo zilikuwa na watoto wenye akili? Wale walichaguliwa kwa sababu ya familia zao, kulikuwa na wengi kama wao hawakuchaguliwa.
 
Hoja nzuri,Tamaduni na bahati ya kijografia..

Tafiti za kisayansi zinasema waafrika hatuna Uwezo,hasa tulip kusini mwa Janga la Sahara..,na Kuna tofauti kubwa kati ya Mwafrika aliezaliwa na kukulia Africa na yule aliezaliwa ng'ambo...Je Mazingira yetu Kwa namna gani hayapo favoured?na wenzetu wanabebwa na Nini?? Tamaduni gani zinafanya tuwe duni??

Sure rahisi mzazi msomi kum-expose mtoto wake Katika Elimu kuliko mzazi ambae Hana elimu (privilege).

Mimi nilipenda kusoma sababu home Kuna makabati ya vitabu na hakukua na TV,so nikiwa home sina kazi Wala mahala pa kwenda option ilikua kusoma kitabu chochote chenye cover nzuri..
 
Back
Top Bottom