Kutokujua Kiingereza kunatukwamisha Watanzania kuingia Soko la ajira duniani

licha ya kutojua kiingereZa Pia Akili zetu watanzania ni ndogo sana tuna average IQ, mbongo na Mkongo man elewa zao haziachani sanaa, wale wanawaza muziki sisi tunawaza mpira na bongo freva.
Si suala la IQ, kwa kiasi kikubwa sana ni suala la utamaduni.

Wabongo wengi hawana uwezo wa kufanya abstract na critical thinking, hata kufanya mawazo mapya tu ni kazi.

Kabla ya kufika kwenye Kiingereza. Hata kwa Kiswahili tu.

Hili ni suala la utamaduni na nurture. Si IQ na nature.

Haya si matatizo ya Kiingereza, kwa sababu hata hapa JF tunapotumia Kiswahili wenyewe kwa wenyewe tunayaona vizuri tu. Kiingereza kinayaongeza matatizo yaliyopo tayari.

Na tupo wabongo kibao tuliotoka kwenye mifumo ya Bongo, au ambao tulikuwa na misingi mizuri majumbani huko, tumeepuka matatizo hayo kwa kiasi kikubwa tukajiongeza kuja nje na tumeweza kufanya kazi vizuri tu.

Mimi tangu shule ya msingi nilikuwa napenda Kiingereza. Kwa sababu nilikuwa napenda kusoma halafu nilikuwa naona vibaya sana kuna vitabu vingi sana vimeandikwa Kiingereza halafu mimi siwezi kuvisoma. Nikawa navisoma kwa kutumia kamusi ya Kiswahili na Kiingereza kwa ubishi. Ilikuwa ngumu kwanza, lakini ilinisaidia kujenga msamiati na kuanza kuelewa polepole.

By the time nafika sekondari nikawa ndiye mtu wa kufanya presentation kwa Kiingereza watu wakitegeana.

Msingi huo ulinisaidia sana baadaye kwenda kufanya presentations Wall St, Canary Wharf, Exchange Place na online leading global projects daily kwa watu wa mabara yote ya dunia nikiongoza very complex na technical projects.

Na mimi sijihesabu kama mtu mwenye uwezo mkubwa sana wa asili (IQ). In fact napinga hoja nzima ya IQ. Najihesabu kama mtu ambaye nilipata bahati ya kuzaliwa sehemu fulani ambayo watu walianza kusoma mapema kwa standards zetu, wakajenga utamaduni wa kusoma, na mimi mwenyewe nikajiongeza kwa kuwa na passion ya kujifunza, kusoma, kuongea, si Kiingereza tu, bali mambo mapya mengi kama teknolojia.

Hili ni suala la maandalizi, mazingira na utamaduni kwa kiasi kikubwa sana, kuliko habari za IQ ambazo wasomi wa mambo ya clinical psychology wanapingana nayo.
 
Mkuu ni kweli mfumo wetu wa alimu hautupi na fasi ya kua critical thinkers, jinsi ya uulizaji maaswali kujibu ni kukalilisahwa tu, masawali ya multiple choice hayasaidie mtoto kufikilia,........elimu elisaha kufa kwasbb ya siasa
 
Kanini waende uingereza wakati hapa hapa bongo kuna fursa. English muhimu sana
Huyo anaishi mwaka 1985.

Badala awaze kutengeneza ajira. Ye ye anawaza kuajiriwa.

Na kama hao waajiri anao wataja wanahitaji watu wanao jua kiingereza kwanini wasiende zao Uingereza moja kwa moja kwa watu ambao ndio lugha Yao kabisa waje kwako wewe ambae umefanya kujifunza?
 
Jichanganye, wachina english ni mandatory elimu yao, huwez tengeneza products na kufanya biashara na mataifa mengine halaf hujui english

Lugha inakuzwa na ushawishi na uchumi wannchi husika
Wachina😀 ni bora ni msikilize Mtanzania akizungumza kiingereza ila sio mchina.
 
Kwamba Watanzania mkijua kiingereza wamarekani wataacha kuchukua wachina,wahindi,wakorea,wajapan,wayahudi na wazungu wenzao watakuchukua wewe Mtanzania kwenye fani fulani kisa unajua kiingereza ? 😀 ujue kuna ujinga mwingi humu akianani
 
Hakuna ajira unayokosa sababu ya Lugha, nchi nyingi hata Kiingereza wanaojua ni wachache,,, ajira za kimataifa ni jambo la mtu binafsi siyo sera wala shida ya Taifa zima,,, anayetaka kwenda nje ajisomeshe lugha anayotaka kuijua.
 
Wao kufanya biashara kwa kutumia majina ya vivution ,kama hiyo ndia cause basi unajua kidogo mno?

Airtz iko wapi kuhakikisha wanatumia vya kwao effective?

Tz haijajipanga kikamilifu bado sana
Ndege ni national carriers.

Siyo biashara za kutegemea sana.

Hata hiyo KQ imejaa hasara kila siku.

Bahati nzuri haiendeshwi kwa kodi za wakenya.

Imeorodheshwa NSE.
 
Hio sio hoja, Tatizo kuu ni kua watz hatupamabani kutika kutafuta fursa nje ya nchi, tumeridhika sana na maisha yetu. Na pia Serikali haitoi support na wala kutafutia connection kwa wananchi wake. Hayo mambo ya lugha sio hoja yenye mashiko.
 
Asilimia kubwa ya wachina hawajui kiingereza lakini uchumi wao uko wapi?

Kazi kubet unadhani utapata mendeleo ya kiuchumi?
Hiyo ni kauli potofu, kwa taarifa yako tu wanaanza kusoma kuanzia third grade, na kuendelea

China anafanya biashara ya ushindani na mataifa makubwa, US, europe, uta win vipi bila kujua namna ya kuwafikia wateja kwa lugha yao?
 
mimi nimekwambia asilimia kubwa na siyo mia, hata hapa kwetu private sector wengi wanajua kiingereza
 
Back
Top Bottom