Kutoza watu pesa kuingia viwanja vya Sabasaba na Nanenane haijakaa sawa

Zamani tukienda 7 7 ilikuwa tukifika saa nne asubuhi moja kwa moja banda la TBL [emoji481] na mabaharia wenzangu
Ilikuwa ukiagiza bia 1 unapewa 1 ya offer,ukiagiza tena unapewa 1
Ilikuwa si mchz...
.miaka ya sahv hamna mambo hayo

Ova
 
Nadhani tukiachana na mapato basi ile fee ni njia ya kudhibiti idadi ya watu wanaoingia ndani sehemu hizo.

Sehemu kama Dsm ikiwa free kule ndani pangejaa mateja hata kukabwa tungekabwa
 
Huu utaratibu mbona upo miaka nenda! Saba saba na Nane nane, miaka yote huwa na kiingilio.

Kumbuka kuna kuna maandalizi ya hayo maonesho. Gharama za kufidia zitatoka wapi iwapo tutaingia bure?
Ni uhuni wa miaka mingi. Wanapata pesa nyingi kutoka kwa wenye mabanda na wanaofanyabiashara mule ndani.

Mkulima unamtozaje pesa kwenda kujifunza masuala ya kilimo? Mbona wafanyakazi hawatozwi viingilio?
 
Nadhani tukiachana na mapato basi ile fee ni njia ya kudhibiti idadi ya watu wanaoingia ndani sehemu hizo.

Sehemu kama Dsm ikiwa free kule ndani pangejaa mateja hata kukabwa tungekabwa
Mbona zamani nanenane tuliingia bure na hakukuwa na uhuni wowote! Kama watu wengi wafanye kila wilaya.
 
Kwanini wakulima na wafanyabiashara watozwe pesa kuingia kuangalia mambo siku ya sikukuu zao? Mbona wafanyakazi hawatozwi pesa kuingia viwanjani siku ya mei mosi?

Waandaaji watafute namna ya kupata pesa lakini siyo kuchaji wakulima na wafanyabiashara. Ni utapeli.
Cha bure ni hewa tu unayovuta vingine vinahitaji gharama
 
Nyie mnaolalamika mmekuja Dar na malori ya magimbi..? Huo utaratibu upo tangu enzi na enzi. Sabasaba77 ni International Business Exhibition msifikiri ni maonyesho ya Siku ya Gulio katerero au kishumundu...
Nilihudhuria Dubai Expro sikuona mtu akinidai kiingilio siku tatu mfululizo. Wanachohitaji ni kujisajili.

Halafu nikuulize, kwenye mikutano ya siasa mbona hamdai viingilio? Siku ya kuvunja matofali na kuonyesha silaha za kivita mbona hamdai viingilio?
 
Badili mtazamo, kitu kuwepo tangu kitambo hakiwezi kuwa kigezo cha kuthibitisha uhalali wake. Mabadiliko hayana budi kuja ikiwa ni ya muhimu. -Wanaorusha matangazo ya 77 kwenye tv na redio wanalipia sh ngapi?
- wafanyabiashara wanaongesha biashara zao na ubunifu wao wanalipaje?

Wangeweza hata kuificha hiyo tozo kwenye bei ya kila bidhaa mtu anayonunua ili kuzuia wafanyabiashara wasitumie maonyesho kama sehemu ya kuuza hivyo kushika nafas kubwa ya kuweka bidhaa nyingi za aina moja hadi sehemu za kupita zinakuwa finyu, pale tuonyeshwe tu tukanunue huko kwao madukani
 
Pia kama kuna watu kutoka mataifa ya nje basi wawekewe utaratibu wao mbona kitu simple tu hii nchi kila sehemu ukigusa utasikia hii haiwezekan kuwa kipo tangu Nyerere huwa najiuliza sana dunia inaenda kasi kuna maeneo lazima twende sawa na dunia
 
Uliingia kwa ticket ya "Standard" ambayo inakua limited na muda. Maonyesho ya Dubai yanaenda miezi zaid ya 3-6 ili kuruhusu watu kutoka mataifa mbalimbali kufika... Halafu ukumbuke ulienda kama mtalii/mgeni nchini Dubai, kwahio tayari kuna indirect fees wamekuchaji...
Hakuna maonyesho ya bure duniani lazima charges ziwepo
 
Nitajie

Nitajie nchi yenye International Business Exhibition na kiingilio ni miguu yako?
 
Uliingia kwa ticket ya "Standard" ambayo inakua limited na muda. Maonyesho ya Dubai yanaenda miezi zaid ya 3-6 ili kuruhusu watu kutoka mataifa mbalimbali kufika... Halafu ukumbuke ulienda kama mtalii/mgeni nchini Dubai, kwahio tayari kuna indirect fees wamekuchaji...
Hakuna maonyesho ya bure duniani lazima charges ziwepo
Sasa kama ni hivyo ndio kufanyike changes kama hivyo au kulingana na mahitaj yetu kama nchi
 
Badili mtazamo, kitu kuwepo tangu kitambo hakiwezi kuwa kigezo cha kuthibitisha uhalali wake. Mabadiliko hayana budi kuja ikiwa ni ya muhimu. -Wanaorusha matangazo ya 77 kwenye tv na redio wanalipia sh ngapi?
- wafanyabiashara wanaongesha biashara zao na ubunifu wao wanalipaje?

Wangeweza hata kuificha hiyo tozo kwenye bei ya kila bidhaa mtu anayonunua ili kuzuia wafanyabiashara wasitumie maonyesho kama sehemu ya kuuza hivyo kushika nafas kubwa ya kuweka bidhaa nyingi za aina moja hadi sehemu za kupita zinakuwa finyu, pale tuonyeshwe tu tukanunue huko kwao madukani
Wabongo mnataka turudi enzi za ujima... Duniani kote hakuna Free entry ktk maonyesho ya kimataifa...
 
Cha bure ni hewa tu unayovuta vingine vinahitaji gharama
Hata hewa yenyewe Mrusi anaelekea kuimalizia kwenye mitungi ya Iskander. Soon kila mtu atatembea na birika lake la gesi ya Oksijeni mgongoni, baada ya kulipia bili yake pale TRA Magogoni 🙂 🙂 🙂
 
Saba saba ipi watu walikuwa wanaingia bure .....

Ova
Wewe tozo huzioni? Hadi nywele bandia na kodi ya kichwa, Mguu wa Chumba anaziandaa, soon zinaingizwa kwenye chaneli mtaani.

Upofu wa serikali huuoni? Upigaji wa kasi ya 10G hujauona? Miradi? Safari kibao za Uarabuni na Marekani kwenye Royo Tuwa? Wamaasai Serengeti & Loliondo? Machinga? Hivi soko la Kariakoo liko sehemu gani vile?

Halafu, mmekopa trilioni ngapi hadi sasa? Vipi kuhusu usimamizi wa mali za umma na udhibiti wa matumizi ya rasimali na fedha?
 
Mkurugenzi yupo humu nadhani ni msikivu so next year anaweza kulifanyia kazi.
 
Huu utaratibu mbona upo miaka nenda! Saba saba na Nane nane, miaka yote huwa na kiingilio.

Kumbuka kuna kuna maandalizi ya hayo maonesho. Gharama za kufidia zitatoka wapi iwapo tutaingia bure?
Gharama za maonyesho zinalipwa na waonyeshaji tatizo ni matumizi wizi mtupu
 
Back
Top Bottom