Kutoza watu pesa kuingia viwanja vya Sabasaba na Nanenane haijakaa sawa

Kutoza watu pesa kuingia viwanja vya Sabasaba na Nanenane haijakaa sawa

Huu utaratibu mbona upo miaka nenda! Saba saba na Nane nane, miaka yote huwa na kiingilio.

Kumbuka kuna maandalizi ya hayo maonesho. Gharama za kufidia zitatoka wapi iwapo tutaingia bure?
Mimi nafikiri kuna haja Sasa kwa Tanzania kuwa na Sikukuu za:-

1. Moja Moja
2. Mbili Mbili
3. Tatu Tatu
4. Nne Nne
5. Tano Tano
6. Sita Sita
9. Tisa Tisa
10. Kumi Kumi
11. Kumi na Moja Kumi na Moja
12. Kumi na Mbili Kumi na Mbili
 
Kuna tofauti KUBWA SANA kati ya kujinasibu kisha kudiriki dhahiri shahiri kupambana dhidi ya upigaji, na kuwahamasisha ^war-who-knee^ wale kadiri ya urefu wa kamba zao. Huu ni ushamba wa kiwango cha Iskander.
Mkuu sasa tufanyaje
Hatuna jinsi,waache wale
Wapige mpaka wenyewe waseme inatosha..

Ova
 
Nilienda nchi moja hata kushiriki/kuona wakati wakichoma maiti zao kuna kiingilio nililipa $10.

Bure ni ghali na inapoteza heshima na utu wa mtu.
77 ikiwa bure nadhani watu watakuwa wengi kuliko ukubwa wa eneo mwisho wa siku ni wizi,vifo nk lile ni tukio la mara moja kwa mwaka hivyo mtu anatakiwa ajiandae kiuchumi kwenda 77 kwa kulipa kiingilio kuona bidhaa/huduma na kununua.
 
Mimi nafikiri kuna haja Sasa kwa Tanzania kuwa na Sikukuu za:-

1. Moja Moja
2. Mbili Mbili
3. Tatu Tatu
4. Nne Nne
5. Tano Tano
6. Sita Sita
9. Tisa Tisa
10. Kumi Kumi
11. Kumi na Moja Kumi na Moja
12. Kumi na Mbili Kumi na Mbili
Hii Saba saba miaka ya nyuma ilikuwa ni sikukuu kubwa sana. Na chimbuko lake lilikuwa ni kuzaliwa kwa chama cha TANU tarehe na mwezi huo, mwaka 1954! Na ilikuwa ni sikukuu ya wakulima!

Sasa miaka ya 90 wakaleta mambo ya Nane Nane kama mbadala wa Saba saba! Na hii saba saba ikafanywa kuwa siku ya maonesho ya nini sijui.
 
Mkuu sasa tufanyaje
Hatuna jinsi,waache wale
Wapige mpaka wenyewe waseme inatosha..

Ova
Ulivyo mwoga hata hutaki kujitoa mhanga kwa ajili ya wajukuu zako watakaozaliwa huko 2070?

^If we speak the truth, we die; if we keep quiet, we die. I, Dinno Melaye, has chosen to speak the truth and die!^ 🙂 🙂 🙂

(From conman: Senator Dinno Melaye)
 
Huu utaratibu mbona upo miaka nenda! Saba saba na Nane nane, miaka yote huwa na kiingilio.

Kumbuka kuna maandalizi ya hayo maonesho. Gharama za kufidia zitatoka wapi iwapo tutaingia bure?
Tafuteni fedha sehemu zingine ili wakulima wanaowauzia mazao kwa bei ndogo waje kupata Elimu wengi wa wanaokuja ni wale wanaojiweza na wa mjini mpo busy kugharamia mwenge vitu vya msingi mnaulizia mtapata wapi pesa ila naamini kizazi kijacho kinachojitambua kitaondoa hizo mambo wacha tuendelee kuwaibia wakulima haki zao...
 
Muhula huu wa utawala wa ^war-who-knee,^ manyang'au yamepania kuwapiga, kuwabinya, kuwaguyuguza na kuwakamua raia hadi furaha na shangwe yao ya the last five years ipotolee kusikojulikana. Ni mwendo wa ^REDO!^

Anyways, BETTER DAYS TO COME! Freedom is coming tomorrow!
Lakini Hili analolisema mtoa mada halijaanza leo
 
Lakini Hili analolisema mtoa mada halijaanza leo



Ni nini unachotaka kujaribu kuandika? [emoji2369]

Kwamba kwa kuwa halijaanza leo ndio kusema haiwezekani kuwa lilikuwa likifanyika kimakosa kwa miaka mingi ?

Je hata kama limekuwa likifanyika kimakosa liachwe na kuendelea kufanyika kimakosa?

Au marekebisho yaanze kufanyika sasa ?

Jambo kufanyika Kwa muda mrefu haina maana kwamba limekuwa likifanyika Kwa usahihi muda wote.
 
Lakini Hili analolisema mtoa mada halijaanza leo
Lakini awamu hii ndipo tumesikia kauli tata kama:

^Nafungulia nchi!^

^Kuleni urefu wa kamba zenu!^

^Hili nalo hebu mkalitizame!^

^Wanaoiba madini, hebu waache mara moja!^

^Wakandarasi embu jitahidi jamani. N'takuja tena kuwachungulia chungulia!^
 
Back
Top Bottom