Mtu akishakufa hasikii wala hajui kinachoendelea duniani.
Akishatoka ulimwengu huu,akiwa katika roho na nafsi yake (bila mwili ambao unarudi kuwa mavumbi) anaenda katika ulimwengu mwingine tofauti na huu.
Isipokuwa akiwa kule anaweza kukumbuka yale aliyofanya duniani kabla hajafa! Mfano ni huyu tajiri alikumbuka watu wa duniani na kuomba wasije huku alikokuwa ametupwa,(Luka16:22-31)
Kule kuna Peponi au rahani na Kuzimu kwenye mateso ya moto! Mtu anaenda kuishi huko kulingana na jinsi alivyoishi alipokuwa duniani! Kama alitubu dhambi na kuishi maisha ya usafi na utakatifu akifa anaenda peponi,(Luka23:43),(Luka16:19-22).
Kama hakutubu dhambi zake akaendelea katika maisha ya dhambi akifa anaenda Kuzimu kwenye mateso ya moto,(Luka16:22-31)
Angalizo! Hata marehemu angeombewa kiasi gani,sala,sawala au maombi ya watu hapa duniani hayasikilizwi! Pale viongozi wanapowaombea sijui ee! Iweke roho ya mtu mahali PEMA Peponi au kuwasikizisha maneno sijui ukiulizwa mtume wako ni nani-Hayo ni maneno ya kuwafariji wafiwa.
Kingali mtu anaishi aache dhambi,atubu dhambi aishi maisha mema! Akifa hakuna haja ya kuombewa! Anaingia mahali PEMA PEPONI MOJA KWA MOJA!