Kuuliza si ujinga, Mtu akifariki watu wanasema Apumzike kwa Amani huwa wanamwambia marehemu au wanamaanisha nini?

Kuuliza si ujinga, Mtu akifariki watu wanasema Apumzike kwa Amani huwa wanamwambia marehemu au wanamaanisha nini?

wakuu ni aje
Leo naomba kuuliza, kwanini mtu akifariki utaona watu wanaandika RIP au pumzika kwa Amani ndugu fulani au Mr fulani au Mrs fulani.
Hivi huwa wanamwambia Nani?! Marehemu au huwa wanamaanisha nini? Au ni tamaduni tu kama vile kunywa chai asubuhi japo hata usippkunywa haufi!
Wajuzi wa mambo karibuni.

R.I.P Wameiga kwa makafiri wa kimagharibi, na haina maana yoyote, wao wanafikiri marehemu anaenda kupumzika!
 
Jaribu ufe leo. Tutakupumzisha kwa amani kama waliotangualia!
You just kufa.
 
Mkuu kabla ya kuzaliwa si ulipumzika mabilioni ya miaka sasa unataka upumzike nini tena na maisha ni miaka 50 tu ukiwa na nguvu ni 60!!
Miaka 50 unazurura duniani mkuu halafu Tanganyika.
 
Hakuna kitu nje ya space, time na universe kwa ujumla.
🤣🤣🤣kwani mkuu Mbona kuna vitu vinandelewa kugunduliwa?
Mimi swali langu Kwann unahitimisha kwamba hakuna kitu? Katika ulimwengu huu na teknolojia inayokuwa kila siku kwa kasi tusiseme siku moja sayansi itatuletea majibu kuhusu kifo au baada ya kifo? Kwanini unalazimisha hakuna?
Wakati tunaona vitu vinakuwa modified na fumbuzi nyingi zinaendelea kuvumbuliwa na majibu kupatikana
 
wakuu ni aje
Leo naomba kuuliza, kwanini mtu akifariki utaona watu wanaandika RIP au pumzika kwa Amani ndugu fulani au Mr fulani au Mrs fulani.
Hivi huwa wanamwambia Nani?! Marehemu au huwa wanamaanisha nini? Au ni tamaduni tu kama vile kunywa chai asubuhi japo hata usippkunywa haufi!
Wajuzi wa mambo karibuni.
Ukifariki ndio utakuja kujua maana yake..
 
Marehemu ni mtu aliyekufa mwili but roho yake inaishi - ipo. Mwili wako unaweza uka-shut down (ukafa) na roho yako isipate pumziko - May his/her soul rest in peace - ni kuitakia matashi mema tu...

Ni sawasawa na kumwambia mtu - safari njema, ufike salama, ulale salama, kazi njema n.k Hizi ni good wishes tu
acha siasa mkuu
 
R.I.P Wameiga kwa makafiri wa kimagharibi, na haina maana yoyote, wao wanafikiri marehemu anaenda kupumzika!
Ina maana makafir wao wamemuiga nani?
Kama marehemu hawaendi kupumzika wanafanya nini huko? Na wewe umejuaje?🤣🤣
 
Hata sayansi kwenye masuala ya mungu ipo neutral haisimami upande wowote sababu kila siku tafiti zinaendelea.
Mimi mekuuliza swali jepesi ukaleta stori zingine. Kwanini ni rahisi kusema hakuna kitu lakini si rahisi kusema kwamba hatujui? TutajuJe maendeleo ya sayansi miaka 200 inayokuja itakuwa na majibu kiasi chake au kuna vitu vitakuwa vimevumbuliwa?😂😂
Kwanini ni lazima kwamba baadda yakifo hakuna kitu na si kwamba hatujui sababu sayansi inaweza kuvumbua kitu fulani miaka 500 baadae kuhusu kifo?

Kwanini unahitimisha hakuna kitu?
Kifo kipo ndani ya universe, time and space.

Hivyo tunaweza kupima na kujua kwamba baada ya kifo cha kiumbe husika au kitu husika "Existence" ya hicho kitu hubadilika kutoka state moja kwenda state nyingine hapa hapa duniani.

Kiumbe hai hubadilika na kuwa udongo kisha kuwa sehemu ya udongo uliopo ndani ya ardhi ya dunia underground.

Nje ya hapo kitu hicho kilichokufa Hakipo kwa namna yoyote ile.

Vitu ni energy tuna change from one state to another hapa hapa duniani.
 
Mtu akishakufa hasikii wala hajui kinachoendelea duniani.
Akishatoka ulimwengu huu,akiwa katika roho na nafsi yake (bila mwili ambao unarudi kuwa mavumbi) anaenda katika ulimwengu mwingine tofauti na huu.
Isipokuwa akiwa kule anaweza kukumbuka yale aliyofanya duniani kabla hajafa! Mfano ni huyu tajiri alikumbuka watu wa duniani na kuomba wasije huku alikokuwa ametupwa,(Luka16:22-31)
Kule kuna Peponi au rahani na Kuzimu kwenye mateso ya moto! Mtu anaenda kuishi huko kulingana na jinsi alivyoishi alipokuwa duniani! Kama alitubu dhambi na kuishi maisha ya usafi na utakatifu akifa anaenda peponi,(Luka23:43),(Luka16:19-22).
Kama hakutubu dhambi zake akaendelea katika maisha ya dhambi akifa anaenda Kuzimu kwenye mateso ya moto,(Luka16:22-31)
Angalizo! Hata marehemu angeombewa kiasi gani,sala,sawala au maombi ya watu hapa duniani hayasikilizwi! Pale viongozi wanapowaombea sijui ee! Iweke roho ya mtu mahali PEMA Peponi au kuwasikizisha maneno sijui ukiulizwa mtume wako ni nani-Hayo ni maneno ya kuwafariji wafiwa.
Kingali mtu anaishi aache dhambi,atubu dhambi aishi maisha mema! Akifa hakuna haja ya kuombewa! Anaingia mahali PEMA PEPONI MOJA KWA MOJA!
 
labda sababu upo na fake ID huenda nakufahamu . Kama unayo ikawa tested na verified lazima watu was mini na tuanze kutumia.
Hao wote walifanya chunguzi baadae watu wakaja kuziboresha zaidi. Na wapo waliokuja na theories nyingi zikawa criticised na watu wakaja kuzifanyia tafiti Ilya na zikazaa matunda.
Ndio maana nikakuuliza Kwanini unasema sayansi ilishatoa majibu wakati sayansi ya mwaka 1800 si hii ya mwaka 2023. Sababu ya kukua kwa teknolojia Kwanini unahitimisha kwamba hakuna kitu? Kwanini usiseme hatujui sababu maendeleo ya sayansi yanavyokua May be somedays in future miaka 500 kutakuwa na majibu?
Sijui kama unaelewa lakini🤣🤣
Nakuelewa sana mkuu sema wewe ndio hautaki kunielewa mimi , kwanza nikuelezee tu situmii,fake id kwa kuhofu chochote, ilitokea tu kutumia ila sasa naona ni vizuri nitumie tu ili tuweze kujadiliana na kila mtu , na kukuhakikishia kwa jinsi wa tz walivyo wanafki kuna watu wangetumia I'd zao za ukweli kuna wimbi kubwa humu lingegeuka machawa badala ya wachangiaji.
 
🤣🤣🤣kwani mkuu Mbona kuna vitu vinandelewa kugunduliwa?
Vina gunduliwa kwenye universe na ndani ya dunia ambayo ipo sio nje ya hapo.
Mimi swali langu Kwann unahitimisha kwamba hakuna kitu? Katika ulimwengu huu na teknolojia inayokuwa kila siku kwa kasi tusiseme siku moja sayansi itatuletea majibu kuhusu kifo au baada ya kifo? Kwanini unalazimisha hakuna?
Wakati tunaona vitu vinakuwa modified na fumbuzi nyingi zinaendelea kuvumbuliwa na majibu kupatikana
Baada ya kifo, Kitu kipo.

Si kwamba hakipo, ila kinachotokea baada ya kifo ni kwamba kitu kina change from one state to another state.

Mtu anaoza na kuwa udongo.
 
utaelewaje biblia bila kutumia akili
Ili uelewe mambo ya kiimani inabdi uweke akili njema pembeni utumie akili ya kizuzu , mfano , nuhu aliingiza wanyama wawili wawili aina zote kwenye kisafina maji yakajaa dunia nzima , hii unaweza kuielewa bila kuwa na akili ya kipopoma?
 
Baada ya kifo wapi?

Kifo ndio mwisho wa uwepo wa kitu hapa duniani.

Sasa kama unadhani kuna kitu kipo baada ya kifo, inabidi ueleze kinakuwepo sehemu gani tofauti na hii Universe ambayo ipo.

Hakuna kitu nje ya space, time na universe kwa ujumla.

Kila kitu hata kifo kipo ndani ya universe, time and space.

Nje ya hapo hakuna kitu.
Hakuna kitu ni nini mkuu?
 
Ili uelewe mambo ya kiimani inabdi uweke akili njema pembeni utumie akili ya kizuzu , mfano , nuhu aliingiza wanyama wawili wawili aina zote kwenye kisafina maji yakajaa dunia nzima , hii unaweza kuielewa bila kuwa na akili ya kipopoma?
unaposema kisafina una maana gani?
Maana tafsiri ya ki mara nying ni kitu kidogo na Li mara nyingi ni likitu likubwa.
Embu tueleweshe kisafina una maana gani?🤣🤣
 
Ili uelewe mambo ya kiimani inabdi uweke akili njema pembeni utumie akili ya kizuzu , mfano , nuhu aliingiza wanyama wawili wawili aina zote kwenye kisafina maji yakajaa dunia nzima , hii unaweza kuielewa bila kuwa na akili ya kipopoma?
mkuu kuna sehemu imeandikwa nuhu aliingiza wanyama safinani
hebu tuwekee hapa tuone kama akili zako zipo sawa au unaambiwa tu na huchanganyi na za kwako
 
Back
Top Bottom