Mwanamaji
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 2,905
- 4,518
Argument yangu mimi iko very simple, sijui hata kwanini umenikandika miswali yote hiyo.Ni dini gani iliyojenga viwanda vya kutengeneza Hijab, kanzu, suti au majuba? Mungu alitosha, anatosha na atatosha hata kesho, mavazi sio dini, hayatengenezwi na dini na wala hayatoki mwa mungu na hutaenda peponi kwa mavazi tu. Tunawaonea wanawake kwanini? Mbona wanaume nao wanatembe vichwa, vifua na mabaya vikiwa wazi? mbona wanawake hawahoji?
Labda nirudie:
Mwenyezi Mungu ametoa ridhaa ya mwanadamu kuishi kulingana na vile anavyoona inafaa, na pia kuwajibika na madhara au matokeo (consequences) ya machaguo hayo.
Ukiamua kuabudu masanamu, hana shida na wewe, ila uwe tayari kwa consequences za wewe kuchagua kuabudu hayo masanamu. (Angeweza kulizuia hili lisitokee kama angetaka, lakini ameliruhusu litokee kwa sababu anaheshimu UHURU WA MWANADAMU KUJICHAGULIA HATMA YAKE YEYE MWENYEWE)
Hivyo basi, kama wewe KAVULATA unataka kutembea uchi, bila viatu. RUKSA. (Maana huo ndio utaratibu wako)
Wanaotaka kuvaa hijab. RUKSA. (Na wao huo ndio utaratibu wao)
Anayetaka kutembelea mgongo badala ya miguu. RUKSA (Nayeye huo ndio utaratibu wake).
Tatizo ni pale "sisi binadamu" tunapotaka kuanza kuwalazimisha wengine wafuate machaguo yetu.
Mifano:
1. Watu wa Iran wanawalazimisha watu wasiotaka kuvaa hijab, wavae hijab. (TATIZO HILO)
2. Wewe Kavulata unawalazimisha watu wanaoamini kwamba kuvaa hijab ndio utaratibu sahihi, wasiamini hivyo. (TATIZO HILO).