Hapana hapana hapana, vitu vyote muhimu vya MwenyeziMungu hajaviacha huru ili wewe ujichagulie ufanye au uache, vitu vyote kutoka kwa Mungu ni lazima ufanye la sivyo utakufa hapohapo au utasambaratika. Kwakuwa Mungu amekuumba yeye anajuwa ni lipi unaweza na lipi unashindwa kama vile wewe usivyoweza kupakia container kwenye bajaj. Mungu anataka wewe upumue hivyo ni lazima upumue la sivyo utakufa, anataka ule chakula, utoe haja kubwa na ndogo, ulale usingizi, uzae, uchukie, ucheke, ukohoe, nk huwezi kujichagulia neno la Mungu. Kama hijab ingekuwa ni kwaajili ya mungu mtu angekufa hapohapo akiivua au akiikosa. Hijab isisababishe watu kuuana, ndoa kuvunjika, watu kudharauliana nk kwakuwa hijab sio dini, it is something nice to have, sio lazima wala muhimu/.
Nadhani mimi nawewe tunaongea kitu kimoja. Anayetaka kuvaa hijab avae, asiyetaka asivae.
Kumlazimisha mtu asiyetaka kuvaa hijab, aivae. Hilo ni kosa ambalo tunalifanya sisi binadamu.
Kuhusu mifano yako, sijui ni wapi tunabishana au kupingana ndugu yangu.
Kwa uchache Mungu ameumba binadamu na kumpangia utaratibu wa kula, kupumua, n.k lakini amemuachia chaguo yeye (binadamu) aamue nini afanye, nini asifanye with an associated consequence.
Binadamu akiamua kula na kupumua, consequence yake anaishi.
Binadamu akiamua kukataa kupumua (akajiziba pumzi) na akaamua kukataa kula, consequence yake atakufa.
Chaguo ni la binadamu, Mungu hakulazimishi ule au usile, hilo ni chaguo lako kulingana na utashi wako.
Yeye ameweka tu utaratibu ila suala la kuufuata au kutokuufuata ni juu yako.
Katika hatua nyingine, Mungu ameweka utaratibu wa kumuabudu.
Ukichagua kumuabudu, kuna consequences za kufanya hivyo. Ukichagua kutokumuabudu kuna consequences zake pia. Unachagua wewe mwenyewe "uzike au usafirishe".
Mambo ya hijab ni dini au sio dini, mambo hijab zimeumbwa na nani, hayo tuyaache maana sio sehemu ya wasilisho langu na wala sioni umuhimu wa kuyajadili hapa.