Kuvaa Hijab ni dini au udhaifu wa wanaume?

Kuvaa Hijab ni dini au udhaifu wa wanaume?

Nimezungumzia now hatuvai namna zilivoamrishwa zivaliwe manakshi nakshi ni mengi kias kutamanisha ndo lengolangu lilikuwa hapo
Anaetakiwa kurekebishwa na kuacha tamaa ni mwanaume, na sio kumpa mwanamke mzigo wa manguo, binadamu anauwezo wa ku control hisia zake
Kama vile tu baba hawezi tamani mtoto wake wa kike ,ila anae tamani ni mgonjwa wa akili ndo hivyo wanaotamani hovyo wanawake kisa nywele ni wagonjwa wa akili (sex maniac)
 
Binadamu wote wake kwa waume wanazaliwa wakiwa uchi kabisa, kuvaa nguo ipi na ivaliwe wapi na nani kwa sababu gani ni utashi tu wa wanajamii wenyewe. Bahati mbaya au nzuri Mwenyezi kuna maeneo na viungo vya mwili ambavyo alishavifunika yeye mwenyewe kwa sababu zake kwa kutumia nywele ndefu na nywele fupi kutokana na umuhimu wake na sababu zake. Mfano, Mungu amekifunika kichwa cha kila mtu kwa nywele ndefu bila kujali jinsia yake, kabila wala dini yake, Mungu akakifunika kinena cha kila mtu aliyebalehe kwa nywele ndefu tunazoziita mav*zi. Hakuishia hapo akakifunika kidevu na kifua cha mwanaume kwa nywele ndefu pia kwa sababu zake mungu mwenyewe. Hakuishia hapo akaifunika ngozi ya mwili ya watu wote kwa nywele fupi tunazoziita malaika kwa sababu zake pia, akatupa pia nyusi, kope na nyweli puani bila ya kumuomba. Hivyo kila nywele ilikuwa na sababu yake na ilitosha kabisa kuifanya kazi iliyokusudiwa kufunikwa na kukingwa. Hii ni kuonyesha kuwa Mungu anayajuwa mahitaji yetu yooote.

Ni nani ambae hataki kumuona mwanamke ambae asiyefunika nywele zake? Je, ni mwanamke mwenyewe kwa sababu zipi? Je, ni mwanaume kwa sababu zipi na je, ni Mungu aliyetufanya tuzaliwa uchi lakini akatufunika kwa nywele kwa sababu zipi?

Utafiti wangu kwenye hili ni kwamba, sio Mungu anaetaka wanawake wavae Hijab bali ni wanaume tu kwa sababu ya wivu na kujifanya kuwa wao ni dhaifu kwa kutazama tu nywele, matiti, mapaja na vitovu vya wanawake wakasahau kuwa Mungu angetaka asingeshindwa kuwafanya wanawake wazaliwe wakiwa na hijab tayari. Tuache ujinga wa kuwadhulumu wanawake kwa kujificha kwenye kichaka cha dini. Nini sio Hijab wala nywele za mtu.

Ona haya mauaji na maandamano ya kijinga kabisa, eti msichana hakuvaa hijab.

ni 1wakorinto 11:24
 
Muelekeza mtunzi wa hijab ni Umar

Nukuu ya waislamu wanatujuza aya ya hijab ilipotokea
Umar said:.... , both righteous and evil doers enter your wives, so why don't you tell them to observe the hijab? Then the verse of hijab was revealed. ...... and it was revealed like that. Musnad Ahmad 157
Hivi unajua maana ya hijab?
 
Hivi unajua maana ya hijab?
Ndio hii Umar alileta idea yake , Muhammad akaweka verse

Soma
Umar said:.... , both righteous and evil doers enter your wives, so why don't you tell them to observe the hijab? Then the verse of hijab was revealed. ...... and it was revealed like that. Musnad Ahmad 157
 
Ulichoandika hakina maana ni uchafu mtupu!! Haya usivae nguo uone ,Hayo mambo ni katika kuslow down mahaswi kutokana na Tamaa za kibadamu kinaweza kuchochea uzinifu .

Hakuna mahali umelazimishwa ila kama unataka kuifuata uislamu basi tii Sheria hyo kwa mwanamke kwa nn unapenda kufuatilia vitu havikuhusu ,nenda kaangalie masisters wanavaaje kanisani kama hujui hekima ya wao kuvaa ile hijabu ni ishu za kujistiri angalia na mapadre ulishawai kuona wapo padre kavaa kipensi, nenda hata ofisini uvae kipensi uone .
Unanikumbusha, Vijana wa kariakoo na mbezi, wakipita wadada walivaa kimini cha kihasara hasara, wanamzonga wengine wakiingiza mikono yao kule, mpaka wanamchania hicho, kisketi mpaka anabaki Uchi, ila uzuri wanawake wanasitliana, hujitokeza mama mwema, na kumpa kitenge chake.

Ila siku hizi, wadada wameacha kuvaa nguo hizo hayo maeneo.
 
Kwa hiyo tukubaliane kwamba shida sio Mungu ila ni sisi tu ndo tuna shida kuamulia watu wamfuate Mungu kwa nguvu.
Kila mtu kaumbwa na Mungu na kuzaliwa peke yake, hivyo kazi ya kumuamini, kumshukuru na kumuabudu ni jambo na kazi binafsi pia. Kusimangana, kupigana na kushurutishana juu ya Mungu sio sawa na sio jukumu la mtu mwingine. Ndio maana Mungu akasema atamheremu na kumuokoa yule amtakae. Na hajasema huyo atakaeokolewa atakuwa ana sifa gani, kavaaje au anaabuduje,
 
Kuvaa hijabu ni amri ya Mwenyezi Mungu kwa wanawake wote wa Kiislamu. Na hii inawasidia wenyewe wasiudhiwe hasa kutokana na maungo yao kuwa ya kuvutia kwa hivyo wakijisitiri hawapati usumbufu.
Haya mavazi ndio hayo hayo aliyoyavaa Mama yake Issa/Yesu (Yaani Mariamu) na ndivyo wanavyo vyaa masista wa katoliki.

QURAN 33: 59
" Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo kutafanya watambulikane (kuwa ni wenye kujiheshimu) wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu."
Kwa hiyo huyo mwenyezimungu aliwaambia Muwalazimishe wavae hata wasipotaka kuvaa?
 
We mtoa mada kama unaamini Mungu ndie ameumba wanaadamu basi lazma ujue kuna sheria zake zinazopatikana katika misingi ya dini. Kasome dini ya uislamu ufahamu vzr na ukristo ufahamu vzr ndio ulete tena mada. Maana hapo umebwabwaja pumba tupu.
Hizo sheria zake aliwaambia nyie wala mlenda mulazimishe watu wazifuate?
 
According to hadith za kiislam...Umar (Rafiki ake mtume/Swahaba)ndio alitaka wanawake wafunike uso.
Alimfata Muhamad na kumsihi apitishe sheria hii ila muhamad akawa kama haitaki vile.

Umar siku moja akaenda mahali wanakojisaidia wanawake (Enzi hizo hamna vyoo, kulikuwa kuna maeneo tu huko jangwani ya kwenda kujisaidia)
Akapambana mpaka amuone mke wake Mtume akijisaidia...Alipomuona akamuambia "Wewe Aisha nimekujua"

Akaenda kumsimulia hilo tukio Mtume na kumwambia kuwa angejifunika uso, Umar asingemtambua.

Basi Ewala...Mungu fundi, Usiku huo huo Malaika Jibril akashuka na Aya za kuwalazimisha wanawake wafiche sura zao.
Allahu Akbar.
Kwahiyo wanawake wavae hijab na nicarb kwasababu TU ya kichaa aliyekwenda kuwachungulia wanawake wanaojisaidia porini, siku hizi mtu kama huyo SI anafungwa miaka 30? Siku hizi haKuna vichaka vya kujisaidia kila mtu anakwenda chooni kwenye marumaru, vioo, AC, maji na jacus, kama sababu ilikuwa hiyo je hivi sasa Kuna haja ya hijab tena? Lakini Aya si unateremshiwa ukiwa usingizini ukiwa peke yako na wewe ndiye unaesema nimeoteshwa, hakuna shahidi.
 
Ndio hii Umar alileta idea yake , Muhammad akaweka verse

Soma
Umar said:.... , both righteous and evil doers enter your wives, so why don't you tell them to observe the hijab? Then the verse of hijab was revealed. ...... and it was revealed like that. Musnad Ahmad 157
Hujajibu swali, nahitaji jibu tu
 
Mwanaume ndio mwenye Dunia yake na mwanamke alitoka ubavuni mwa mwanaume kwa hiyo lazima apangiwe masharti jinsi ya kuishi katika utawala wa mwanaume asiishi jinsi anavyotaka yeye
Wanaume wote mmetoka kwenye tupu za wanawake, mama zenu, lazima muwe na staha na wanawake, lazima muwaseme vizuri. Ulikuwa tumboni kwa mwanamke halafu ghafla unasema mwanaume ndiye mwenye dunia yake, tuache ulofa.
 
Sikiliza wewe na usiwe kama umekumbwa na uhayawani, kila mahali kuna taratibu zake kwa mujibu wa imani zilizopo huko. Hawajawahi kuingilia huo wako unaoishi nao, basi heshimu ya wengine.

Iran nzima inajulikana inaongozwa kwa sheria za kiislamu kali tena chini ya dhehebu la shia, mavazi na taratibu zingine zinafuatwa maana ni sheria ya nchi. Hii hata ukienda mgeni unatakiwa uitimize sawasawa, kwani wao wakija huku ulipo wewe wanakutana na sheria zake na wanazifuata.

Chuki ya dini kubwa mnaileta nyinyi, waislamu hawana habari na nyinyi na wala hawagusii kuhusu sheria za kwenu. Ndiyo kama hao Iran wanafanya yao, cha ajabu wewe upo mbali nao unaanza kusambaza maneno ys chuki.

Waislamu wanafundishwa kuheshimu imani za wengine na hata enzi za Mtume mwenyewe alishaishi na wakristo na wayahudi na hakuwahi kuingilia imani zao. Huku kuwachokonoa na kuleta chuki zako, wakija kujibu au kufanya jambo kwa kuchukizwa useme ni wabaya.

Wewe shika dini yako achana na za watu, kama kuna makosa yanatokea kwao hata kwako yanatokea pia. Kabla ya kumnyooshea mtu kidole, hakikisha mkono wako ni msafi.
Sasa taratibu za mahali zinatoka kwa Mungu? Acha ulofa.
 
Wanaume wote mmetoka kwenye tupu za wanawake, mama zenu, lazima muwe na staha na wanawake, lazima muwaseme vizuri. Ulikuwa tumboni kwa mwanamke halafu ghafla unasema mwanaume ndiye mwenye dunia yake, tuache ulofa.
Yaleyale ya Kuku na Yai, abgalia chimbuko la mwanadamu
 
Back
Top Bottom