Hapa ndipo nilipoona ujinga wako Kavulata. Inaonesha hujui chochote kuhusu Uislam. Ungekuwa unafahamu kuhusu Uislam usingeandika hivi. Ungekuwa unajua kuwa katika Uislam mbora ni yule MchaMungu usingeandika hivyo.
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَـٰكُم مِّن ذَكَرٍۢ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَـٰكُمْ شُعُوبًۭا وَقَبَآئِلَ لِتَعَارَفُوٓا۟ ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ ٱللَّهِ أَتْقَىٰكُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌۭ ١٣
O humanity! Indeed, We created you from a male and a female, and made you into peoples and tribes so that you may ˹get to˺ know one another. Surely the most noble of you in the sight of Allah is the most righteous among you. Allah is truly All-Knowing, All-Aware.1 (Qur'an 49:13)
Ungekuwa unajua kuwa katika Uislam hakuna ubora wa Mwarabu juu ya asiyekuwa Mwarabu, au Asiye Muarabu juu ya Muarabu, wala hakuna ubora wa Mweupe juu ya Mweusi wala Mweusi juu ya Mweupe isipokuwa UchaMungu, usingeandika hivyo.
Abu Nadrah reported: The Messenger of Allah, peace and blessings be upon him, said:
Ungekuwa unajua kuwa "Miji haitakasi watu", kuwa Abu Jahl, Utba bin Rabi'ah, Walid bin Mughirah, Umayyah ibn Khalaf na wenzao walikuwa Maquraish wakiishi karibu na Ka'abah lakini walimkataa Mtume na kufa katika Ushirikina hivyo kuishi kwao Makkah hakutowafaa kitu, ungekuwa unajua hilo usingeandika hivi. Ungekuwa unajua kuwa Abu Lahab, baba yake mdogo Mtume (Swalla Allahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam), ataingia motoni tena alibashiriwa Moto katika Qur'an, usingeandika hivyo. Ungekuwa umesoma na kuifahamu kisha kuitafakari Sura hii ya Qur'an, nadhani wala usingeandika hayo;
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0
1. Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia.
1
2. Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma.
2
3. Atauingia Moto wenye mwako.
3
4. Na mkewe, mchukuzi wa kuni,
4
5. Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa.
5
Ungekuwa umesoma Hadith hii ifuatayo, Wala usingeandika maneno yako hayo.
عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَجُلا قَالَ : يَا رَسُولَ اللَّهِ ، أَيْنَ أَبِي ؟ قَالَ: ((فِي النَّارِ)) فَلَمَّا قَفَّى دَعَاهُ ، فَقَالَ: ((إِنَّ أَبِي وَأَبَاكَ فِي النَّار)) مسلم
Kutoka Anas (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Ewe Mjumbe wa Allaah, baba yangu yuko wapi? Akasema: ((Motoni)). Alipogeuka akamwita kisha akamwambia: ((Baba yangu na baba yako wako motoni)) [Muslim]
Ushawahi kumsoma Bilal ibn Rabah (Radhiya Allahu 'Anhu)?
Fahamu, kuwa ubora wa watu utakuja kwa kule kushikamana na dini hii ya Allah kama alivyoifundisha Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) juu ya ufahamu wa Sahaba zake (Radhiya Allahu 'Anhum) ambao walimuamini Mtume kwanza kuliko watu wengine waliofuatia, wakachukua mafundisho yake moja kwa moja na wao ndio wakaisambaza dini na wakawazidi wengine katika Ummah huu kwa UchaMungu wao na kule kumnusuru kwao Mtume.
Hivyo huyo Akhi uliyemnukuu huenda akawa bora zaidi kuliko hao mabinti wa Iran hata kama , kama unavyodai, wanakaribiana zaidi kinasaba na Mtume. Si ajabu ukakuta wengi wao hapo ni Mashia, wajinga wasiofahamu dini, Masekula ambao hawataki dini kabisa (wakiwemo Atheists) na wengine huenda wakawa ni Majusi (Zoroastrians) au Waislam maasi, jambo ambalo haliwafanyi kuwa bora.
Na Allah anajua zaidi.