Nawaza moyoni kama mtoa mada alivoyosema. au naongeza umuhimu wa mwanamke kuvaa nguo za heshima, lakini kuvaa hijabu mpaka kufunika miguu na uso, naona kama ni uonezi mkuu sana kwa wanawake.
Kwa upande wangu nafikiri mwanzilishi wa dini inawezekana kuwa alichangia kwa kuwa yeye pia alikuwa na bidii sana katika uhusiano na wanawake (alioa wanawake 9 na vile vile alikuwa na masuria kibao). Msifikiri na kashifu kiongozi wa dini hii, la hasha, bali naeleza ukweli aliokuwa nao, nafikiri Ili kupunguza hilo (kwa mawazo yake) ni kuwafanya wanawake wajifunike mwilini mzima, ili wanaume wasitamani wanawake (sijui na yeye pia?) Kumbe tatizo sio tu wanawake kujifunika bali moyo ukiharibika hauna dawa mpaka Mungu pale anavyoweza kuingilia kati. Nchi zenye sheria kali kuhusu ngono zinapunguza tabia hii kwa namna fulani, lakini nadhani sio hijabu iliyopunguza, kilichopunguza ni sheria kali. Kama si hivyo walegeze sheria lakini waruhusu hijabu kama tabia ya uasherati haitapanda. Ubaya wake sheria hizi kali zimelenga upande mmoja tu wa wanawake wala sio wanaume.
Kwa kutojua mtu anafanya biashara ya nguo anajifunika uso, mara nyingine najiuliza huyu amekuja kufanya biashara ya nguo, karanga au? Biashara inaendana na uchangamfu wa mtu, uso wake unapooneka. Lakini wengine kwa ujinga wao kuelewa Qur'ani ni kujifunika uso ndio kunampeleka mbinguni.
Dini kwa sehemu kubwa inawakandamiza sana wanawake, ingawa wanawake hawajui hilo. Kwa dini ya Kiislamu hakuna mbingu ya wanawake, ni ya wanaume tu, ambao watakuwa na mabikira huko. Jamani usipande jazba nimetoa yale niliyosoma na kufikiri kama mtu mwenye akili za mtazamo wangu, wala usifikiri mimi wa dini fulani inayopinga Uislamu. Naandika juu ya uonezi wa wanawake kidini.