Kuvamiwa kwa Mbowe: CHADEMA yacharuka, Mnyika amvaa IGP amuonya kuhusu uongo unaotengenezwa na Jeshi la Polisi

Kuvamiwa kwa Mbowe: CHADEMA yacharuka, Mnyika amvaa IGP amuonya kuhusu uongo unaotengenezwa na Jeshi la Polisi

View attachment 1488940

Katibu Mkuu wa Chadema Mh John Mnyika leo ametoa kauli kali ambayo ndio kauli halali ya Chama chake kuhusiana na Propaganda za kishamba zinazosambazwa na Jeshi la polisi zikiongozwa na IGP Sirro mwenyewe kuhusiana na shambulizi alilofanyiwa Mh Mbowe na Watu waliotumwa kumdhuru .

Hakuna ushahidi wowote kwamba Mbowe alilewa kama Sirro na waliomtuma wanavyoropoka mitaani , tarehe 8 na 9 June Mh Mbowe hakuwahi kukanyaga Royal Village Hotel kama watunga uongo wanavyodai , na kama kuna anayebisha alete ushahidi wa Mh Mbowe kuwepo eneo hilo kwa tarehe zilizotajwa kama waongo wanavyodai , Hakuna mtu yeyote kati ya wapiga kelele akiwemo Ndugai au Sirro wanaoweza kuthibitisha jambo hilo , wala hakuna Daktari hata mmoja katika waliomtibu Mbowe aliyethibitisha hilo , bali uongo huu unaosimamiwa na IGP kwa kulishwa maneno na Ndugai umeletwa makusudi kwa lengo la kuzima uchunguzi wa kuvamiwa kishamba kwa Mh Mbowe , kama Sirro ana ushahidi auweke hadharani .

Natoa wito kwa Chadema kumchukulia hatua IGP Sirro kwa kujiingiza kwenye siasa tena kwa kutumia Mguu wa kushoto , ikiwa Sirro anahitaji uongozi wa kisiasa basi amuombe Mwenyekiti wake wa ccm amruhusu ili tupambane naye majukwaani , Asijiingize bila taarifa ili asitumbuliwe .
Sirro ni Zero Brain kwa Sasa!!
 
Aliyempiga mbowe ni lijuakali na Msukuma na mtu mmoja Asiyejulikana, walivaa mask asiwatambue haraka hata shambulio walifanya kwa haraka sana huku wakiogopa kuonekana na kukimbia wakatokomea mle mle kwenye nyumba zao. Wataumbuka tu kwani chadema wanaenda kusoma Albadiri kwa kila mwana CCM anayewahujumu kuwaonea.
Msukuma ni mshamba aliyechangamka
 
Hayo ni matumizi mabaya ya ofisi kwa nini Mbowe asemewe kwenye hilo yeye hana mdomo? Yeye na hawara yake Joyce mukya ndio wanatakiwa waseme kilichotokea.Chadrma hakikuweko eneo la tukio huo usiku wa manane.Mnyika acha kuongelea Walevi waache wenyewe waongee
 
Ni wajinga wachache tu ndio wanaoamini tena wapo mitandaoni Kama humu jf
Wewe upo kwenye karatasi au mitandao?
Mbowe mlimshambulia ili hamna aja ya kupinga...Tumewaona wengi mkisema wapinzani wavunjwe miguu
 

Attachments

  • VID-20200610-WA0074.mp4
    3.4 MB
Hata kama alilewa nyumba anayoishi ina cctv ambazo zipo controled na serikali kwanini wasilete ushahidi wa video siku wakina siro watakapokuwa nje ya madaraka tutawashughulikia vibaya sana kwa upumbavu wanaofanya hawana kibali cha Mungu .
Watu kama hao ni kuingia kwenye page zao za kijamii wanapewa maneno yao pale hadi akili inawakaa sawa
 
Mbowe alilewa waache kumfichia aibu
Kila mtu anajua Mbowe ni mlevi wa kutupwa
Mwambieni huyo mseminari Mnyika aache kubwabwaja
Mjifunze kuweka akiba ya maneno. Hivi mnajua kwa nini hadi sasa Mbowe amekuwa kimya juu ya huu uzushi wenu? Ngoma ikivuma sana ujue inakaribia kupasuka. Aibu kubwa inawasubiri sijui mtaweka wapi nyuso zenu. Wahenga waliosema kukaa kimya ni jibu mujarabu kwa mpumbavu hawajakosea. Upumbavu wenu utawagharimu sana.
 
Ule ndio ushahidi waliofanyia uchunguzi! Sasa Mbowe kwanini asitokee mwenyewe aseme kilichotokea badala ya kuwatuma kina Mnyika?
Na kwanini amekaa kimya muda wote huo hadi Myika nakuja na shutuma dhidi ya IGP dadala ya kueleza jinsi Mbowe alivyovamiwa na wasiojulikana!
 
Inanikumbusha enzi za Omari Mahita alionyesha visu vyenye mipini ya rangi zinazofanana na bendera ya cuf, akiaminisha watanzania eti vimeletwa kwa ajili ya kuanzishia fujo kipindi cha kampeni. Lile contena hata leo halijaonyeshwa, hivi kweli karne ya 21 bado watz wanalishwa matango pori !!!!!!. Baada ya kustaafu akaenda kuomba ubunge na aliachwa mapema tu. Ma IGP muogopeni muumba
Ingawa nilikuwa mdogo ila nakumbuka huyu IGP alikuwa katili sijapata kuona
 
Back
Top Bottom