Kuvamiwa kwa Mbowe: CHADEMA yacharuka, Mnyika amvaa IGP amuonya kuhusu uongo unaotengenezwa na Jeshi la Polisi

Kuvamiwa kwa Mbowe: CHADEMA yacharuka, Mnyika amvaa IGP amuonya kuhusu uongo unaotengenezwa na Jeshi la Polisi

Na kwanini amekaa kimya muda wote huo hadi Myika nakuja na shutuma dhidi ya IGP dadala ya kueleza jinsi Mbowe alivyovamiwa na wasiojulikana!
Ngoja CCM na wapambe wao wamalize uzushi wao wooote, ila siku zote anayecheka mwisho ndiye hucheka saaaana na kwa sauti ya juuuu hadi iache mwangwi.
 
Yaani maisha haya, Mnyika anamcheka siro eti anatumwa, sas sijue yeye anajituma au antumwa na mbowe mtu alilewa ,yeye anakazana kurefusha kamdomo kake kumshutumu siro utadhani siro.ndiye aliyempa mbowe konyagi. amuchie mbowe aseme baada ya kupiga konyagi aliona nini? wengine huwa wanaona ndugu zao waliotangulia
 
Mnyika aliahid kutoa taarifa rasmi ya chama juu ya kinachoitwa kushambuliwa kwa mh. Mwenyekiti Mbowe. Na katika taarifa yake ya awali, Katibu mkuu alidai Mbowe hakua peke yake. Sasa yapata mwezi, hiyo taarifa haipo. Sasa Nini Wanachadema, hasa wa humu jukwaani mnataka sisi watembea kote(swing voters) tuamini Nini? Leteni ripoti yenu, tuchague wa kumuamini.
 
Mnyika aliahid kutoa taarifa rasmi ya chama juu ya kinachoitwa kushambuliwa kwa mh. Mwenyekiti Mbowe. Na katika taarifa yake ya awali, Katibu mkuu alidai Mbowe hakua peke yake. Sasa yapata mwezi, hiyo taarifa haipo. Sasa Nini Wanachadema, hasa wa humu jukwaani mnataka sisi watembea kote(swing voters) tuamini Nini? Leteni ripoti yenu, tuchague wa kumuamini.
Ripoti kamili itatolewa kwa wakati uliopangwa na siyo kwa shinikizo. Ngoja wazushi, wambea,wadaku,waongo,wazandiki na wapiga ramli wamalize kwanza matamanio yao.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakina imani na uchunguzi unaofanywa na jeshi la polisi kuhusiana na tukio la Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

Kimedai shambulizi la Mbowe linashabihiana na alilofanyiwa Makamu Mwenyekiti Bara, Tundu Lissu, na kwamba tofauti ni kiwango cha madhara.

Hivi karibuni Jeshi la Polisi kupitia kwa msemaji wake, David Misime, lilitoa ripoti inayoonyesha kuwa Mbowe hakushambuliwa kama inavyodaiwa bali alianguka kutokana na kulewa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, alisema chama kinaendelea kutafakari hatua za ziada za kuchukua.

Aliutaka umma upuuze njama alizodai zinatumika kuhalalisha kauli za uongo zinazotolewa katika kipindi hiki cha uchaguzi ili kuwachafua viongozi wa chama hicho na chama kwa ujumla.

“Tulidhani polisi itaendesha uchunguzi huu kitaalamu, kauli ya IGP (Mkuu wa Polisi, Simon Sirro) inaashiria bado jeshi linajihusisha katika propaganda hasi.

“Tuna vyanzo mbalimbali na mimi nimepata bahati ya kuzungumza na ambaye alikuwepo kwenye eneo la tukio, waliokwenda hospitali, maelezo ya wote hao hayaonyeshi popote kwamba mwenyekiti Mbowe alilewa chakari, nani aliyethibitisha, ajitokeze hadharani.

“Kipimo cha ulevi ni suala la kitabibu, ajitokeze daktari aiyempokea Mbowe na kumpima na polisi itoe ushahidi wa ‘CCTV camera’ kuthibitisha madai kwamba alianguka akiwa amelewa,” alisema Mnyika.

Alisema baada ya tukio hilo kutokea walifanya utaratibu wa kumleta Mbowe Dar es Salaam ili afanyiwe uchunguzi wa kitabibu kwenye maeneo mbalimbali ya mwili yakiwemo unyayo wa mguu na mguu wote kwa upana wake.

“Wakachukua X- ray ya sehemu ya kipande cha mguu ambacho hakikuvunjika wakaacha X- ray ambayo inaonyesha sehemu aliyopata madhara yaliyosababisha hadi afanyiwe operesheni ili kuhalalisha uongo kwamba hakuumia.

“Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani ana walinzi wa Serikali lakini tarehe 9 wameonekana nyumbani kwa Mbowe wakifanya mahojiano, je wamepata maelezo kwanini waliondolewa, na ikawaje baada ya kushambuliwa ndiyo wakarejesheshwa siku ya tarehe 9? Jeshi la polisi litoe maelezo,” alisema.

KUREJEA LISSU

Kuhusu suala la kurejea kwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu, alilitaka jeshi la polisi liwahakikishie ulinzi wake pindi atakaporejea.

Kwa mujibu wa Mnyika, kwa nyakati kadhaa chama hicho kiliamuandikia barua IGP likimuomba ulinzi kwa ajili ya Lissu pindi atakaporejea lakini hazijajibiwa.

“Licha ya kukuandikia ujumbe Januari 7 mwaka huu bado hujatupatia majibu, kimya chako hiki hakipendezi, jaribio la mauaji dhidi ya Lissu lilizua maswali mengi sana ambayo hadi leo hayajapatiwa majibu…anaomba kupata ulinzi wakati atakaporejea nyumbani iweje leo linapata kigugumizi kutoa jibu la ombi hilo”? alihoji Mnyika.
 
Polisi wanaletewa script wasome hawana cha uchunguzi wala nini, eti alikuwa royal village akilewa, kumbe siku hiyo hata hakukanyaga hilo eneo, watu wa hovyo sana hawa.
 
Hapo Chadema nao wanaonesha wapo tayari ushahidi wa CCTV Camera utumike, Sirro anatakiwa kutuletea ushahidi wa CCTV Camera waache kelele, hizo kelele zao zitapita kama upepo, mwisho wa siku ukweli wote utakuwa wazi.

Ile mipasho yote ya kule bungeni na wote walioizungumza kuhusu hilo tukio wanaenda kuumbuka, umma wa watanzania ujue aina ya Spika tuliyenaye na baadhi ya wabunge wa chama chake walivyo na akili fupi.
 
Kwanini hili suala asije Mbowe mwenyewe aeleze kilichotokea?

Kwanini kina Mnyika ndio wapo mstari wa mbele kumtetea Mbowe badala ya yeye mwenyewe kuja kueleza umma?

Chadema acheni uhuni
 
Ripoti kamili itatolewa kwa wakati uliopangwa na siyo kwa shinikizo. Ngoja wazushi, wambea,wadaku,waongo,wazandiki na wapiga ramli wamalize kwanza matamanio yao.
- KumbukiziMTAFUTANO.jpg
 
Kwanini hili suala asije Mbowe mwenyewe aeleze kilichotokea?

Kwanini kina Mnyika ndio wapo mstari wa mbele kumtetea Mbowe badala ya yeye mwenyewe kuja kueleza umma?

Chadema acheni uhuni
Ni wapiga zumari Wake Mr faru john
 
Back
Top Bottom