Khaaaaa
Pole mkuu, Yaaani ukishaona Mtu anauza bidhaa hasa electronics Anadai ana Duka na ni nje ya Dar halafu haanzi kwa kutaja exact location Anajinadi kusema popote tunakutumia, Anza kutumia akili yako vizurii....
Wanatumia trick ya nje ya dar hasa zanzibar maana wanajua Ni ngumu kuifuata,
Na anajua wateja wengi wapo Dar, au Ana ndugu Dar, hivyo akikuambia yupo Dar ni simple tuu utahitaji kumuona au kutuma mtu.
Huyo ni tapeli, hauzi simu na Asilimia kubwa yupo Dar...
Ila vitu vingine ni kujiongeza tuu, sasa kweli mtu anakuambia Anauza simu, yupo Manyara, Tabora, Iringa(kupatana wamejaa hawa) Ukiangalia Mazingira ni bonge ya Duka, Bei nayo hata ya China haioni ndani....
Khaaa sasa kweli kweli kwelii mtanzania mwenzangu Duka la Simu bei chee tena iphones na Macbook za maana likose kote kwa kukaa likae Mara na sumbawanga?????
Halafu pia hii habari ya mjini ya sasa ya free delivery ndio inawaumiza watu..
Ni nzuri ila kiafrica wengi wana mlengo wao mwingine..
Na binafsi hata kama hamna utapeli, sio mpenzi wa biashara za free delivery hasa zile ambazo zinahitaji ukaguzi, bora hizi za kimataifa za kuagiza nje, ila bongo uaminifu bado sana
Raha ya biashara uone bidhaa, ukague, ulidhike, ulipe uchukue..
Sio ulipe uletewe, ulazimike kuchukua,
Ukienda dukani waweza ukutane na option nyingi quality tofauti tofauti uamue mwenyewe ya kuchukua.