Kuwa Makini: Kuna Matapeli huko Instagram wanaodai kuuza iPhone na Smart TV etc wakidai wapo Pemba au Zanzibar

Nenda police na kama una mtu unamjua police atakusaidia vizuri...kama aliweka tangazo lame na ulichati nae wanampata fasta tu alipo hata kama line kavunjavunja
 
Ogopa sana matapeli nyumba hii haiuzwi😎😎
 
Watu mna pesa za kucheza nenda Instagram uko uko ukalielie
 
Kwa hali hii basi Wasukuma tuendelee kuitwa washamba tuuu: maana hatukubaligi kabisa biashara ya nadharia. Ngosha lazima afike dukani alinganishe ubora sana ndo alipie kitu. Sasa hii ya skuizi ya β€œmikoani tunatuma” itawapiga sana nyie wajanja wa mjini.
 
Hapo ndipo Mwanaume wa Dar anapowazidi wa mikoani ( BRAIN 🧠)
 
Kwanza ni uzembe kuibiwa hivyo c unamwambia atakae nipo mzigo Ndio nitakae mpa pesa
 
Ulikua ushajiandaa mwenyewe kuja kupandisha nyuzi za kuponda tecno zetuu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna dada alikua anauza laptop,nikaipenda tukaelewana bei nikaridhia,nikamwambia sasa tuonane nikague,akaniuliza kwani we uko wapi,nikamwambia niko Zenj,akasema yeye yuko dar nitume pesa ananitumia boti ya saa sita,nikagoma nikamwambia nitatuma ndugu yangu kesho yake waonane aikague then atawalipa watamkabidhi,akakubali kesho yake namtafuta nimwonganishe na ndugu yangu,naona porojo zimekua nyingi,mara yuko Tanga nimtumie pesa,nikamwambia nina ndugu Tanga nikuunganishe nae akague mkabidhiane,nikashangaa nimekula BLoCk matata!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…