Kuwa Makini: Kuna Matapeli huko Instagram wanaodai kuuza iPhone na Smart TV etc wakidai wapo Pemba au Zanzibar

Guys tubadilishe mitazamo,huyu ni mwana JF mwenzetu,na hapa ni sehemu ya kupata maarifa,ushauri hata msaada pale inapobidi....

Tumsaidie mwenzetu ili kukomesha hii tabia maana huwezi jua,Leo huyu katapeliwa Kwa njia hii kesho wewe Kwa njia nyingine au ndugu yako..
 
Mkuu cheki hii kitu mfanyabiashara gani anazui comment section kwenye bidhaa yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaa kweli mkuu
 
Tobaaa....
 
Hapo unakuta ulijichanga takribani mwaka mzima ili utimize ndoto, kisha zinakwapuliwa na wajuba dakika sifuri... karibu mjini. [emoji847]
 
Mkuu ndio wenyewe hao wamentapeli jaman[emoji22]
Hao jamaa wameweka location ya duka lao kuwa lipo Mwemberadu, mimi nipo huku Zanzibar na Mwemberadu kuna jamaa yangu anaishi hapo. Mwemberadu yote hakuna duka la simu, kuna maduka ya vifaa vya magari (motor vehicle used spare parts), maduka ya TV used na mpya pamoja na maduka ya vifaa vya nyumbani. Halafu kwenye account yao ya Instagram wamezuia comments jiulize kwanini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo umemaliza mkuu
 
Ulichokifanya ni sawa na ILE PESA WEKA KWENYE NAMBA HII...pole MKUU
 
Aisee pole sana .
mimi binafsi nikitaka kitu online naangalia kama wana duka, namtafuta muuzaji kwa namba mbili tofauti kama watu tofauti asiponipa majibu yanayofanana [emoji724] ni mwizi.
Unamcheki mtu kwamba umependa bidhaa anaanza kukwambia ukituma hela tunakufanyia deliver, ukimuuliza duka liko wapi anakwambia duka liko mbezi , ukimcheki kwa namba ingine anakwambia duka liko mbagala halafu mtu wa aina hii anaanza kwanza kukuuliza wewe uko wapi? ili akutajie sehemu ya mbali ushindwe kufata utume hela.

niliwahi kutuma hela one time kwa ajili ya Cake na nilituma pesa ambayo hata nikiipoteza isingeniuma lakini huyo dada katika watu sio waswahili ni yule nilipata kitu changu mda ule ule katika ubora ule ule.
 
Unatuabisha ma expert members mkuu.
Wewe huja tapeliwa, umegawa pesa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…