Kuwa mwanamke wa kisasa Tanzania ni changamoto sana katika mahusiano/ndoa

Kuwa mwanamke wa kisasa Tanzania ni changamoto sana katika mahusiano/ndoa

Hakuna kitu wanaume wanaogopa kama kushindwa na mwanamke katika maisha,kazi,pesa,elimu na kila kitu

No wonder kuna wanaume wanaamuq kuoa golikipa bora maisha yampige lakini awe na mnyonge wake nyumbani

Inferiority complex yasumbua wanaume
Na ndio sifa ya MWANAUME
 
Ukivaa nguo za kubana sio wife material

Ukitoka nyumbani unatakiwa kuomba ruhusa.

Ukichelewa kurudi nyumbani tatizo
Hayo ukiyafanya kama mwanamke unajiona upo sawa upstairs?

Kwanini uvae nguo za kubana unamuonesha nani maumbile yako?

Kwanini utoke nyumbani bila ruhusa ya mume? Usipoomba ruhusa huoni unaleta picha mbaya ya kwanini utoroke?

Kwanini uchelewe kurudi nyumbani kama mke wa mtu? Ukitaka kujirudia muda uutakao kuwa bachelor uone kama kuna mtu atahangaika na wewe kukuuliza tu hata wapi ulipo.
 
Yaani watu wanataka kuwa na version ile ile ya wanawake wz mwaka 47 ili hali kila kitu kinabadika. Kama ilivyo mabadiliko ya kiteknolojia, tabia nchi etc ndio hivyo binadamu hubadilika.

Inabidi kuishi kutokana na haayo mabadiliko na kutafuta jinsi ya kuendana nayo. Otherwise, tutapata tabu sana
Bibie sio Kila mtu ana fagilia huu usasa ambao wengi mnaukumbatia, Kuna wengine huo usasa hatutaki hata kuuskia na tumeridhika na Hawa conservative lifestyle na hivyo hata mwanamke tunayemtaka ni lazima awe tayari kuendana na flow zetu za ki old-fashion
 
Feminists ni wanawake au watu waliopaswa kupuuzwa tangu tuingine Karne ya 21.

Mwaka 2022 baada ya warusi kuvamia Ukraine na raisi Zelensiky kutangaza kwamba wanaume wote wa Ukraine ambao wako above 18 ni lazima waingie vitani kupambana na warusi na wakati huo akiwaruhusu wanawake wakimbie nchi tena akawaletea kabisa na trains za kuwasafirisha kwenda nchi jirani ya Poland.....

Nikategemea feminists around the globe wanalahani sana kile kitendo Cha Zelensiky kuwanyima wanawake wa Poland haki yao ya msingi ya kutetea taifa lao dhidi ya wavamizi wa kirusi, lakini wapi Kila mtu alikuwa kimyaaa na ndio kwanza wakaanza kuleta justifications za kipuuzi eti kwa sababu vita imeanzishwa na wanaume basi wanapaswa kupigana kwenye hiyo vita ni wanaume wa Ukraine.

Ndio maana Mimi nikiona mwanaume anashoboka na feminism huwa naghafilika sana
Kwenye mgawanyo wa rasilimali ndio nguvu ya feminism inapoonekana.

Sasa hii ni indirectly colonialism
 
Ukiwa Feminists ni shida,

Single mother ni shida,

Ukiomba pesa malalamiko

Ukimzidi mwanaume wako kipato kama yeye sio marioo tatizo.

Ukimzidi mwanaume elimu ni tatizo

Ukivaa nguo za kubana sio wife material

Ukitoka nyumbani unatakiwa kuomba ruhusa.

Ukichelewa kurudi nyumbani tatizo.
tukusaidie kupumua au
mwanamke ni mtawaliwa kama sisi tulivowatawaliwa na ccm, wakisema kitu lazima kufuata
kinyume chake utajuta
 
All women are modern, sawa mkuu???, ndio maana wanaish katika modern society.

Wewe wanawake unaomaanisha kimtaani tunawaita " wadada wa mjini"
Kama hii ndio tafsiri ya modern woman kwako basi una mawazo finyu sana/shallow minded.
Modern woman ni
Mwanamke free thinker/mwenye mawazo huru.
Mwanamke anayejali uhuru wake.
Mwanamke anayejua mahusiano, ndoa na kulea watoto sio kila kitu, na maisha ni zaidi ya hayo mambo.
Mwanamke asiyefugwa au kufanywa mwanafunzi wa shule ya msingi na mwanaume kwa kupangiwa mavazi ya kuvaa na kutakiwa kuomba ruhusa.
Mwanamke asiyekubali kuwa mke mwenza.
N.k
 
Kwanini uvae nguo za kubana unamuonesha nani maumbile yako?

Kwanini utoke nyumbani bila ruhusa ya mume? Usipoomba ruhusa huoni unaleta picha mbaya ya kwanini utoroke?

Kwanini uchelewe kurudi nyumbani kama mke wa mtu? Ukitaka kujirudia muda uutakao kuwa bachelor uone kama kuna mtu atahangaika na wewe kukuuliza tu hata wapi ulipo.
Mke/mwanamke wako sio mtoto wako.
 
Ukiwa Feminists ni shida,

Single mother ni shida,

Ukiomba pesa malalamiko

Ukimzidi mwanaume wako kipato kama yeye sio marioo tatizo.

Ukimzidi mwanaume elimu ni tatizo

Ukivaa nguo za kubana sio wife material

Ukitoka nyumbani unatakiwa kuomba ruhusa.

Ukichelewa kurudi nyumbani tatizo.
Wanawake mlioolewa na ma binti mnaotarajia kuolewa MSIFATE hili bandiko LITAWAPOTEZA😀

Sorry mtoa mada kama nitakukwaza ila sio sawa mke awe anajiondokea tu nyumbani bila kuaga na kuruhusiwa na mumewe na mwanake kuwa na tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani HAIFAI HAIKUBALIKI na HAIPENDEZI.
 
wameshakuambia hawataki ndoa wao ni upinde inabidi uwe upinde kama wao ndio utaendana nao, hivyo wanaume wasioshabikia mambo ya upinde hawawezi kuendana na hao maswaiba wako.

Ndoa ni janga kwenye jamii ya watu waupe na wausi Duniani sababu ndio jamii inayopenda kwenda na mabadiliko inapenda trend .
Jamii ya wahindi na waarabu imejitahidi na inaendelea kuilinda jamii yake kupokea hovyo trend za kidunia . Wahindi na waarabu wana rate ndogo sana za taraka kuliko wazungu na weusi Duniani.
Kaka umeongea jambo la msingi sana na kwenye uhalisia, hata hapa hapa bongo tu tuna jamii ya waarabu na wahindi, Hawa watu ni nadra sana hata Kukutana nao kwenye madawati sijui ya jinsia na vituo vya ustawi wa jamii kwa sababu jamii zao Bado ziko imara kutokana na kuendelea kuukumbatia utamaduni wao na hawana migogoro migogoro ya ndoa kama sisi weusi... Njoo kwetu Sasa yaani ni vurugu tupu
Kama hii ndio tafsiri ya modern woman kwako basi una mawazo finyu sana/shallow minded.
Modern woman ni
Mwanamke free thinker/mwenye mawazo huru.
Mwanamke anayejali uhuru wake.
Mwanamke anayejua mahusiano, ndoa na kulea watoto sio kila kitu, na maisha ni zaidi ya hayo mambo.
Mwanamke asiyefugwa au kufanywa mwanafunzi wa shule ya msingi na mwanaume kwa kupangiwa mavazi ya kuvaa na kutakiwa kuomba ruhusa.
Mwanamke asiyekubali kuwa mke mwenza.
N.k
Kwa kifupi tu tafsiri yako ya mwanamke wa kisiasa ni mwanamke wa ovyoo anayeendekeza uhuru usiokuwa na mipaka kama kunguru.

Kiufupi ni mwanamke asiyekuwa na thamani kwenye soko la mahusiano/ndoa na ndio maana hapo umetumia kauli ya "ndoa sio Kila kitu", haya endeleeni kufurahia huo uhuru jinga na hakuna atakayewaingilia.
 
Wanawake mlioolewa na ma binti mnaotarajia kuolewa MSIFATE hili bandiko LITAWAPOTEZA😀

Sorry mtoa mada kama nitakukwaza ila sio sawa mke awe anajiondokea tu nyumbani bila kuaga na kuruhusiwa na mumewe na mwanake kuwa na tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani HAIFAI HAIKUBALIKI na HAIPENDEZI.
Kwa mfano wewe ni daktari imetokea dharura unahitajika ghafla hospitalini au eneo la tuko halafu unamuomba ruhusa mume wako anakataa utafanyaje?

Mfano wewe ni waziri wa Ulinzi kuna masuala ya kiusalama yanakuhitaji ghafla halafu mume wako anakataa kukupa ruhusa utafanyaje?

Mfano mlikuwa mnavunja kikoba na mashosti zako jioni shughuli ikafana ikawa nzuri mkanywa na kucheza muziki muda ukaenda hadi mida ya saa nne usiku tatizo liko wapi??
 
Na nyie dada zangu shida huwa nini lakini na mahaba kwa wanaume wa hovyo?
Unakuta mwanamke mzuri ameganda kwa mtu mwenye mawazo ya caveman wa karne ya saba!
Hakuna kazi ngumu kama kudate mwanaume uliyemzidi kiwango cha elimu,wana inferiority complex...imagine unatoa tu ushauri wa kawaida kabisa let say" tusipande maua pembeni ya ukuta yanaleta sana mmbu ndani"utasikiia nyinyi wasomi ni wajuaji sana maua na mbu yana uhusiano gani?ukibisha sasa kanuna atasema unamdharau😅😅
 
Kwa mfano wewe ni daktari imetokea dharura unahitajika ghafla hospitalini au eneo la tuko halafu unamuomba ruhusa mume wako anakataa utafanyaje?

Mfano wewe ni waziri wa Ulinzi kuna masuala ya kiusalama yanakuhitaji ghafla halafu mume wako anakataa kukupa ruhusa utafanyaje?

Mfano mlikuwa mnavunja kikoba na mashosti zako jioni shughuli ikafana ikawa nzuri mkanywa na kucheza muziki muda ukaenda hadi mida ya saa nne usiku tatizo liko wapi??
sasa wewe kuwa waziri au daktari au member wa vicoba unashindwa kuwasiliana na mumeo akakuelewa ukiwa Rais wa nchi ,muigeni Mhe. Mama SSH yeye mbona ana uwezo wa kugawa muda wake Kuna muda tunamuona na mume wake,Kuna muda tunauona yupo na wajukuu kina muda anaingia jikoni anapika tena protokali hairuhusu Rais apike chakula kaonyesha juzi hapa live anapika sasa wewe uwazi na udaktari shida kuendana na mume wako ,mwanamke ukiukubali uumbaji wako wa kiunamke na kujua mipaka Yako na kujua mamlaka ya mwanaume na ukayakubali na mkatendeana Kwa trust,love and care mkisaidiana kusameahana mnapo koseana mkijijengea hivyo mwanamke hatapata shida na mwanaume ndio maana USA wapo wanaomshawishi mke wa Obama ,Michele Obama agombee Urais sababu wamemuona ni kwa jinsi gani alivyo bega kwa bega na mume wake,jamii yote ,mlezi.mzuri kwa watoto wake , mwanamke anayefanikiwa kwenye ndoa ni yule anayejua ku balance majukumu yake ya kazi/biashara na majukumu yake na wajibu wake kwa mume wake ukitoka nje ya hapo utaleta Kila aina ya visingizio.
 
Kwa mfano wewe ni daktari imetokea dharura unahitajika ghafla hospitalini au eneo la tuko halafu unamuomba ruhusa mume wako anakataa utafanyaje?

Mfano wewe ni waziri wa Ulinzi kuna masuala ya kiusalama yanakuhitaji ghafla halafu mume wako anakataa kukupa ruhusa utafanyaje?

Mfano mlikuwa mnavunja kikoba na mashosti zako jioni shughuli ikafana ikawa nzuri mkanywa na kucheza muziki muda ukaenda hadi mida ya saa nne usiku tatizo liko wapi??
Ukiwa daktari au waziri hiyo mbona mume tayari anakua anajua mkuu?!

Ila awe mama wa nyumbani au bread winner wa familia LAZIMA mke aombe ruhusa kwa mumewe huwezi tu kuwa ukijisikia unakurupuka kiguu na njia.

Hiyo ya vicoba inaweza isiwe shida na kama unaona dalili za kuchelewa si unapiga tu kumjulisha mapema.
Shida inakuja inapokua ni tabia.

Hii picha ya mke wa mtu kujiondokea bila ruhusa na kurudi late inagoma kichwani mwangu hasa nikifikiria wengi waloolewa ni kama vilema kila kitu akutafutie mwanaume hlf umdharau hivyo😀 ndo mana nawaelewa KATAA NDOA.
 
Yaani watu wanataka kuwa na version ile ile ya wanawake wz mwaka 47 ili hali kila kitu kinabadika. Kama ilivyo mabadiliko ya kiteknolojia, tabia nchi etc ndio hivyo binadamu hubadilika.

Inabidi kuishi kutokana na haayo mabadiliko na kutafuta jinsi ya kuendana nayo. Otherwise, tutapata tabu sana
Binadamu mabadiliko yake anayopitia ni ya ukubwa na udogo wa miili ila tabia ndo zile zile toka adam mpaka binadam wa mwisho hivi unavyoona wanawake walivyo ni matokeo ya wanaume,sisi ndo tunawaweka wanawake vile walivyo tukiamua wanaume wote tuwafanye mama wa nyumbani wote mtakuwa mama wa nyumbani hata huo uhuru wao wamepewa na wanaume magasho wanaojiona wao ni kama wanawake.Wanaume wenzangu ili kuifanya dunia iwe tulivu na salama popote ulipo hakikisha unambana mwanamke,kwani mwanamke hawezi kuutumia uhuru ukimwacha huru ataalibu kama unabisha kama unaishi na mke we mpe uhuru alafu subiri kitakacho tokea,kama dada zako wa kike fanya hivyo alafu subiri matokeo Dawa bana hawa kwa ustawi wa dunia na walimwengu.
 
Back
Top Bottom