Kuwa mwanamke wa kisasa Tanzania ni changamoto sana katika mahusiano/ndoa

Kuwa mwanamke wa kisasa Tanzania ni changamoto sana katika mahusiano/ndoa

Ukiwa Feminists ni shida,

Single mother ni shida,

Ukiomba pesa malalamiko

Ukimzidi mwanaume wako kipato kama yeye sio marioo tatizo.

Ukimzidi mwanaume elimu ni tatizo

Ukivaa nguo za kubana sio wife material

Ukitoka nyumbani unatakiwa kuomba ruhusa.

Ukichelewa kurudi nyumbani tatizo.
Wewe unatakaje kwa mfano? Unatamani kuwa mwanaume?
 
Binadamu mabadiliko yake anayopitia ni ya ukubwa na udogo wa miili ila tabia ndo zile zile toka adam mpaka binadam wa mwisho hivi unavyoona wanawake walivyo ni matokeo ya wanaume,sisi ndo tunawaweka wanawake vile walivyo tukiamua wanaume wote tuwafanye mama wa nyumbani wote mtakuwa mama wa nyumbani hata huo uhuru wao wamepewa na wanaume magasho wanaojiona wao ni kama wanawake.Wanaume wenzangu ili kuifanya dunia iwe tulivu na salama popote ulipo hakikisha unambana mwanamke,kwani mwanamke hawezi kuutumia uhuru ukimwacha huru ataalibu kama unabisha kama unaishi na mke we mpe uhuru alafu subiri kitakacho tokea,kama dada zako wa kike fanya hivyo alafu subiri matokeo Dawa bana hawa kwa ustawi wa dunia na walimwengu.
Una mawazo ya hovyo sana ya uharibifu, mke wako, watoto wako wa kike na wakwe zako wana hasara sana.
 
Feminism ni nini?

Mbona neno hili huwa hatulisikii kwenye mada zinazohusu vita?

Au wenzangu mnikumbushe labda pengine kuna siku Feminist waliwahi kudai haki ya wanawake kukaa front line huko Ukraine na Gaza ila mi tu sikusikia?

"Ladies first" ni kauli mbiu nayokutana nayo mara nyingi kwenye maswala ya kimaslahi na sio kwenye mambo magumu.
Kwa nini wanawake wakafe katika vita vilivyoanzishwa kwa ujinga wa wanaume wenye kushindanisha ego zao na kutunishiana misuli?? Hata wanaume wenye akili huwa wanajitahidi sana kuepusha, kuepuka au kuepukwa na vita.
 
Kweli aisee. Hii nimeshuhudia Babu alikuwa na wake wanne na mke wa tatu alimkuta na watoto wawili akaja nao kukaa Kwa babu na wale watoto walimheshimu Babu kama baba yao mpaka Leo japo ni marehemu
Marehemu ni nani sasa, hao watoto, au babu au baba yao?
 
Hakuna kitu wanaume wanaogopa kama kushindwa na mwanamke katika maisha,kazi,pesa,elimu na kila kitu

No wonder kuna wanaume wanaamuq kuoa golikipa bora maisha yampige lakini awe na mnyonge wake nyumbani

Inferiority complex yasumbua wanaum
Wanaogopa 'ulevi' unaotokana na hayo uliyoyataja.
 
Feminists ni wanawake au watu waliopaswa kupuuzwa tangu tuingine Karne ya 21.

Mwaka 2022 baada ya warusi kuvamia Ukraine na raisi Zelensiky kutangaza kwamba wanaume wote wa Ukraine ambao wako above 18 ni lazima waingie vitani kupambana na warusi na wakati huo akiwaruhusu wanawake wakimbie nchi tena akawaletea kabisa na trains za kuwasafirisha kwenda nchi jirani ya Poland.....

Nikategemea feminists around the globe wanalahani sana kile kitendo Cha Zelensiky kuwanyima wanawake wa Poland haki yao ya msingi ya kutetea taifa lao dhidi ya wavamizi wa kirusi, lakini wapi Kila mtu alikuwa kimyaaa na ndio kwanza wakaanza kuleta justifications za kipuuzi eti kwa sababu vita imeanzishwa na wanaume basi wanapaswa kupigana kwenye hiyo vita ni wanaume wa Ukraine.

Ndio maana Mimi nikiona mwanaume anashoboka na feminism huwa naghafilika sana
Wewe ukiwa mwanaume utakubali kwenda kupigana katika vita vilivyoanzishwa na wanawake?
Hata kama haukubali, huo ndio ukweli
Vita vikubwa vyote vya dunia vimeanzishwa na wanaume, genocides zote zimeanzishwa na kutekelezwa na wanaume, ni ujinga kudai wanawake wafe kwa sababu ya ujinga usiowahusu. Kama mnataka na wawo washiriki kikamilifu vitani na katika mauaji ya kimbari wapewe fursa kikamilifu za kuanzisha vita, mizozo ya kisiasa na mauaji ya kimbari.
 
Kwa jinsi ulivyo shusha mada yako kwa manung'uniko mkuu, naona unajilaumu kuwa Mwanamke!
Hapana, fikiria nje ya box na uwe na fikira pana, kuelewa hali ya kundi fulani la watu sio lazima uwe mmojawapo wa kundi hilo.
 
Huenda hapa ndipo tatizo kubwa zaidi lilipo. Inabidi wanawake kwenye ndoa wajitihadi sana ku-offer zaidi ya sex na kutunza watoto.
Vipi lakini ukiolewa ukiwa kama sio kilema unachangia mchango mzuri kuboresha hali ya familia??
Kabisa mkuu.
Kuacha mtu mmoja apambane peke yake(maisha yote😭) binafsi naona sio sawa.

ILA hata kama sio kilema na unasaidia ukishakubali tu kuolewa maana yake ni kuwa chini ya huyo aliyekuoa na ndio hapo vitu kama kuomba ruhusa ndio utoke vinakua sehemu ya maisha yako.Ukiona hiyo ni shida usiolewe sbb kwenye ndoa lazima mwanaume awe juu mwanamke chini.Ikiwa tofauti hamfiki!
 
Hajaja, mmekutana, na wakati mwingine hata ni wewe umemfuata yeye.
Akakubaliana na masharti yangu siyo? Kuepuka kuwa chini ya usimamizi wa mtu mwingine ni kutoingia kwenye mahusiano ama ndoa hapo utapuyanga hata ukeshe klabu hakuna wa kukuuliza.
 
Back
Top Bottom