Kuwa na mpenzi "mtoto" inahitaji ujasiri sana

Unafanya hivo usha yapatia maisha, ila kama ndo wale wa ukiumwa unaanza kusumbua ndugu michango, hapo utaangukia pua
 
Meridah uko vizuri acha moyo wako usukume damu tu mengine yote waachie wengine
 
Umefanya vema kuachana na huyu kijana asiyejitambua, ungeendelea kuishi na huyu jamaa angekuumiza moyo au hata pengine ungekuja kujiua kwa presha ya mapenzi.
 
Binafsi ninapokuwa nadate na mtu mara zote huwa namuuliza tupoje pale napoanza kuona mapicha picha ili nijue upande niliopo.
 
Kwa kifupi kakuacha ila hakutaka kukutamkia ili uachie ngazi mwenyewe...

Kupanga ni kuchagua na yeye amepanga akachagua kuwa baba wa mtoto huyo wa hiyo pesa utatuma hutumi!

Au ninasema uongo ndugu zangu?
 
Huyo alidhamiria kuacha tu wala hamna lingineπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Swali rahisi tu, unadhani huko uendako ndo utakutana na mwanaume ambaye ha-cheat? Tuliza hasira zako bi dada, kaa na mwenzako mueleze na kumbushe yapi yalikuwa malengo yenu!
Atakutana nae wapo wengi tu ila ndio hela hawana 😁😁😁 mwenye kazi lazma awe na micheps
 
inaonekana bado unampenda sana alafu yeye hakupendi kama wewe unavyompenda
 
Mara kapanga chumba kimoja, mara starehe mara hajielewi!
Huyo jamaa anajielewa sana ila ukweli ni kwamba hakupendi.
Siwezi kulazimisha kuwa labda ananipenda, hilo jibu analo yeye na moyo wake.
Lakini kitu ambacho ninakiongelea hapa ni zaidi ya chumba kimoja Mkuu. Vijana wengi wanaridhika na kitu kidogo na wanajisahau kupiga hatua. Kama yeye anajisahau sana. Tatizo sio chumba ila kutimiza plan ambazo mtu anaziweka. Kutoka hapa kwenda pale. Sio kwa sababu umeanza kutambaa basi as long as unaweza kwenda hapa na pale, inatosha. Hapana. Utahitaji kubeba sahani ya chakula, utatembea vipi ukiwa unatambaa. Hopful you are old enough to understand what l mean.
 
Sawa pole ila umekosea kumuita mtoto halafu ukataja miaka 31 kuna wengine wamekuwa kiakili.

Kiufupi nimegundua huwenda wewe ni mkubwa kwake ama la basi hakupendi tu.
 
Kwa kifupi kakuacha ila hakutaka kukutamkia ili uachie ngazi mwenyewe...

Kupanga ni kuchagua na yeye amepanga akachagua kuwa baba wa mtoto huyo wa hiyo pesa utatuma hutumi!

Au ninasema uongo ndugu zangu?
Bora ukweli mkuu
 
Sawa pole ila umekosea kumuita mtoto halafu ukataja miaka 31 kuna wengine wamekuwa kiakili.

Kiufupi nimegundua huwenda wewe ni mkubwa kwake ama la basi hakupendi tu.
Sababu hana misimamo kama mwanaume. Hata leo ananitumia ujumbe kunilaumu kwanini simtafuti wakati jana tumekubaliana kila mtu ashike lake, anajisahaulisha. Namwitaje mkubwa sasa ingawa yeye ni mkubwa kwangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…