Kuwasili kwa treni ya abiria jijini Arusha kwa mara ya pili baada ya miaka 30

Kuwasili kwa treni ya abiria jijini Arusha kwa mara ya pili baada ya miaka 30

Udukumani kuna kila kitu. Kama train ipo, meli zipo, ndege zipo, magari yapo, dhahabu ipo, almasi ipo, Jiji lipo, wanawake wazuri wenye miguu kama chupa ya bia wapo, wasomi wapo, ng'ombe zipo na Rais yupo. Je, una lingine?
Nikukumbushe Afrika ndo kwenye kila kitu lakini ss ni maskini wa kutupwa compared na mabara mengine,unahisi kwann?ukipata jibu tafakari ulichoandika.
 
Hebu nikumbusheni kidogo!Labda nilikuwa bado mdogo.Hivi serikali iliyokuwa madarakani kipindi hicho huduma za treni zinasitishwa kwa miaka 30 ilikuwa chini ya chama gani!Kama ilikuwa chini ya chama pinzani kwa kweli ccm wanastahili pongezi kurejesha tena huduma hizo.
CCM watu wa ajabu Sana,train kipindi Cha mkapa,mwinyi,JK ilikuwepo hawakuikarabati.Leo wenyewe wanaikarabati kwa Kodi za wananchi wanashangia mbona hamkuikarabati kabla? Mlikuwa wapi?pesa mlikuwa mnapeleka wapi?
 
Nimeangalia nguvu na majivuno ya jana kuhusu uzinduzi wa gari moshi la kutoka Dar - Kili- Arusha. Nikawa na maswali mengi kichwani. Hivi CCM hii treni ni ya Chama au ni ya Umma wa Watanzania?

Hivi leo mnapojisifu ni serikali ya chama gani iliua hii reli? Maana Mzee Ndesa (RIP} alipiga kelele sana kuhusu hii reli kwa maendeleo ya kanda ya kaskazini lakini Ccm na serikali yenu mliweka pamba masikioni.

Tuna kumbuka Ccm kupitia kwa mwenyekiti mlituambia mnaendeleza mikoa iliyo achwa nyuma na kwamba mikoa ambayo haikuwapa kura isahau maendeleo. Najiuliza, mmekumbuka nini huko kaskazini hadi mtumie nguvu za kichama kuzindua reli ya umma? Je, mmesha malizana na mikoa iliyo wapa kura?

Eleweni kama kuna mnao wadanganya kwamba CCM isipochaguliwa hakuna maendeleo sio ukanda huo.. Lami waliiona kabla ya uhuru, shule za mkoa wa Kilimanjaro pekee ni nyingi kiliko za mikoa mingine yote ya Tanzania kwa ujumla. Watu walisoma kwa nguvu za wazazi wao na sio elimu bure. Hivyo Mr Slow elewa una deal na watu wa aina gani?

Chief Mareale alipo enda UNO aliomba uhuru wa kanda ya kaskazini kwamba wako tayari kujitawala. Mwambie Meko kati ya kosa kubwa alilo fanya miaka yake mitano ni kuwabagua watu wa kaskazini. Na kumuonyesha hawajali hakuna alie lalamika.

Siku zaja historia itajiandika..
 
Nafananisha treni kufika Arusha Kama rushwa ya uchaguzi, nafananisha polepole kwenda Arusha kwa tren Kama mtoa rushwa ya uchaguzi.

Njia pekee yakupinga rushwa kipindi hiki cha uchaguzi na kuacha kupokea na hata ukilamishwa unachukua ila kura inapelekwa kwa kwa wenye kusimamia maslahi yao.

Tujiulize polepole lini alienda kwao na treni? Lini viongozi wa ccm walisafiri toka dar to arusha hata kwa bus licha treni?

Kibaya zaidi treni inaelezwa kujaa bia Kama vile kiu ya wa Arusha Ni bia na siyo maendeleo. Nawashukuru leo mmeonyesha kwamba bia za treni hazina ladha tofauti, mmeonyesha ninyi siyo wakuongwa treni. Nadhani huku kwetu mwanza tutahoji ilipo tumbaku na pamba, tutahoji yalipo masangara na masato yanayopakiwa ndege...tunawasubiri wabeba maono
 
Back
Top Bottom