Kuwasili kwa treni ya abiria jijini Arusha kwa mara ya pili baada ya miaka 30

Kuwasili kwa treni ya abiria jijini Arusha kwa mara ya pili baada ya miaka 30

Leo Jumatatu Shirika la reli linafanya majaribio ya safari za treni ya abiria toka Moshi kwenda Arusha. Mgeni mualikwa ni katibu mwenezi wa ccm Humphrey Polepole.

Nimejiuliza tu kumbe TRC ambalo ni shirika la umma, ni wakala wa CCM siku hizi?...
Kwani CCM siyo mali ya watanzania ?
 
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM ndugu Polepole leo anazindua Huduma ya usafiri wa treni kati ya Moshi na Arusha.

Mkoa mzima umetulia kimya na watu wote wameelekea stesheni kushuhudia treni ya kwanza ya TRC iliyobeba makada wa CCM ikianza safari ya kihistoria.

Chanzo: Channel ten.

Maendeleo hayana vyama!
Kwahiyo kutoka Dar mpaka Arusha ni treni? Price Tsh ngapi?
 
Mtapanda tu. Usilete kejeli wewe
Moshi kwenda Arusha wananchi wanatumia coaster bus TSH 3,000 kwa kutumia masaa 1.30 kuingia arusha.sasa train kutoka Moshi kwenda Arusha itatumika masaa 4 Nani wa kuisubiri? Itapalia abiria kwa TSH 330 au?
 
Hizo ni ndoto za mchana. Na ukiona unaota mchana ujue karibu utakuwa chizi
Apande huyo slow slow na mke wake!

Na mwisho wao wa kukaa uraiani ni pale Lissu akiapishwa kuwa rais, haya makando kando yote waliyoyafanya ccm yatawacost
 
Hata mimi naamini iko siku wapinzani watachukua nchi lakini si kizazi hiki cha sasa. Labda mwaka 2045
Siasa za kishamba Sana. Swali langu Ni moja tu Hivi nikweli wanaamini watatawala milele bila kupigwa chini?? Siku itafika ujanja ujanja wote utaisha kwa kuwa Hakuna kitu Cha kudumu maishani hata uhai wetu Ni wa muda TU sembuse utawala!!? Nachofurahi wajinga wengi wameamka usingizini.
 
Wachagga siyo wapumbavu kiasi cha kwenda kushangaa ujinga bwashee!

Yani mangi aache kuchoma nyama, manka aache kupeleka ndizi kiboriloni aende kumshangaa ki-homo eractus kutoka zama za mawe kati kikizindua garimoshi lililokuwapo miaka ya nyuma kisha wakaliua hao hao wanaodai kulizindua Leo?
Kwani Kilimanjaro wanaishi Wachagga tu?
 
Wameamka kwa lipi mbona ni washamba tu
Wapendwe kwa hiyo treni outdated Kaka! Watu wa huko wameamka miaka mingi nyuma. Mtu aache kusafiri na Youtung lenye AC ndani kwa muda mfupi, apakie treni la masaa 18 Ms-Dar? Halafu kupendwa ni kitu automatic na sio kwa vitu. Kuna mwanamke nilikuwa nampenda balaa hapo mlimani, kanilia sana hela zangu, lakini alikuwa anampenda muhuni wake muuza mitumba hapo Mwananyamala, tena muhuni mwenyewe alikuwa hapo kitu.

Hao wanaoipenda ccm wataendelea kuipenda, ila wanaopenda upinzani wataendelea hata wakifungiwa mabomba ya maziwa ndani. Usitegeemee Simba ikichukua makombe, basi mashabiki wa Yanga wataipenda.
 
Udukumani kuna kila kitu. Kama train ipo, meli zipo, ndege zipo, magari yapo, dhahabu ipo, almasi ipo, Jiji lipo, wanawake wazuri wenye miguu kama chupa ya bia wapo, wasomi wapo, ng'ombe zipo na Rais yupo. Je, una lingine?
na heri huo ujinga angefanya ukanda wa wasukuma huko kaskazini anapoteza muda wake tu
 
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM ndugu Polepole leo anazindua Huduma ya usafiri wa treni kati ya Moshi na Arusha.

Mkoa mzima umetulia kimya na watu wote wameelekea stesheni kushuhudia treni ya kwanza ya TRC iliyobeba makada wa CCM ikianza safari ya kihistoria.

Chanzo: Channel ten.

Maendeleo hayana vyama!
Nalisikia ndio linaingia Arusha town saa hii na honi kama zote.
 
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM ndugu Polepole leo anazindua Huduma ya usafiri wa treni kati ya Moshi na Arusha.

Mkoa mzima umetulia kimya na watu wote wameelekea stesheni kushuhudia treni ya kwanza ya TRC iliyobeba makada wa CCM ikianza safari ya kihistoria...
Hongera sana Magufuli kwa kweli,unastahili sifa zote.Mmm,Nyerere,Mwinyi,Mkapa na Kikwete waliturudisha nyuma sana kwa kweli.Hii ni hukumu kwao wote, popote walipo, hata kama sio ya mahakamani.
 
Ndio maana nimepita maeneo ya ushirika na kwa mr price kinyaa watu hakuna. Jamaa a yangu yupo Uchira anasema wamekodi Coaster kwenda kuishangilia treni. Ccm hoyeeee
Duh! mr price imefungwa zamani!!!!! huko Moshi wewe
 
Back
Top Bottom