Kuweka Records Sawa: Utaratibu alioupendekeza Shabiby ndio uliokuwepo kabla, Haufai


Kwanini asipewe nafasi kwa anachokisema akawa proved wrong?

Mbona nyungu, bupiji na NIMRICAF tulizipa nafasi hizo?

Mbona Masudi Kupanda na gari lake alipewa nafasi hiyo?

Mbona hata Prof. Manyele na kamati ya vinyesi walipewa nafasi?

Yaonesha wapigaji wamejipanga kutokuwa proved wrong.
 
Kwa akili yako unamuamini Shabiby kuwa kweli kuna mafuta ya robo ya bei tunayopata sasa?

Kwanini asiwe proved wrong kwa vitendo bali mmekomalia maneno tu? Haya si ndiyo ya akina Manyele?



Kwani nani walimwamini Masudi Kipanya na ndinga lake?
 
πŸ˜‚πŸ˜‚ kupunguza bei za mafuta kwa 50% ya bei za sasa...."Only in Tanzania "πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Sababu nyingi zinaweza kusababisha mshtuko wa bei ya mafuta. Zinajumuisha mabadiliko makubwa katika mahitaji au usambazaji popote ulimwenguni, kwani mafuta ni bidhaa ya kimataifa.
Mishtuko pia inaweza kutokana na;
●vita,
● mapinduzi ,
●vipindi vya ukuaji wa haraka wa uchumi katika mataifa makubwa yanayoagiza bidhaa kutoka nje,
● matatizo ya ndani katika nchi wasambazaji bidhaa, kama vile migogoro ya kisiasa au ukosefu wa uwekezaji katika sekta ya mafuta.
 
Ushauri wa bure kabisa. Alichokisema shabib mbunge na anacho kiapo cha kikatiba. Kiundiwe kamati kifanyiwe kazi haraka haraka kisha wajiridhishe fact ni zipi iwasaidie kuamua. Wasimpuuze hata kidogo. Nchi hii ni yetu sote. Kama serikali inashauriwa jambo zuri ilipokee kwa mikono miwili. Tuacheni mambo ya kujiona tumemaliza kila kitu. Maana wengine wakishakuwa na mamlaka huona wengine hawawezi kiwashauri au kuwaambia lolote. Uteuzi hufikia mwisho na utumishi pia hukoma.
 
Mzee Magufuli alilipenda sana hili taifa. Nimesoma hoja/challenges za ununuzi holela na BPS nashawishika kusema BPS ilikuwa muhimu kuanzishwa
 
Kwanini kuandikia mate? Kwanini umeng'ang'ania kuandikia mate? Kwamba bei hazitashuka kwa ubora ule ule kwani wewe ni Kerubi?
Ukitumia common sense vizuri utaona analosema shabbiby haliwezekani, bei kushuka kwa 50% maana yake ni kuwa mafuta yauzwe sh 1400 kwa lita ya diesel!! Bei hii haipo kokote duniani, Epra Kenya ambao ndio leguratory board kama ilivyo ewura kwetu , wametangaza bei mbaya sana kwa mafuta kwa mwezi huu huko kenya
 
Mzee Magufuli alilipenda sana hili taifa. Nimesoma hoja/challenges za ununuzi holela na BPS nashawishika kusema BPS ilikuwa muhimu kuanzishwa
BPS ilianza mwishoni mwa utawala wa kikwete
 
Kama Shabiby kuna chimbo la mafuta ya bei chee, kwa nini asiishauri serikali ikanunue huko? Huo ndio uzalendo kwa Taifa, sio ujanja ujanja wa kutaka kufaidika mwenyewe
 
Shabiby anaongea point, katika yote watakayoongea mwisho wake sisi tunataka kuona mafuta yamepungua bei ifikie ile wakati magufuri yupo 1600-200/l

Ile ilikuwa sababu ya corona viwanda vilifungwa na nchi nyingi zilikuwa kwenye lockdown kwahiyo mahitaji yalipungua.
 
Hiki ulichokiandika, kama mafuta ni 2,830/- kwa lita moja, kwa Dar, HAKINA MAANA
 

Ninakazia: Shabiby awe proved wrong kwa vitendo si kwa maneno vinginevyo ni porojo tu!
 
Monopoly ya nini? Dogo ruhusu biashara huru na wewe Tpdc + ewura pambana na wenzio, tutanunua kwa mwenye bei ndogo
 
Kwanini bei isingeendelea kuwa ile ile kwa siku 27 usiache kwanza ambayo yalinunuliwa kwa bei ya chini?
asante mkuu πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™. Kwa kweli kuna hoja hapo.
Mzigo wa zamani upo wa kutosha siku 27, mzigo mpya usubiri kwanza huu uishe ndo tubadilishiwe bei .
Mbona duniani huko bei ikishuka huku hawashushi kwa kisingizio et kuna mzigo wa zamani mwingi .EWURA litazameni hili .
 
Utaona kabisa namna wafanyabiashara wanavyofanya lobying kwa wawakilishi wetu ili kutimiza azma zao.
 
Utaona kabisa namna wafanyabiashara wanavyofanya lobying kwa wawakilishi wetu ili kutimiza azma zao.

Wakifanya lobbying tukapata mafuta safi na kwa bei nafuu Kwanini nyie inawauma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…