Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 95,871
- 116,627
Sababu ya kodi kibaoKupanda kwa mafuta asilimia kubwa imesababishwa na serikali yenyewe
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sababu ya kodi kibaoKupanda kwa mafuta asilimia kubwa imesababishwa na serikali yenyewe
Sasa anashindwaje kuleta mafuta ya bei chee hata sasa? Mfumo wa BPS unashindanisha kampuni zote interested kuingiza mafuta na unatoa tenda kwa kampuni iliyo na bei ya CHINI kupita zote. Kwa akili za kawaida hapo Shabiby anazuiwa vipi kampuni yake kuomba kwa bei ya chini (lowest bidding price) ili kuingiza mafuta kwa bei ya chini? Kwanini kwenye mchango wake hakuelezea sababu za serikali kuachana na mpango wa zamani (anaoupendekeza) na kuingia kwenye mpango mpya?
Kwa akili yako unamuamini Shabiby kuwa kweli kuna mafuta ya robo ya bei tunayopata sasa?Anakuwa je mpigaji kupendekeza msingi wa kupunguza bei kufikia 50%?
Kama huo ni upigaji kwa hakika huo ndiyo tunaoutaka!
Kwa akili yako unamuamini Shabiby kuwa kweli kuna mafuta ya robo ya bei tunayopata sasa?
Ukitumia common sense vizuri utaona analosema shabbiby haliwezekani, bei kushuka kwa 50% maana yake ni kuwa mafuta yauzwe sh 1400 kwa lita ya diesel!! Bei hii haipo kokote duniani, Epra Kenya ambao ndio leguratory board kama ilivyo ewura kwetu , wametangaza bei mbaya sana kwa mafuta kwa mwezi huu huko kenyaKwanini kuandikia mate? Kwanini umeng'ang'ania kuandikia mate? Kwamba bei hazitashuka kwa ubora ule ule kwani wewe ni Kerubi?
Mzee Magufuli alilipenda sana hili taifa. Nimesoma hoja/challenges za ununuzi holela na BPS nashawishika kusema BPS ilikuwa muhimu kuanzishwa
BPS ilianza mwishoni mwa utawala wa kikweteMzee Magufuli alilipenda sana hili taifa. Nimesoma hoja/challenges za ununuzi holela na BPS nashawishika kusema BPS ilikuwa muhimu kuanzishwa
Shabiby anaongea point, katika yote watakayoongea mwisho wake sisi tunataka kuona mafuta yamepungua bei ifikie ile wakati magufuri yupo 1600-200/l
Hiki ulichokiandika, kama mafuta ni 2,830/- kwa lita moja, kwa Dar, HAKINA MAANAWakuu Kwema?
Mimi kwa kiasi fulani ni mdau wa mafuta, kwani hapo kabla miaka ya nyuma nilishawahi kufanya kazi katika kampuni ya mafuta Kwa kama miaka kadhaa Hivi
Hivi karibuni Mbunge wa Gairo Bw. Ahmed Abdallah Shabiby amependekeza kua ili Bei ya mafuta iweze kushuka basi Serikali iruhusu Wafanyabiashara binafsi waagize mafuta hayo.
Napenda kuweka taarifa sawa tu kua Utaratibu huu anaoupendekeza Bw. Shabiby utumike ndio uliokuwepo hapo awali. Serikali ilikuja kuubadilisha huu utaratibu kutokana na sababu au mapumgufu yake kadhaa, na chache nitazitaja hapa chini.
Kwanza ni ku avoid "Transfer Pricing". Yaani kampuni A iliyopo Tanzania ni tawi la Kampuni B iliyopo labda S.A. Sasa kampuni B ndio inayonunua mafuta inakokujua kisha inaiuzia kampuni A ya hapa nchini kwa bei kubwa kuliko bei ya soko.
Sasa kampuni A ya hapa katika hesabu zake za kodi ya faida 30%x (Mapato - Matumizi) inajikuta inalipa kodi kidogo sababu gharama za uendeshaji zimekua kubwa kutokana na gharama kubwa za manunuzi ya mzigo. Kwa mtindo huu kampuni zingine hufikia hata kuandika wamepata hasara (Manunuzi + Gharama zingine vimezidi Mapato). Kifupi kampuni hukwepa kodi kwa kusingizia gharama kubwa za manunuzi kumbe humo humo anapomlipa Kampuni Mama na faida au dividend anasafirishia hapo hapo kinyemela.
Sababu ya pili Mpaka Serikali ikaondoa utaratibu huu ni kufaidi "Discount on Bulk Purchases". Yaani kampuni 10 zikinunua labda lita million 10 kila moja ni tofauti na kampuni moja ikinunua lita 10mil x 10 = Lita 100mil. Huyu anaenunua lita nyingi ni rahisi ku bargain na kupewa Discount kubwa tofauti na yule anaenunua kidogo. Discount hiyo hupelekea unafuu wa bei Mwishowe kwa finale user.
Tatu ni kua na records za mafuta yaliyoko nchini. Yaani soko likiwa holela kila mtu anaagiza mnaweza kushindwa kujua hata mahitaji ya nchi kwa kipindi husika ni kiasi gani. Hii pia huwezesha Serikali kukadiria (bajeti) Kodi itakayokusanywa kutokana na mafuta haya.
Nne ni kupata bidhaa iliyo bora na standard. Kutokana na Bei mbalimbali zinazosababishwa na ubora mbalimbali basi wengine wanaweza kuchukua au kuagiza hata yale yenye ubora wa chini sababu tu ya unafuu wa bei bila kujali athari zake kwenye matumizi yake. Standard hapa ni viwango vifanane kati ya kampuni moja na ingine. Kusiwe na tofauti kati ya anaejazia BP/Puma au yule anaejazia Oilcom (Ceteris Peribus).
Tano ni kuondoa mafuta ya magendo kwenye soko. Since Mnunuzi wa kutoka nje atakua ni mmoja tu na ndie atakaewasambazia Makampuni ya ndani then kunapunguza uwezekano wa mafuta mengine yasiyolipiwa ushuru kuingia kwenye soko.
Sita, Kwa kuagiza pamoja kunaleta uniformity kwenye Bei. Ingawa Labor na Other Overhead Expenses zaweza kua tofauti lakini bei ya kununulia bidhaa ambayo ndio huchukua sehemu kubwa ikiwa sawa basi Bei hazitapishana sana. Ingawa bei Hupangwa na Ewura lakini kipindi hicho huu utaratibu unawekwa ni Makampuni yenyewe yalikua yanajipangia Bei baada ya kukukokotoa Gharama mbalimbali za kuanzia Manunuzi na Undeshaji pia.
Saba, Kuzuia kuficha mafuta. Kampuni zingeweza kusema hazina mafuta (lower supplies) ili kutengeneza Demand kubwa then bei zipande. Lakini since uagizaji na/kisha ugawaji wa mafuta hufanywa Kwa pamoja then ni rahisi kujua stock ya kila kampuni. Hivyo si rahisi kwa Kampuni husika kuficha taarifa za mafuta iliyo nayo.
Sababu zilikuwa nyingi, nimejaribu kukumbuka chache. Inawezekana mazingira ya wakati ule yangechochea tuhamie kwenye uagizaji wa pamoja labda sababu hizo sio valid anymore so turudi tu kule kule tena. Nimeona kama (nilieliekua) mdau wa mafuta basi nisikae kimya watu wafikiri kua hatujawahi kua katika huo utaratibu alioupendekeza Bwana Shabiby.
Muwe na Siku njema.
Ukitumia common sense vizuri utaona analosema shabbiby haliwezekani, bei kushuka kwa 50% maana yake ni kuwa mafuta yauzwe sh 1400 kwa lita ya diesel!! Bei hii haipo kokote duniani, Epra Kenya ambao ndio leguratory board kama ilivyo ewura kwetu , wametangaza bei mbaya sana kwa mafuta kwa mwezi huu huko kenya
Waambie Mkuu, wajinga wamejazana kumuabudu Magufuli mpaka wanajidanganyaBPS Ilianza wakati wa Kikwete.
Monopoly ya nini? Dogo ruhusu biashara huru na wewe Tpdc + ewura pambana na wenzio, tutanunua kwa mwenye bei ndogoWakuu Kwema?
Mimi kwa kiasi fulani ni mdau wa mafuta, kwani hapo kabla miaka ya nyuma nilishawahi kufanya kazi katika kampuni ya mafuta Kwa kama miaka kadhaa Hivi
Hivi karibuni Mbunge wa Gairo Bw. Ahmed Abdallah Shabiby amependekeza kua ili Bei ya mafuta iweze kushuka basi Serikali iruhusu Wafanyabiashara binafsi waagize mafuta hayo.
Napenda kuweka taarifa sawa tu kua Utaratibu huu anaoupendekeza Bw. Shabiby utumike ndio uliokuwepo hapo awali. Serikali ilikuja kuubadilisha huu utaratibu kutokana na sababu au mapumgufu yake kadhaa, na chache nitazitaja hapa chini.
Kwanza ni ku avoid "Transfer Pricing". Yaani kampuni A iliyopo Tanzania ni tawi la Kampuni B iliyopo labda S.A. Sasa kampuni B ndio inayonunua mafuta inakokujua kisha inaiuzia kampuni A ya hapa nchini kwa bei kubwa kuliko bei ya soko.
Sasa kampuni A ya hapa katika hesabu zake za kodi ya faida 30%x (Mapato - Matumizi) inajikuta inalipa kodi kidogo sababu gharama za uendeshaji zimekua kubwa kutokana na gharama kubwa za manunuzi ya mzigo. Kwa mtindo huu kampuni zingine hufikia hata kuandika wamepata hasara (Manunuzi + Gharama zingine vimezidi Mapato). Kifupi kampuni hukwepa kodi kwa kusingizia gharama kubwa za manunuzi kumbe humo humo anapomlipa Kampuni Mama na faida au dividend anasafirishia hapo hapo kinyemela.
Sababu ya pili Mpaka Serikali ikaondoa utaratibu huu ni kufaidi "Discount on Bulk Purchases". Yaani kampuni 10 zikinunua labda lita million 10 kila moja ni tofauti na kampuni moja ikinunua lita 10mil x 10 = Lita 100mil. Huyu anaenunua lita nyingi ni rahisi ku bargain na kupewa Discount kubwa tofauti na yule anaenunua kidogo. Discount hiyo hupelekea unafuu wa bei Mwishowe kwa finale user.
Tatu ni kua na records za mafuta yaliyoko nchini. Yaani soko likiwa holela kila mtu anaagiza mnaweza kushindwa kujua hata mahitaji ya nchi kwa kipindi husika ni kiasi gani. Hii pia huwezesha Serikali kukadiria (bajeti) Kodi itakayokusanywa kutokana na mafuta haya.
Nne ni kupata bidhaa iliyo bora na standard. Kutokana na Bei mbalimbali zinazosababishwa na ubora mbalimbali basi wengine wanaweza kuchukua au kuagiza hata yale yenye ubora wa chini sababu tu ya unafuu wa bei bila kujali athari zake kwenye matumizi yake. Standard hapa ni viwango vifanane kati ya kampuni moja na ingine. Kusiwe na tofauti kati ya anaejazia BP/Puma au yule anaejazia Oilcom (Ceteris Peribus).
Tano ni kuondoa mafuta ya magendo kwenye soko. Since Mnunuzi wa kutoka nje atakua ni mmoja tu na ndie atakaewasambazia Makampuni ya ndani then kunapunguza uwezekano wa mafuta mengine yasiyolipiwa ushuru kuingia kwenye soko.
Sita, Kwa kuagiza pamoja kunaleta uniformity kwenye Bei. Ingawa Labor na Other Overhead Expenses zaweza kua tofauti lakini bei ya kununulia bidhaa ambayo ndio huchukua sehemu kubwa ikiwa sawa basi Bei hazitapishana sana. Ingawa bei Hupangwa na Ewura lakini kipindi hicho huu utaratibu unawekwa ni Makampuni yenyewe yalikua yanajipangia Bei baada ya kukukokotoa Gharama mbalimbali za kuanzia Manunuzi na Undeshaji pia.
Saba, Kuzuia kuficha mafuta. Kampuni zingeweza kusema hazina mafuta (lower supplies) ili kutengeneza Demand kubwa then bei zipande. Lakini since uagizaji na/kisha ugawaji wa mafuta hufanywa Kwa pamoja then ni rahisi kujua stock ya kila kampuni. Hivyo si rahisi kwa Kampuni husika kuficha taarifa za mafuta iliyo nayo.
Sababu zilikuwa nyingi, nimejaribu kukumbuka chache. Inawezekana mazingira ya wakati ule yangechochea tuhamie kwenye uagizaji wa pamoja labda sababu hizo sio valid anymore so turudi tu kule kule tena. Nimeona kama (nilieliekua) mdau wa mafuta basi nisikae kimya watu wafikiri kua hatujawahi kua katika huo utaratibu alioupendekeza Bwana Shabiby.
Muwe na Siku njema.
asante mkuu 🙏🙏🙏🙏🙏. Kwa kweli kuna hoja hapo.Kwanini bei isingeendelea kuwa ile ile kwa siku 27 usiache kwanza ambayo yalinunuliwa kwa bei ya chini?
Utaona kabisa namna wafanyabiashara wanavyofanya lobying kwa wawakilishi wetu ili kutimiza azma zao.