Kuwekwa kwa somo ya Kiislamu kwenye Tahasusi kunaashiria nini?

hilo ni somo kama somo lingine lazma walipwe.pia lina faida katika kujenga maadil ndani ya jamii.
 
Mbona hujajibu maswali Mengine?
Hiyo ni Imani, Ideology ( unamprogram mtu ) hilo sio somo la kawaida.

Maadili?
So, mmomonyoko wa maadili ni kwa kuwa hatuna somo la kiislam kama somo rasmi?
bila shaka kizazi kinatpotea kwa kukosa mafunzo ya maadili.na uislam unafundisha hayo maadili.acha chuki.
 
Hilo somo la physical education lipo katika nchi jirani,au lipo kimataifa,au tunakuwa corrupted na soccer?
 
bila shaka kizazi kinatpotea kwa kukosa mafunzo ya maadili.na uislam unafundisha hayo maadili.acha chuki.
Chuki iko wapi mkuu?
Kwanini nikuchukie wewe au yeyote yule?
Ntapata nini nikikuchukia.
Serikali ( isiyo na dini ) inatumia kodi za wananchi ( wa dini zote) kufundisha ideology fulani ( ambayo sio wananchi wake wote wanaiamini).
Hichi ni kichekesho.
Mnataka hao watoto ( mnaowaprogramm tangu wakiwa wadogo) waje kuwa kina nani?
Mnatengeneza taifa la wafanya mihadhara?
 
Umeeleweka KAFIRI,chuki yako dhidi ya uislamu ni kubwa mno
 
Kwani hiyo "tahasusi" unayoiongelea ni lazima mtu asiyeitaka aisome?
 
Jiandaeni huko mbeleni tenda au Ajira za Bandari zitakuwa na kifungu hiki: Knowlege of Islamic and Arabic Language will be an added advantage
Siyo "mbeleni" Hata sasa ni advantage kubwa sana kwenye banking Industry toka zilipoanzishwa Islamic Bnking na kutapakaa duniani. Pia kama ulivyoona kuna Takaful ambayo ni Islamic Insurance imeshaanza kutapakaa duniani.

kama hayo hayatoshi, Wizara ya mambo ya je ni advantage kubwa sana masomo hayo Pia UWT, tena UWT ukiwa na masomo hayo unatafutwa wewe, hutafuti kazi. Hiyo ni dunia nzima.

Kwanini ubaki nyuma?
 
Wanataka wawe na watu competent wakufanya mihadhara tu kuzodoa dini zingine.

Wanatengeneza wafia dini kwa ajili ya kumnusuru Allah
 
bila shaka kizazi kinatpotea kwa kukosa mafunzo ya maadili.na uislam unafundisha hayo maadili.acha chuki.
Unajua inabidi tufike sehemu tutofautishe “state” and “religion”. Wanaohoji wana haki maana asilimia 4 ya mapato ya muungano huenda Zanzibar. Pia katiba ya Jamhuri ambayo ni katiba mama ina elimu ya juu kama suala la Muungano. Kuchukua hela yangu kumlipa mwalimu wa dini wa upande mmoja ni kosa.
Kama ambavyo leo Bible knowledge ni option huku kwingine hiyo Islamic religion ingekua option. Anayeisoma ajigharamikie mwenyewe. Hapo tutakua na state sponsored religion. Sio haki.
 
Hizo combi si zipo Zanzibar tu, ss ww inakuuma nn ingekuwa zipo na bara Sawa. Hapo cha kufanya ili usiendelee kuumia peleka ombi wizara ya elimu ili waweke kombi za bible knowledge, hata wakristo wenyewe hawataki kuijua dini yao. Zanzibar wao wana imanı wanasoma uislamu mpk kwenye combi lkn ukiileta bara hakuna atakayetaka kusoma bible knowledge kila mtu atakimbilia kombi za PCB, PCM n.k ili baadae waje kuwa wapigaji
 
AMA KWELI LEO NDIO NIMEAMINI KUWA WATANZANIA WAPE KICHWA CHA HABARI TU MAELEZO YA HABARI WATAYASHUSHA WAO WENYEWE.

licha ya hivyo, mtoa mada kaweka na maelezo kabisa kuwa, Somo la islamic limeongezwa kwenye combination Kwa upande wa ZANZIBAR tu. Cha ajabu karibu asilimia 90 ya wachangiaji wanachangia kana kwamba Hilo Somo limeongezwa kwenye combination Kwa Tanzania bara.

Tambua vitu vifuatavyo Kwa upande wa ZANZIBAR hapo ndipo utaona umuhimu wa kuziweka Somo hili kwenye combination.

1. 95% ya wazanzibari ni waislamu na wanahimiza kuishi katika maadili ya muislamu.

2. Kutokana na wingi huo wa waislam na himizo la kufuata maadili ya uislam, Somo la EDK (elimu ya dini) inafundishwa kuanzia ngazi ya awali mpaka sekondari, na nilazima Kwa Kila mwanafunzi kulisoma.

3. Somo la EDK linafanywa na Kila mwanafunzi kwenye mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi na sekondari pia.

4. WALIMU wa EDK wanalipwa mshahara kutoka serikalini na Kila shule ina walimu hao na wanaajiriwa na serikali kama walimu wengine.

Mpaka kufikia hapo utaona jitihada kubwa inafanywa na serikali ya zanzibar kwenye Somo hili ambalo ndio msingi mkubwa maadili Kwa upande wao.

Kwa kuongezea, chuo kikuu Cha waislam wa morogoro kinatoa kozi kadhaa zinazohusisha Somo la islamic, kwahiyo lazima pawe na combination zitakazowapa fursa watoto kujiunga na kozi hizo.

Kuna vyuo vingi mpaka uingereza huko vinavyotoa kozi zinazohitaji mtu ambae kasoma islamic studies ngazi ya advance...hivyo wazanzibari watakuwa na fursa ya kusoma huko. Na sisi wabara huku tutakuwa na fursa hiyo Kwa kuwa Kuna baadhi ya shule za private Somo la islamic ni lazma Kwa Kila mwanafunzi kulisoma hata akiwa PCM ataongezea Somo la islamic studies.

Mpaka sasa Mimi sijaona tatizo la Somo la islamic studies kuwekwa kwenye combination Kwa upande wa ZANZIBAR kulinganisha na mfumo wa kimalezi na kimaadiki Kwa upande wao.

Wachangiaji wengi wamechangia wakisukumwa na chuki za kidini (dini ya muislamu)....imagine mtu anachukia mpaka Arabic language kuwekwa kwenye combination. Wakati ukienda pale taasisi ya lugha ya kiarabu Tanzania Kuna wakristo kibao (hasa wakenya waishio TZ) wanasoma lugha ya kiarabu. Inafikia hatua chuki inamtia mtu upofu mpaka anashindwa kutofautisha UISLAMU na KIARABU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…